Wednesday, April 3, 2013


Stori: Mwandishi Wetu
Mtangazaji wa Kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Radio, Loveness Malinzi ‘ Diva’ juzikati amefunguka kuwa, kosa kubwa alilowahi kulifanya kwenye maisha yake ni kummegea penzi mwanamuziki anayefahamika kwa jina la Mo Racka.
Diva alifunguka hayo ikiwa ni mara ya pili baada ya kufanya hivyo mwaka jana kupitia mtandao wa Twitter ambapo aliandika : “Kutoka kimapenzi na Mo Racka ni kosa kubwa ambalo nimelifanya, nilikuwa mdogo na nilitokea kumpenda mvulana mtanashati Dar, na kila msichana aliyekuwa akituona aliishia kusema ‘Mungu wangu’, ilikuwa balaa. Hata hivyo, sasa hivi tuko poa na ni marafiki sana.”
Diva aliwahi kuwa kwenye uhusiano na kijana huyo na inasemekena kila mmoja alikuwa kamzimia mwenzake ndiyo maana haupiti muda mrefu mmoja kati yao lazima atakumbushia enzi zao.

No comments: