Monday, November 24, 2014

Stori:  Waandishi wetu
Ulozi! Chipukizi sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Fetty’ amenaswa makaburini akiwanga katika kile kinachodaiwa kuwa ni kutekeleza masharti ya ‘sangoma’ ili ajipatie umaarufu na kuwafikia mastaa kama Wema Isaac Sepetu, Jacqueline Wolper Massawe na Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Chipukizi sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Fetty’.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Makaburi ya Ufi yaliyopo maeneo ya Ubungo-Kisiwani jijini Dar, mishale ya saa nne usiku.
Fatuma Ayubu ‘Fetty’ akiandaa mazingira.
...Akiendelea kuandaa.
...Akivunja nazi kaburini.
Habari zilidai kwamba msanii huyo alifumwa akivunja nazi na kuzungumza maneno yasiyoeleweka.
Awali, ilidaiwa kwamba, Fetty ambaye anaonekana kwenye Filamu ya House of Death akiwa na mwigizaji Kulwa Kikumba ’Dude’ alitinga kwenye makaburi hayo akiwa ameshika kimfuko huku akiangaza huku na huku kisha akatoa nazi na kuivunja huku akinuiza maneno bila kujua kuna mtu alikuwa akimpiga picha.

...Akiendelea kufanya yake.
Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Fetty na kumuuliza juu ya madai hayo, alianza kujikanyaga kabla ya kufunguka kuwa hapendi mambo ya kishirikina ila alilazimika kufanya hivyo kutokana na masharti aliyopewa na mganga wake kutokana na matatizo yake ya kimaisha yanayomsumbua pamoja na ndoto yake ya kuwa msanii mkubwa.
Vipande vya nazi vikiwa kaburini baada ya kuvunjwa na Chipukizi sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Fetty’.
Imeandaliwa na Mayasa Mariwata, Denis Mtima na Shani Ramadhani.

No comments: