Monday, January 14, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA SHULE YA SEKONDARI MLIMANI-MATEMWE, UNGUJA

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi (kulia) na Afisa mwandamizi  kutoka katika kitengo cha elimu katika ofisi ya Benki ya Dunia nchini, Bwana Nobuyuki Tanaka wakikata utepe wakati wa hafla ya ufunguzi wa Shule ya Sekondari ya Mlimani  Matemwe huko Zanzibar jana. Shule hiyo imejengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Benki ya Dunia.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia vitabu vya masomo katika maktaba ya shule mpya ya Sekondari ya Mlimani Matemwe muda mfupi baada ya kuifungua rasmi jana. Kulia ni Ofisa mwandamizi kutoka ofisi ya Benki ya Dunia nchini anayeshughulikia masuala ya elimu Bwana Nobuyuki Tanaka na kushoto ni Mwalimu mkuu wa Shule hiyo, Mohamed Mzee Choum.
(PICHA NA FREDDY MARO / IKULU)

No comments: