Wednesday, May 22, 2013


Na Mwandishi Wetu
IKIWA ni miezi tisa imekatika tangu msanii Rose Thomas Maguzo afariki dunia, mwigizaji mwenzake Jennifer Kyaka ‘Odama’ ameshindwa kujizuia na kuangua kilio upya makaburini wakati wakijengea kaburi la msanii huyo.
Odama (katikati) na ndugu wa marehemu wakiangua kilio.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Makaburi ya Mabibo, Dar ambapo Odama na ndugu, jamaa na marafiki wengine wa marehemu walifika hapo kwa shughuli ya kujengea kaburi hilo.
Marehemu Rose, ingawa alifanya kazi na watu wengine lakini siku za mwisho za uhai wake alifanya kazi kwenye kampuni ya Odama ya J Film 4 Life ambapo pia alikuwa mtaalamu wa kuwapamba wasanii ‘make up artist’.
Wakati shughuli ya kujengea kaburi hilo ikiendelea, ghafla Odama alianza kuangua kilio, hali iliyosababisha watu waliokuwa eneo hilo kupata kazi ngumu ya kumbembeleza.
...Akiwa na simanzi.
“Alikuwa kawaida tu na alijitahidi sana kujikaza maana muda mwingi alionekana mwenye mawazo na mkimya lakini ghafla akaanza kulia.
“Tulipata kazi kubwa ya kumbeleza lakini ndiyo kwanza alizidi kulia huku akisema anamkumbuka sana rafiki yake. Tunashukuru ilifika wakati akatulia,” alisema mmoja wa watu wa karibu wa Odama ambaye alikuwa makaburini hapo.
...Ndugu wa marehemu wakijaribu kumtuliza Odama.
TUJIKUMBUSHE
Marehemu Rose alicheza sinema nyingi wakati wa uhai wake ikiwemo Chocolate, Rude na House Maid ambayo alicheza kama rafiki wa Odama aliyekuwa akifanya kazi kwenye nyumba ya mzee Magali ‘Charles Magali’.
Alifariki Agosti 3, 2012 na kuzikwa Agosti 5, 2012 makaburini hapo ambapo alisindikizwa na wasanii wenzake wa tasnia ya filamu Bongo.

No comments: