Friday, April 12, 2013


NATASHA ASENGENYWA NA WASANII WENZAKE


Mkongwe wa filamu nchini, Suzan Lewis ‘Natasha’ hivi karibuni alisengenywa na wasanii wenzake wakidai kuwa, amewashonea madira ya Kanumba Day ambayo hayaendani na gharama waliyolipia.

Suzan Lewis ‘Natasha’.

Wasanii hao wakiwa kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar alikozikwa Kanumba walisikika wakilalamika kuwa, Natasha amewaingiza chaka kwa madira hayo ambayo siyo ya shilingi 35,000 walizotoa.
“Jamani mbona hizi nguo haziendani na pesa tuliyoitoa? Hivi haya ni madira ya elfu 35 kweli?” alianzisha msanii mmoja wa kike aliyeungwa mkono na wenzake.
Badaa ya kunasa malalamiko hayo, mwandishi wetu alimpigia simu Natasha ili kujua ukweli juu ya tuhuma hizo ambapo alisema: “Ukweli wasanii wenzangu nimewazoea kwa hiyo hata sishangai, nililitegemea hilo.

No comments: