Wednesday, September 4, 2013

MWANAMKE ANAENYONYESHA MTOTO WA MIEZI MIWILI AFUMANIWA NA MUMEWE GESTI AKIVUNJA AMRI YA SITA NA NJEMBA NYINGINE
Usiku wa kuamkia juzi ulikuwa mbaya kwa mke wa mtu, Rukia Issa au mama Sabrina baada ya mumewe, Shukuru Nia kumfumania gesti na mwanamme mwingine huku yeye akiwa na kichanga cha miezi miwili na nusu..


Rukia ambaye ni mkazi wa Goba, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam alifumaniwa katika gesti moja (jina tunalo) iliyopo Mbagala, Dar akiwa na mwanamme aliyefahamika kwa jina la Ally Said ambaye pia ni mkazi wa Goba.

Ilielezwa kuwa, siku ya tukio Rukia akiwa na kichanga chake mgongoni alimuaga mumewe kwamba anakwenda kwenye msiba Kongowe wilayani Temeke, Dar ambako angelala mpaka siku ya pili yake, yaani Jumanne. Mume alimruhusu mkewe huyo huku akimwagiza akawape pole wafiwa wote.

Mnyetishaji wetu akasema mke alipondoka na mume alitoka nyumbani kwenda kununua mahitaji f’lani dukani, kwa mbali alimwona mke wake huyo amesimama akizungumza na mwanamme mmoja ambaye amekuwa akimshuku anatembea naye.Kufutia tukio hilo la mkewe kusimama na ‘mwizi’ wake, mwanamme huyo aliamua kumpigia simu nduguye mmoja aliyekuwa msibani na kumweleza hisia zake kuhusu safari ya mkewe baada ya kumwona amesimama na jamaa, akamwambia akifika tu kwenye msiba amfuatilie kwa undani nyendo zake.

Habari zinadai kuwa, safari ya mama Sabrina ilimfikisha msibani Kongowe kama alivyomuaga mumewe na alishiriki shughuli zote ambazo alipangiwa huku uso wake ukionesha majonzi ya msiba huo.

Chanzo chetu kikazidi kueleza kuwa ilipofika majira ya saa tano usiku, akakibeba kichanga chake na kuondoka bila kuaga mtu.

Baada ya mama Sabrina kuondoka tu, hata hajafika umbali wa uwanja wa mpira, kijana mmoja akatumwa na mtu aliyepewa jukumu la kumfuatilia nyendo mwanamke huyo, akaambiwa atembee nyuma yake hadi atakapoishia.

Mtoa taarifa anasema ni ndani ya dakika kama kumi na tano tu, kijana huyo alirejea na ujumbe kuwa, mama Sabrina aliingia gesti na mwanamme, mrefu kidogo, amevaa sendozi, suruali ya kadeti na T-shirt nyekundu yenye michirizi ya rangi nyeupe na chata ya Adidas upande wa kushoto wa kifua.

Kijana akaulizwa: Mtoto je?
Kijana: Ameingia naye, tena kambeba mgongoni.
Watu waliokuwa msibani hapo wakaulizana nani ana simu yenye muda wa maongezi wa kutosha? Akajitokeza mmoja ambapo simu yake ikatumika kumpigia mume wa mwanamke huyo na kumpasha kila kitu.

Mume baada ya kupata taarifa hizo zinazoweza kumpa mtu ugonjwa wa moyo ghafla, alifanya mawasiliano na baadhi ya ndugu wengine ikiwa ni pamoja na kumtwangia simu mpigapicha wetu.

Ilikuwa saa 8:34 usiku, tukio lipo Mbagala, mpigapicha wetu yupo Kijitonyama, Kinondoni. Ilibidi apande pikipiki yake iendayo kasi kuliko nyingine katika teknolojia ya kisasa.

Ndani ya nusu saa, mpigapicha watu, mume wa mwanamke huyo, ndugu wengine na kijana aliyetumwa kufuatilia walikusanyika nje ya gesti hiyo na kupanga mbinu ya namna ya kuvamia chumbani ambapo waliipata.

Baada ya kuvamia, wote walipigwa butwaa kufuatia kumkuta mama Sabrina na jamaa yake wakiwa ‘vibaya’ huku kichanga kikiwa pembeni kimelalishwa chali tena kikiwa macho, maskini malaika wa Mungu.

Baada ya kuona kwa macho yake tukio hilo ambalo halitatoka kirahisi kwenye kumbukumbu zake kichwani, baba Sabrina alipagawa. Akamgeukia mpigapicha wetu:

“Ndugu mwandishi, siku moja nilikutana na huyu bwana, ni jirani yangu kule Goba, kwa kuwa nilishasikia anatembea na mke wangu nikamwomba aachane naye.

“Cha ajabu alinijibu kwa ujeuri kuwa niachane na yeye kwa vile hatembei na mke wangu, mbaya zaidi akanisukuma nikaanguka, nikajizoazoa pale na kuondoka zangu, niliumia sana.

Akamgeukia mkewe: Kwanza inawezekana huyu mtoto si wangu, umemleta hapa gesti kwa baba yake ili umtambulishe.

Hata huyu mtoto nakukabidhi mimi si wa kwangu, haiwezekani arobaini yake tangu azaliwe imepita juzijuzi tu, hata mimi sijakuingilia kwa sababu una mtoto mchanga leo unakuja kufanya upuuzi wako huku, hapana huyu si mwanangu.

Ndugu na jamaa walishindwa kuongea chochote kutokana na mshtuko lakini mama Sabrina kwa upande wake alijaribu kujitetea kuwa, hamu ya mapenzi ndiyo ilimshawishi kufanya hivyo.

Mwisho wa sakata hilo, wawili hao (mwanamke akiwa na mtoto wake mgongoni) walipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar kwa ajili ya hatua zaidi.

No comments: