Tuesday, December 8, 2009

Jamani Didier Drogba na timu yake ya Taifa wanatua Bongo Laiv bila chenga!


Timu ya taifa ya Ivory Coast ina mpango wa kuweka kambi jijini Dar kwa maandalizi ya kombe la mataifa ya afrika huko Angola mwakani. hivyo wadau tukae mkao wa kula wa kumuona Didier Drogba na wenzie.

Rais wa TFF Leodegar Chilla Tenga kawaambia waandishi wa habari sasa hivi kwamba Ivory Coast watatua Dar January 2, 2010 na kucheza mechi mbili. ya kwanza kasema itakuwa January 4 na ya pili January 7, na timu ya taifa - Taifa Stars.

tayari ujumbe mzito wa toka nchi hiyo upo Dar kwa maandalizi ya awali na hivi sasa upo hoteli ya New Africa kuongea na waandishi wa habari.

ujumbe huo ambao ni makamu wa kwanza wa rais wa chama chama cha soka cha huko, Idris Diallo, katibu mkuu wake pamoja na kocha wao, Vahid Halilhodzic, wameshatembelea hoteli kadhaa na pia uwanja mpya wa neshno na wameonesha kuridhika. ila wametoa rai kwamba uwanja wa gymkhana ambao watafanya mazoezi mepesi urekebishwe..

Ikumbukwe Ivory Coast imefuzu kucheza kombe loa dunia sauzi na mechi yao ya kwanza wanapiga na Ureno June 20, 2010 kabla ya kuivaa Brazil Juni 25 na kumalizia na Korea Kaskazini katika mzunguko wa kwanza.

No comments: