Tuesday, December 8, 2009

Mshiriki wa Miss Utalii kinondoni atimuliwa baada ya kubainika kuwa na mtoto


Mshiriki wa Miss Utalii Kinondoni 2009- Christina Masandeko (pichani juu), amefukuzwa katika kambi ya Washiriki kutokana na kuwa na Mtoto ikiwa ni pamoja na kuwa Ameolewa na hadi sasa anakaa na mume wake katika maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo imefuatia kutoakana na Kanuni za Mashindano hayo kutoruhusu Mshiriki kuwa na Mtoto ama kuwa na Ujauzito,

kutokana na Uchunguzi uliopatikana kutoka kwenye Vyanzo vya Washiriki, Mrembo huyo alikuwa akishiriki kwa kificho lakini hata hivyo hakuna siri Duniani na hivyo aliweza kubainika wakati washiriki wenzake walipokuwa wakifanya Utafiti baada ya kuwepo na fununu kuhusiana na suala hilo.

Kambi ya Washiriki Miss Utalii Kinondoni inaendelea katika Ukumbi wa New Msasani Klabu, chini ya Mwalimu wao Miss Utalii Iringa 2005 Ester Kinyunyi, ambapo jumla ya washiriki KUMI TANO wapo katika Ushindani Mkali kutokama na wote kuwa na sifa za kuwa washindi.

Fainala Miss Utalii Kinondoni zimepangwa kufanyika Tarehe 11 katika Ukumbi wa New Msasani Klabu, ambapo Wasanii wa kizazi kipya kwa kushirikiana na Vikundi vya Ngoma za Asili watasindikiza Onyesho hilo sambamba na Kundi la Vaibration Sound, ikiwa ni pamoja na TID, Abubakari Msasu(KIBOOT), Diamond,

kwa Upande wa Vikundi vya Ngoma watakaosindikiza Onyesho hilo ni Irene Sanga na kundi lake, Mandela Theatre chini ya Mzee Jangala, Mfalme Band chini ya Costa Siboka, Black Wariours, Makumbusho Dancing, ambapo onyesho limepangwa kuanza majira ya saa tatu na nusu Usiku.

Wadhamini waliojitokeza kusaidia shindano hilo ni pamoja na Mine De Copper, Fom Com International, Empire Furniture, A-one Tours & Safaris, Aucland Tours & Safaris, Aurora Security, Mashujaa Pub & Intertainment, Mamaa Sakina Trans, Ele-Tech & Lighting Agency, Regency Hotel, The Grand Villa Hotel, Clouds Fm, Prime Time Promotions, Kitangoma Magazine, Michuzi Bloggs, Mlonge By Makai Interprisess, Cm Motors, Mh.Idd Azan Mbunge, Billionea Club, Dage Saloon, Al Water Well Drilers,Rose Gaden Restaurant, B-kule Records, Tom Diamond,Ambiance Club,Varry Spring, Ngorongoro Crater,Tanga Beach Resort na Tanapa.

No comments: