Friday, May 17, 2013


DAVID BECKHAM AFUATA NYAYO ZA KIBABU FERGIE NA SCHOLES, ATANGAZA KUSTAAFU SOKA MWISHONI MWA MSIMU HUU!!


Waving goodbye: David Beckham will retire from football after 20 years at the top 
KWAHERI SOKA: David Beckham atatundika dalagu baada ya kucheza soka kwa muda mrefu 
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Dili la kustaafu lazidi kuitikisa nchi ya Uingereza baada ya magwiji wa soka na kocha maarufu kustaafu kufundisha soka.
 Wiki moja baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson, Paul Scholes, leo hii mchezaji wa zamani wa Man United na nahodha wa zamani wa England DAVID BECKHAM ametangaza kutundika daluga.
Beckham mwenye umri wa mika 38, ameisadia Paris Saint-Germain PSG Kutwaa mwari wa Ligue 1 nchini Ufaransa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 19 mwishoni mwa wiki iliyopita
Pamoja na kupewa ofa ya mkataba mpya na timu hiyo ya Ufaransa, mkongwe huyo atastaafu baada ya mchezo wa mwisho tarehe 26 mwezi huu .
Alisema: “Shukrani sana kwa PSG kwa kunipa nafasi ya kuendelea kuwa hapa lakini sasa nadhani ni muda sahihi wa kustaafu, kucheza kwenye soka la kiwango cha juu”
Beckam alianza kucheza akiwa na Manchester United, akifunga mabao 85 katika mechi 394, kabla ya kuhamia Real Madrid. Aliondoka Spain kwa uhamisho mnono kujiunga na LA Galaxy mwaka 2007 pia aliwahi kucheza kwa mkopo mara kadhaa kwenye klabu ya AC Milan wakati akiwa kwenye Major League Soccer. 


Fond farewell: Beckham soaked up the applause in Paris earlier this week during PSG's open-top bus title parade 
PUMZIKA SALAMA: Beckham huyo kuutazama mpira kupitia Runinga akiwa nyumbani mara tu atakapostaafu mwishoni mwa msimu huu.

Historia ya Beckam katika ngazi ya klabu:

Manchester United – mechi 394, alifunga mabao 85
Preston North End (kwa mkopo) – mechi 5 , alifunga mabao 2
Real Madrid – mechi 115, alifunga mabao 20
LA Galaxy – mechi 118 , alifunga mabao 20
AC Milan – mechi 33, alifunga mabao 2
PSG – mechi 11, hajafunga bao lolote

No comments: