Taarifa za uhakika ni kwamba kweli mwigizaji Sajuki amefariki dunia leo asubuhi (Jan 2, 2013) katika hospitali ya Muhimbili.
Amelazwa hapo kwa wiki mbili ambapo alikua anasubiri kupata urahisi wa kusafiri kurudi India kwenye matibabu ambayo alipangiwa kurudi tena December 2012.
Dinno ambae ni rafiki wa karibu wa Sajuki ameiambia millardayo.com kwamba tatizo kubwa lililomzuia Sajuki kurudi India ni pumzi ambapo walikua wanatafuta ndege yenye huduma ya gesi.
Baada ya kuhangaika sana, dakika za mwisho ndio walikua wamepata ndege ambayo imekubali kutoa huduma ya gesi kwa Sajuki ambapo Shirika la ndege la Emirates ndio lilikua limekubali kutoa huduma hiyo.