Tuesday, August 27, 2013

Stori: Mwandishi Wetu, Zanzibar
ZANZIBAR iliyokuwa ikisifika kwa sifa njema za utu na maadili siyo hii ya sasa, video iliyonaswa na gazeti hili, ikiwaonesha wake na waume za watu wakifanya vitendo vya kifuska, inatosha kutoa taswira ya hali ilivyo visiwani hapa.
Video hiyo inaonesha wazi kwamba kuna watu ndani ya Zanzibar wamekubuhu kwa michezo ya ‘kishetanishetani’ kiasi kwamba hata miji ya Sodoma na Gomora inakuwa cha mtoto kwa kulinganisha matukio.
Biblia na Msahafu ambavyo ndani yake kuna vitabu vinne vitakatifu, Torati, Zaburi, Injili na Kuran, vinaeleza kwa mapana maovu yaliyofanywa na jamii ya mtumishi wa Mungu, Lutu, katika miji ya Sodoma na Gomora.
Video kutoka Zanzibar ambayo imerekodiwa Unguja, ni wazi inafunika uharamia wa Sodoma na Gomora kwa jinsi waume na wake za watu, walivyokuwa wanatenda vitendo vya ngono hadharani, huku watoto wakishuhudia.

UCHAFU WA NGONO KATIKA KIDUMBAKI
Kidumbaki ni ngoma ya asili ya Zanzibar iliyorithiwa kutoka kwa mababu, kwa kawaida huchezwa kistaarabu pasipo kufanya vitendo vya ufuska katikati ya uchezaji.
Uchunguzi uliofanywa visiwani hapa, umebaini kwamba vikundi vibaya hususan mashoga na machangudoa, huitumia vibaya ngoma ya Kidumbaki kwa lengo la kujitafutia wateja.
“Machangudoa na mashoga hujitokeza kwenye ngoma za Kidumbaki ili kujipatia wateja. Kwa kweli Kidumbaki imeharibiwa sana na watu wa siku hizi,” alisema Zulhina Haji Makame.
Zulhina, 61, alimweleza mwandishi wetu: “Zamani tuliitumia Kidumbaki katika sherehe za harusi au pale binti anapovunja ungo. Siku hizi, mtu mwenye heshima zake anaogopa kuleta Kidumbaki kwenye sherehe yake kutokana na mapokeo ya sasa.”

UHARAMIA NDANI YA VIDEO
Kwa mujibu wa vyazo vyetu, video hiyo ilirekodiwa kwenye sherehe ya kumfunda binti aliyekuwa akiolewa, ikijulikana zaidi kama kitchen party.
Ndani ya video hiyo, watoto wanaonekana wakishuhudia uchafu wa watu ambao inafaa kuwa mama, baba, bibi na babu zao.
Vyanzo vyetu viliweka hadharani kwamba asilimia kubwa ya watu waliorekodi video hiyo ni wake na waume za watu.
“Sijui inakuwaje mwanamke anamuaga mume wake kwamba anakwenda kwenye sherehe halafu anakuja kufanya uchafu wa namna ile. Mume wa mtu kweli, anamuacha mkewe nyumbani anakwenda kufanya maonesho ya ngono na mke wa mwanaume mwenzake.
“Zanzibar inaelekea pabaya sana. Mke wa mtu kweli anamwacha mume wake nyumbani kwenda kucheza mchezo mbaya wa maonesho ya ngono na mume wa mwanamke mwenzake, halafu wanakubali mpaka kurekodiwa video. Inasikitisha sana,” kilisema chanzo chetu.
KILICHOMO NDANI
Wake na waume za watu, wanacheza Kidumbaki kwa staili ya kufanya maonesho ya chumbani.
Kuna nyakati wanavuana nguo na kuonesha vikolombwezo (chachandu) huku watoto wakishuhudia.
Katika maonesho ya chumbani, vilevile kuna nyakati wanabusu kwa ulimi maarufu kama denda.
TUNAIMULIKA ZANZIBAR
Kwa michezo hii michafu, gazeti hili linaahidi kuifanyia kazi Zanzibar kabla ya kuweka hadharani kila aina ya uvunjifu wa maadili unaoendelea. MHARIRI.

No comments: