Friday, April 12, 2013

RAS MAKUNJA=ASKARI WA KUTULIZA GHASIA!-KUTOKA KWA ANKAL

Kijiji cha Mkoka wilayani Kongwa Mkoa wa Dodoma kina mbwa wengi sana. Mmoja wao alikatisha katikati ya kadamnasi leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi wa ukarabati wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Shirika la Mfuko wa Changamoto za millenia (MCC) ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Mradi huo utanufaisha jumla ya vijiji 16 vya Dodoma kuwa na umeme wa uhakika. Baada ya kuona mbwa huyo akielekea jukwaa kuu, Ras Makunja mmoja akajitokeza na kuzuia tafrani ambayo ingejitokeza endapo mbwa huyo angetinga jukwaa kuu...
Akionesha ukakakamavu wa hali ya juu Ras Makunja huyo aliweka mambo sawa kwa kumwelekeza mbwa huyo kwengineko. Ni tukio la sekunde tatu lakini Kamera ya Globu ya Jamii iliweza kurekodi kila hatua kama inavyoonekana....
Mbwa mwenyewe ndio huyu hapa....

No comments: