Monday, August 26, 2013

DILLISH KUTOKA NAMIBIA NDIYE MSHINDI WA MIL 480 ZA BBA THE CHASE

Mshindi wa Big Brother The Chase 2013, Dillish Matthews.
MWANADADA Dillish Matthews kutoka nchini Namibia amejishindia zaidi ya shilingi milioni 480 (300,000 usd) baada ya kuibuka mshindi wa Big Brother The Chase 2013.Dillish amewabwaga washiriki wenzake wanne Beverly, Melvin, Cleo na Elikem alioingia nao tano bora. Wa kwanza kutolewa tano bora alikuwa Beverly akifuatiwa na Melvin baadaye akafuata Elikem na kuwaacha Dillish na Cleo wakichuana kutafuta mshindi wa dola 300,000 za Kimarekani. Hatimaye Cleo naye aliondolewa katika kinyang'anyiro hicho na kumuacha Mnamibia Dillish akiondoka na kitita cha zaidi ya milioni 480 na kuwa mshindi wa Big Brother Season 8 The Chase 2013

No comments: