Msanii anayefanya vizuri kwenye filamu lakini asiyekaukiwa na skendo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani) hivi karibuni amekinadi kiuno chake na kudai kuwa kinadatisha watu.
Akizungumza na Ijumaa baada ya kuitundika picha yake kwenye ukurasa wake wa ‘facebook’ ikionesha sehemu hiyo ya mwili wake, Lulu alisema kuwa yeye ni mzuri na anaamini anawachanganya wengi hivyo hakuona haya kuwadhihirishia mashabiki wake.
Sambamba na picha hiyo msanii huyo anayedaiwa kuwa ni ‘sidanganyiki’ aliandika ujumbe unaosema kuwa, kiuno hicho kampa mama yake na wala watu wasidhani kwamba ni cha Kichina.
“Mi ni mzuri na naringia umbo langu hivyo ili kuwathibitishia watu ndiyo maana nikaamua kuiweka picha hiyo kwenye ukurasa wangu,” alisema Lulu.
Hata hivyo, baadhi ya watu walioiona picha hiyo walisema kuwa, wanashangazwa na mambo anayofanya binti huyo hasa ukizingatia kwamba umri wake bado ni mdogo.
“Hivi kwa mtoto mdogo kama huyu kukinadi kiuno chake kuna maana gani kama siyo kutaka kuwafanya watu wamfikirie tofauti? Kimsingi wazazi wake wanatakiwa kuchukua hatua za haraka kumnusuru la sivyo maisha yake yatakuwa yenye matatizo,” alisema mdau mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mama Siwema.
No comments:
Post a Comment