This blog is for critical thinkers, people with open mind, ready to accept criticisms and work on them. Sharing the know-how, skills and experiences of Life and Technology at large. You are warmly welcome!! ---------------------------------------------------- Blogu hii ni kwa ajili ya wenye fikra makini wapendao kupokea na kufanyia kazi ukosoaji. Walio na mtazamo chanya tena mpana katika kushirikishana maarifa, ujuzi na uzoefu wa maisha na teknolojia kwa ujumla wake. Karibuni sana !!!
Tuesday, July 20, 2010
Sababu za kuuawa Prof. Jwani Mwaikusa, hizi hapa (labda)
WAKATI maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam walijitokeza kwa wingi kumzika Mhadhiri Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Jwani Mwaikusa mwishoni mwa wiki iliyopita, wanafamilia na baadhi ya mawakili wamedai kuwa waliofanya mauaji hayo ya kinyama si majambazi na wameyahusisha na kesi za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda zinazoendelea mjini Arusha.
Wakizungumza na timu ya Uwazi, wanafamilia hao akiwemo mtoto wa marehemu Baraka Mwaikusa, walisema profesa alikuwa akisumbuliwa sana na kesi za mauaji ya kimbari za Rwanda ambazo alikuwa mmoja wa mawakili wa watuhumiwa.
“Baba hakuwa na deni au hakuwa akidaiwa na mtu na wala hajawahi kumdhulumu mtu, alikuwa mtenda haki. Mara nyingi katika siku hizi za mwisho wa maisha yake alikuwa akizungumzia kesi ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda ambapo kesi moja alishinda na moja alishindwa na alikuwa anapilikapilika za kuikatia rufaa, hili naweza kusema ndilo tatizo pekee ambalo baba alikuwa akihangaika nalo,” alisema Baraka mtoto wa marehemu.
Wanafamilia hao walionesha wasiwasi wao huo kutokana na kile walichodai kuwa, wauaji hao hawakuchukua kitu chochote baada ya kutekeleza mauaji hayo ya kinyama.
Naye wakili maarufu nchini, Mabere Nyaucho Marando alikwenda mbali zaidi alipopasua jipu kwa kudai kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba mauaji hayo yamefanywa na Wanyarwanda kutokana na ushindi wa mambo aliyokuwa akiibua Prof.
Mwaikusa katika Mahakama ya Kimataifa ya Arusha na kufanikiwa kushinda kesi moja.
“Profesa Mwaikusa ni the besti advocate (wakili mahiri) miongoni mwetu, alikuwa makini kuliko mawakili wengi pamoja na mimi na nilithibitisha hilo tuliposhirikiana naye katika kesi ya Jaji Joseph Warioba na Steven Wassira.
“Sasa katika kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda moja ya kitu kikubwa alichokifanya ni kuiomba mahakama ihamie kwenye tukio kitaalamu tunasema to visit the scene of crime (kutembelea sehemu iliyofanyika uhalifu) na ombi hilo likakubaliwa. Nashawishika kuamini kuwa baadhi ya Wanyarwanda wanaweza kuhusika katika suala zima la kumuua Profesa Mwaikusa baada ya kuona hilo,” alisema Marando.
Aliongeza kuwa kwa hulka ya Wanyarwanda ambao kuuana kwao si jambo geni, kuna uwezekano mkubwa kuwa wameingia nchini na kufanya unyama huo kwa msomi ambaye alikuwa tumaini kubwa katika tasnia ya sheria.
“Wanyarwanda wana kawaida ya kuua watu hata walio nje ya nchi yao, hivyo mimi bado nashawishika kuamini kuwa hawa wanahusika na mauaji haya,” alisisitiza Marando.
Mwanasheria huyo ameliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi haraka na kuwapata waliofanya unyama huo.
Kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) miaka 14 iliyopita, Mei 22, 2009 Msajili wa Mahakama hiyo alimteua wakili Prof. Mwaikusa kumtetea mtuhumiwa, Fulgence Kayishema ambaye alikuwa polisi mpelelezi katika mkoa wa Kibuye, magharibi ya Rwanda na tuhuma zake ni pamoja na mauaji ya kimbari, kwa mujibu wa Msemaji wa ICTR, Roland Amoussouga.
Aidha, Prof. Mwaikusa alikuwa pia ni wakili kiongozi katika kesi nyingine kwenye mahakama hiyo, iliyokuwa inamhusu mfanyabiashara wa zamani wa Rwanda, Yusuf Mnyakazi ambaye aliwekwa katika orodha ya watuhumiwa watano wa kupelekwa nchini Rwanda na ombi hilo lilikubaliwa na mahakama hiyo.
Prof. Mwaikusa (58) aliuawa Jumatatu iliyopita nyumbani kwake Tegeta Salasala, jijini Dar es Salaam na watu wasiojulikana-, ambao pia walimuua mpwa wake, Daud Gwamaka (25) na jirani yake John Mtui (45) ambaye mara baada ya kufika nyumbani kwake alitoka na kukutana na wauaji hao waliodhani kuwa ni mmoja wa watu waliotoka katika nyumba ya profesa.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Charles Kenyela amesema kuwa watuhumiwa sita wamekamatwa na jeshi hilo kufuatia taarifa zilizotolewa kwake kupitia utaratibu wa polisi jamii.
“Nathibitisha kuwa hadi sasa tunaendelea vizuri na upelelezi wa mauaji hayo, msako mkali unaendelea katika maeneo mbalimbali ya Kanda Maalum na nahakikisha kuwa tutawatia nguvuni wote waliohusika na tukio hilo,’’ alisema Kamanda Kenyela.
Ameacha mke, Rofea na watoto wanne Baraka (28), Mussa (26), Amu (22) na Msafiri(19).
Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema roho yake, Ameni.
Monday, July 19, 2010
Kasisi wa Kenya ashtakiwa kuwa na 'bomu
Kasisi wa Kenya amekana mashtaka mawili ya madai ya njama za kutega bomu katika maandamano ya kuipinga katiba mpya.
John Kamau Mbugua na wanaume wengine wawili walikamatwa siku ya Jumamosi, wakidaiwa kuwa na mbolea na milipuko.
Polisi wamesema alikuwa na mpango wa kwenda Mombasa, ambapo makanisa yalikuwa yamesaidia kuandaa maandamano ya kuipinga katiba hiyo.
Mwezi uliopita, shambulio la guruneti katika maandamano ya kanisa hilohilo yalisababisha vifo vya watu sita.
Siku chache kabla ya kupiga kura ya maoni Agosti 4, baadhi wanahofia kuibuka kwa ghasia za kisiasa.
Takriban watu 1,300 waliuawa na 300,000 walilazimika kuhama makazi yao baada ya mgogoro wa uchaguzi wa Desemba 2007.
Huko mahakamani, Bw Mbugua alisema yeye ni kasisi wa kanisa la Victory, ijapokuwa maafisa wa kanisa wanasema alitengwa na kanisa miaka mitatu iliyopita.
Pia ni afisa wa chama cha Rais Mwai Kibaki cha National Unity (PNU).
Rais Kibaki pamoja na Waziri mkuu Raila Odinga wanafanya kampeni kuiunga mkono rasimu mpya ya katiba hiyo.
Baadhi ya makanisa yanaipinga katiba hiyo mpya kwasababu inatambua mahakama za kiislamu.
John Kamau Mbugua na wanaume wengine wawili walikamatwa siku ya Jumamosi, wakidaiwa kuwa na mbolea na milipuko.
Polisi wamesema alikuwa na mpango wa kwenda Mombasa, ambapo makanisa yalikuwa yamesaidia kuandaa maandamano ya kuipinga katiba hiyo.
Mwezi uliopita, shambulio la guruneti katika maandamano ya kanisa hilohilo yalisababisha vifo vya watu sita.
Siku chache kabla ya kupiga kura ya maoni Agosti 4, baadhi wanahofia kuibuka kwa ghasia za kisiasa.
Takriban watu 1,300 waliuawa na 300,000 walilazimika kuhama makazi yao baada ya mgogoro wa uchaguzi wa Desemba 2007.
Huko mahakamani, Bw Mbugua alisema yeye ni kasisi wa kanisa la Victory, ijapokuwa maafisa wa kanisa wanasema alitengwa na kanisa miaka mitatu iliyopita.
Pia ni afisa wa chama cha Rais Mwai Kibaki cha National Unity (PNU).
Rais Kibaki pamoja na Waziri mkuu Raila Odinga wanafanya kampeni kuiunga mkono rasimu mpya ya katiba hiyo.
Baadhi ya makanisa yanaipinga katiba hiyo mpya kwasababu inatambua mahakama za kiislamu.
Mwanamke avua nguo harusini, kisa eti hajaiba simu!!
Alianza hivi kama utani!
Hapa anafungua zipu kwa nyuma!
Mara akabaki na Skin Tight namna hii....
Kula stori nzima hapa chini kisha endelea na picha, hutaamini macho yako, duh! mjini kazi kwelikweli.....
Mwanamke mmoja (pichani) aliyedaiwa kuwa ni mke wa mtu ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, hivi karibuni alikumbwa na aibu ya mwaka baada ya kutuhumiwa kwa wizi wa simu ya mkononi kwenye harusi ya mfanyabiashara maarufu wa Kariakoo, jijini Dar, Bw. Alexander Kimario na Bi. Augustina Mushi, Risasi Jumamosi lina kioja kamili.
Timbwili hilo lililoshuhudiwa na mpiga chabo wetu lilimkuta mwanamama huyo ndani ya Ukumbi wa Deluxe Sinza, Dar usiku wa kuamkia Jumamosi ya wiki iliyopita Julai, 03, mwaka huu ambapo mnuso wa harusi hiyo uliweka kambi.
Huku ‘presenta’ mwenye jina kubwa wa Kituo cha Redio na Runinga cha Clouds, Ephrahim Kibonde ‘Mzee wa Assalaam Alleykum’ akiwa msema chochote ‘MC’, muda mwafaka wa maakuli ‘kuzunguka mlima’ ulifika na ndipo kichwa cha habari hii kilipozaliwa.
Shuhuda huyo alidai kwamba, Kibonde akiendelea kuwachombeza mabibi na mabwana kuelekea kwenye ‘bufee’, mwanamke mmoja (naye jina halikuwekwa kwenye kitabu mara moja) aliacha ‘vifaa’ vyake na aliporudi, akakuta simu imeota ‘mbawa’.
Ilisemekana kwamba, mwanamke huyo aliyedai kukwapuliwa simu alipiga mayowe ya kuomba msaada wamkamatie mwizi wake huku akijiapiza mbele za Mungu kuwa, alimwona kwa mbali mtuhumiwa wake.
Ilidaiwa kwamba, bila kuchelewa na kuogopa kutia sherehe ‘harufu mbaya’, wanakamati kwa kushirikiana na walinzi wa ukumbi huo ‘walimtaiti’ mwanamke aliyetuhumiwa ambaye ana umbo la jimama na kumtaka awaoneshe kadi yake ya harusi iliyompa kibali cha kuzama ndani.
Akaendelea namna hii, duh si mchezo
Ilisemekana kwamba, mtuhumiwa huyo alibainika kuwa, hakuwa na kadi ya mwaliko na pia hakujua hata majina ya maharusi.
Ilidaiwa kwamba, kwa ustaarabu mkubwa wa sherehe hiyo iliyofana vilivyo, wanakamati hao walimtaka mtuhumiwa kumuonesha mgeni mwalikwa mwingine yeyote wanayefahamina lakini akafeli mtihani huo.
Iliendelea kuwekwa kwenye rekodi kwamba, kufuatia mtuhumiwa huyo kutoa majibu yenye utata, wanakamati kwa kushirikiana na walinzi wa ukumbi huo waliamini kuwa mtuhumiwa hakuwa mhusika katika shughuli hiyo hivyo kumtaka atoe simu hiyo kabla ya kutapishwa ‘menyu’ yote ya bufee.
Hatimaye akawa kama alivyozaliwa kwa chini, aisee tumeficha hilo eneo kwa kuzungatia maadili, na pia kuwasaidia wengine (wanaume) wasipate mfadhaiko wa akili.....
Shuhuda alitambaa na mistari kwamba, baada ya kusikia wanataka kumfanyia kitu mbaya, mama huyo aliamua ‘kusaula’ nguo moja baada ya nyingine ili akaguliwe kwenye maungo yake kama alihusika na upotevu wa kilongalonga hicho.
liendelea kuweka kweupe kwamba, kitendo cha jimama hilo kuwazodoa kwa staili ya kusaula, viwalo vyake vya ndani vilisababisha wanakamati na walinzi wa ukumbi huo ambao walikuwa wanaume kupigwa na butwaa huku mama aliyeibiwa akidai huenda amempasia mtu mwingine.
Maharusi waliokuwa wakioana ni hawa hapa
Ikafafanuliwa kwamba, walinzi na wanakamati walipoona kioja hicho ndani ya harusi kinazidi kuchukua sura tofauti, waliamua kumwachia mtuhumiwa aondoke zake kwani hakuwa na kidhibiti cha kumtia hatiani mara moja.
Wednesday, July 14, 2010
Maandamano kumtetea Justin Nyari wa Arusha
Umati mkubwa wa wananchi kutoka Vijiji na Vitongoji vya Kata ya Mererani wakifanya Maandamano makubwa ya kupinga kitendo cha mfanyabiashara na mchimbaji maarufu wa madini ya tanzanite, Justine Nyari kutuhumiwa na jeshi la polisi kuhusika na wizi wa madini
mmoja wa wananchi hao akiohojiwa na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.
Na Novatus Makunga,
Arusha( Kwa Hisani ya Mchuzi Blog)
Umati wa kutoka Vijiji na Vitongoji vya Kata ya Mererani jana alasiri walifanya Maandamano makubwa wakipinga kitendo cha mfanyabiashara na mchimbaji maarufu wa madini ya tanzanite Justine Nyari kutuhumiwa na jeshi la polisi kuhusika na wizi wa madini
Wananchi hao baadhi wakiwa wanatembea kwa miguu na wengine kwa pikipiki wengi wao wakiwa ni wachimbaji katika migodi ya tanzanite ya Mererani walilizonga gari la Nyari aina ya Toyota Landcruiser mara tu baada ya kuwasili katika mji mdogo wa Mererani
Wananchi hao wakiwa na nyuso za hasira walisema kitendo cha Nyari kutuhumiwa kuhusika na wizi huo ni njama za kutaka kumchafulia kunakofanywa na wapinzani wake wa kibiashara na kisiasa
Wakizungumza na Waandishi wa habari wananchi hao Joyce Munisi,Janeth Cleopa,John Akyoo, Riziki Alfonce Ally Sibuga na Philipo Mungure walidai wafanyabiashara hao wanatumia nguvu ya fedha walizonayo kutaka kumwangamiza Nyari.
Walisisitiza kwamba Kitendo cha Wafanyabiashara hao kumsingizia Nyari kwamba anahusika katika uporaji wa madini ya Tanzanite kutoka Ofisi ya kampuni ya Manga Gems za mini Arusha ni cha hatari sana
Walisema Nyari ni wafanyabiashara mwenye roho ya utu kwani amekuwa akitoa msaada kwa makundi yanayoiswhi kwa ufukara yakiwemo ya wajane, yatima na kwa wazee wasiojiweza katika eneo la Mererani tofauti na wengine wenye uwezo kama wake.
Kutokana na tuhuma za madai hayo mapema wiki iliyopita kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Basilio Matei alinukuli na baadhi ya vyombo vya habari ya kwamba jeshi hilo linamsaka Nyari
Hata hivyo Nyari ambaye wakati huo alikuwa mjini Dodoma kwa shughuli za kibiashara alilazimika kurejea mjini Arusha na kwnda kujisalimisha polisi ambao swalimhoji kwa zaidi ya saa mbili
Wananchi hao wameiomba Serikali na Jeshi la Polisi kuwa makini na taarifa zinazofikishwa kwao kwani baadhi ya taarifa hizo zinalenga kuchafuliana katikla jamii
Kwa upande wake Nyari halikata kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kitendo cha kuhojiwa na polisi na pia kitendo cha umati wa wananchi kukusanya na kupinga kuhutumiwa kwa wizi huo
“Jamani mimi sina lolote la kuongea sina cha kuongea kwenye magazeti, wala redio ama telvisheni na waomba wananchi pigeni magoti muniombee kwa Mungu ukifika wakati nitaongea,”Alisema Nyari .
Kwa upande wake, Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha Basilio Matei alikanusha kutoa taarifa za kwamba mfanyabiashara huyo anahusika na wizi wa Madini
Kamanda Matei amesema kuwa amreshangazwa kukuta taarifa hizo katika magazti ilihalio yeye hakuzitoa .
Amefafanua kwamba polisi walipokea taarifa kutoka kwa walinzi wa Kampuni iliyoibiwa madini kuwa Nyari ndiye aliyeuziwa madini yaliyoibiwa kutoka katika ofisi ya Manga Gems.
Hata hivyo kwa mujibu wa Matei Polisi walipopata taarifa hizo waliamua kumhoji Nyari na kufanya upekuzi Ofisini kwake na Nyumba lakini hakuna kitu ambacho Polisi walifanikiwa kupata na hivyo wanaendelea na upelelezi
Amevitaka vyombo vya habari kuepuka kupotoisha habari zinazoweza kusababisha mtafaruku ndani ya jamii ili viandike ukweli kuhusu matukio mbalimbali
Tukio lilitokea usiku wa April 14, mwaka madini ya tanzanite na fedha taslimu vyote vikiwa na tham,ani ya zaidi ya shilingi milioni 100 yaliibiwa katika ofisi za Manga Gems ambapo walinzi wawili waliokuwa wanalinda walitoweka.
Tuesday, July 13, 2010
Hawa pia wamo
Hawa ndo wataalam wa Internet TR5 wakiwa na Ticha Dullah
Monday, July 12, 2010
Friday, July 2, 2010
Subscribe to:
Posts (Atom)