Wednesday, March 30, 2011

Libeneke la kikombe kama cha BABU pia kipoTabora kwa dada

Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Abeid Mwinyimsa na Kamanda wa Polisi mkoani humo Afande Barlow wakiangalia kwa makini utoaji wa tiba unakofanywa na Dada Margareth Mutalemwa huko Urban Centre 'uzunguni' Tabora
Mkuu wa mkoa akiwa na wakuu wa ulinzi na usalama wa Tabora eneo la tukio
Askari polisi akiombewa kabla ya kupata dozi
Picha na Habari na Mkala Fundikira
(pichani Mkala Fundikira akiwa na Dada Magreth) wa Keronyingi blog

Baada ya kumaliza kutoa dawa kwa watu waliokwenda kwake tangu saa kumi alfajiri,jioni hii nilipata nafasi ya kumhoji Magreth Mutalemwa (40) mwenye Mume na watoto wanne,na mahojiano yetu yalikuwa kama ifuatavyo:

Keronyingi- Dada pole na kazi, unaitwa nani?Magreth- Asante, naitwa Magreth MutalemwaKeronyingi- Unaweza ukaniambia pana nini hapa kwako mpaka watu wamejaa kiasi hiki?Magreth- Mimi hapa natoa huduma ya majiKeronyingi- Huduma ya maji kivipi?Magreth- Nawapa watu wanaokuja hapa huduma ya kikombe cha majiKeronyingi- Ili kiwasaidie nini?Magreth- Kinawatibu magonjwa wale wote wenye kusumbuliwa na magonjwa mbali mbaliKeronyingi- Ni tangu lini na vipi wewe umejua unaweza kutibu watu?Magreth- Tangu tarehe 21/March/2011Keronyingi- Enhe nieleze ilikuaje?Magreth- Nilikuwa nikipata msukumo baada ya kuoteshwa kabla ya tarehe 21 na kuidharau ndoto ile nilianza kupata matatizo lakini baada ya kuanza kufanya yale niliyotakiwa kufanya matatizo yakaisha ndio mpaka leo natibu watu.Keronyingi- Dawa yako ina mchanganyiko wa vitu gani?Magreth- Ni mti mmoja tu, ambao nauchemsha na kuwapa watu wanywe.Keronyingi- Je umepata kuwasikia watu wengine wanaotoa tiba kama wewe ambao ni Mchungaji Mwasapila, Babu dogo wa Mbeya?Magreth- Ndio mimewasikiaKeronyingi- Unawazungumziaje?Magreth- Ah ninavyoona mimi huu ni uwezo wa Mwenyezi Mungu tu, kwani katika uoteshwaji wangu nakumbuka sauti iliniambia tupo watatu na tumetunukiwa roho safi kufanya shuhuli hii ya kutoa tiba. Kwa hiyo naamini hao ni wawili na mimi ni wa tatu na ndio tuliotunukiwa.Keronyingi- Pole kwa kazi na nashukuru sanaMagreth- Asante, karibu tena.

Mpendwa mdau nataraji kuendelea kukuletea habari toka kwa Magreth Mutalemwa mpaka nitakaporejea jijini Dar. Endelea kufutilia maendeleo ya dada na tiba yake toka urban quarter, Uzunguni,Tabora

No comments: