Wednesday, March 9, 2011

BABY MADAHA atoa Mimba!!


DIVA wa kiwanda cha filamu na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’, anadaiwa kukanyaga skendo mpya akituhumiwa ‘kuchoropoa’ mimba ya pedeshee mmoja (jina kapuni) anayeishi Mombasa, Kenya, Risasi Mchanganyiko lina fulu mkanda.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichopo karibu na mlimbwende huyo aliyeangukia kwenye tasnia ya filamu, Baby Madaha (pichani) alikuwa na uhusiano wa siri na pedeshee huyo na mara kwa mara alikuwa hakauki kwa kufanya safari kwenda katika ardhi ya Mzee Kibaki.

‘Kikulacho’ hicho kilizidi kutambaa na mistari kuwa, baada ya Baby Madaha ‘kubugia’ ujauzito wa jamaa huyo, ndipo akaanza kuhaha kutafuta njia ya kuuchoropoa lengo likiwa ni kulinda penzi lake la sasa lisiingie mchanga.

“Yaani ilikuwa pata shika nguo kuchanika, baada ya kujishtukia kuwa amenasa akaanza kutumia pombe kali, limao na baadaye akafanikiwa kuutoa ujauzito huo katika hospitali moja nchini Kenya,” kilidai chanzo.

Hata hivyo, imedaiwa kuwa mapaka Baby Madaha anafanikiwa kutimiza lengo lake hilo, alishatumia fedha kibao katika kuhangaika huku na kule bila mafanikio.

Kama kawaida, gazeti hili lilimtafuta msanii huyo ili kujua ukweli wa habari hiyo na alipopatikana alikiri kufanya ukatili huo wa kukatisha maisha ya kichanga kilichokuwa tumboni mwake.

“Aisee kwa kweli ni balaa, nani kawaambia? Anyway ni kweli na sijutii kufanya hivyo kwa kuwa hata Marekani wameruhusu tendo hilo, hayo ni mambo yangu ya ndani siwezi kuendelea kuyaweka hadharani, ila mimba kweli nilitoa,” alisema malkia huyo wa ‘songi’ la Amore ambaye hivi sasa anatamba na wimbo mpya wa Desperado.Mbali na kutamba kwenye muziki, Baby Madaha ameuza ‘nyago’ kwenye Filamu za Misukosuko na House no 44.

No comments: