Thursday, May 9, 2013


Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima.
Na Khadija Mngwai
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, amejiapiza kumtungua kipa wa Simba, Juma Kaseja katika mchezo wa Watani wa Jadi utakaochezwa Mei 18.
Yanga na Simba zinatarajiwa kukutana katika mechi hiyo ya kuhitimisha mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2012/2013 utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Jumatano, Niyonzima alisema mchezo huo utakuwa mgumu, lakini anachoangalia yeye ni ushindi tu siku hiyo kwa kuhakikisha Kaseja anatunguliwa.
“Mechi itakuwa ngumu kutokana na kila upande kuhitaji kushinda lakini tunachoangalia sisi ni ushindi tu katika mchezo huo na hakuna zaidi ya hicho.
“Tunaendelea vyema na mazoezi ili tuweze kuwa fiti katika mchezo huo ambao utakuwa na ushindani wa hali ya juu, naamini tunaweza kushinda,” alisema Niyonzima.

No comments: