Friday, November 21, 2014

HATUFANANI AKILI NA UJASIRI...Ukisikia maajabu makubwa ambayo hufikirii kukutana nayo hapa duniani hii ni moja wapo, Kuna mbuga moja ya kufugia nyoka wakubwa inatoa huduma ya “massage” kwa binadamu kwa kutumia nyoka hao “giant pythons” lakini kabla ya kuanza zoezi hilo nyoka hao hulishwa kuku ambao idadi yao hufikia 10 ili wasije kusikia njaa katikati ya shughuli hiyo.
Nyoka hao wana uzito wa kilo 250 na mtu anayefanyiwa massage anaweza kupiga kelele au hata kupumua bila nyoka hao kufanya chochote.

zoo2

Unaweza usifikirie kama kuna kitu kama hiki kinafanyika lakini mbuga hii iliyopo katika mji wa Cebu nchini Ufilipino inapata wateja wengi sana wakipanga foleni kusubiri huduma ya kukandwa mwili “Massage” ambayo hutolewa bure lakini kwa wanaoweza tu kuhimili mikiki yake.
Nyoka hao wakubwa wanne waliopewa majina ya Michelle, Walter, EJ and Daniel hutolewa nje kutoka kwenye eneo wanapofugwa na kuwekwa juu ya mtu anayetaka huduma huyo wakati mtu huyo akiwa amelala chini kwenye kitanda maalum karibu na lango kuu la kuingilia katika mbuga hiyo.

zoo4

Watu wengi wanashangazwa na mbuga hii na huduma inayotolewa sasa jiulize unaweza kufanya hivyo hata kama una uchovu kiasi gani?

zoo3

No comments: