Wednesday, March 9, 2011

Diamond na Wema sasa mambo yameiva

MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya ‘Bongo Fleva’, Naseeb Abdul ‘Diamond’ (pichani), amenaswa ‘laivu’ na paparazi wetu wakiwa ‘beneti’ na mpenzi wake wa sasa, Wema Abraham Sepetu, Risasi Mchanganyiko linakupa kisa kizima.

Tukio hilo lilichukua nafasi usiku wa kuamkia Machi 7, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa New Maisha pande za Masaki, Dar es Salaam ambapo Diamond alikwenda kwa ajili ya kuangusha shoo huku Wema na mama Diamond wakiwa mashuhuda.
Wakati Diamond akipanda stejini, Wema aliye pia Miss Tanzania 2006/07, alionekana akikwepa kamera na kujifanya mmoja wa mapaparazi kwa ‘kumfotoa’ picha mpenzi wake huyo huku mama Diamond akiwa amejituliza pembeni akifuatilia hatua kwa hatua mambo yalivyokuwa yakinoga ukumbi humo.


Baada ya kumalizika kwa onesho hilo, wote watatu waliingia kwenye sehemu ya kubadilishia mavazi na kuanza kupunga hewa huku wakipongezana kwa shoo nzuri iliyofanywa na Diamond.


Ndani ya dakika sifuri, paparazi wetu alijisogeza na kumkuta Wema akiwa amekaa karibu na mama Diamond.
Kabla ya kusema au kuuliza chochote, Wema alimziba mdomo mwandishi wetu kwa kumwambia kwamba, yuko na mama mkwe ambaye ni mama wa Diamond.

Alisema: “Nimetulia hapa na mama mkwe wangu, sijui unamfahamu vizuri? Huyu ni mama wa Diamond lakini hakuna tatizo kama unahitaji picha ya pamoja na mama yetu, unaweza kutupiga tu ila Diamond yule pale anasalimiana na mashabiki wake, si unajua mtu ukishuka jukwaani pongezi huwa lazima?” Alihoji Wema.


Baada ya utambulisho huo, Risasi Mchanganyiko lililazimika kuchangamkia ‘ofa’ hiyo ya kuwapiga picha ya pamoja huku Wema akisogea karibu zaidi na mama mkwe wake kwa ajili ya picha hiyo ya ukumbusho.
Bila kinyongo, mama Diamond alitoa ushirikiano kwa ajili ya zoezi hilo.
Wakati Wema na mama Diamond wakipigwa picha ya pamoja, ghafla Diamond naye alisogea na kujiunga huku akisema kuwa hiyo ni picha ya familia, akimaanisha yeye, mama yake na Wema.

Katika zoezi hilo, Diamond na mama yake aliamua kumweka Wema katikati kuonesha ishara ya upendo kwa ‘memba’ huyo mpya katika familia yao.
Katika historia ya wawili hao ambao wamekuwa wakidaiwa ‘kutoka’ wote, walimpa paparazi wetu ‘chansi’ ya kuwagonga picha kwa mara ya kwanza wakiwa katika pozi la ‘malavidavi’.
KWA NINI ‘EXCLUSIVE’?
Mara zote wawili hao wamekuwa wagumu kupigwa picha ya pamoja na kuweka wazi juu ya uhusiano wao, lakini kwa sasa haina ubishi tena kwani kinachosubiriwa ni ndoa tu.

No comments: