Monday, July 22, 2013Na Imelda Mtema

NANI amenuna? Hayawi… hayawi sasa yamekuwa!

Mwigizaji mkongwe Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ hatimaye amefunga ndoa ya uzeeni akiwa na umri wa miaka 46.

Tukio hilo lililopambwa na cherekochereko za kufa mtu, lilijiri Jumamosi ya Julai 20, 2013 ambalo lilianzia kwenye Kanisa la Mt. Joseph lililopo Posta, Dar ambapo Natasha alifunga ndoa na mwanaume aitwaye Alex Humba Lumila.

Baada ya ndoa hiyo kufungwa kanisani hapo, mnuso ulihamia kwenye Ukumbi wa Magereza uliopo Ukonga, Dar.

Wakiwa ukumbini, mastaa wa Kibongo na wageni waalikwa waligonga ‘mpunga’ na vinywaji vya kila aina ambavyo vilikuwa vya kumwaga.

Gazeti hili lilipata nafasi ya kuzungumza na Natasha baada ya kufunga ndoa ambapo alisema kuwa siku hizi uzee unaishia Chalinze

No comments: