Monday, December 19, 2011

Kwanini FUNGATE/HONEY-MOON ukafanyie kitanda cha GEST badala ya CHAKO nyumbani kwenu????



WAUMINI wa Kikristo wametakiwa kulala kwenye vitanda vya nyumbani kwao na si vya nyumba za wageni (gesti) wakati wa FUNGATE/HONEY MOON, mara baada ya sherehe za harusi ili kuepuka tabia ya kufanya ngono hovyo hovyo na kuzizoea Gesti kupaona pa kawaida sana.
Haya yalisemwa na Mchungaji Elieza Masoud kutoka Mbeya ambaye alihudhuria harusi ya rafiki yake Mchungaji Thomas Paul wa Usharika wa Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT) Mji Mpya katika Manispaa ya Morogoro ambaye amefunga pingu leo (Jumapili).


"Nashangaa sana, utaona mkazi wa maeneo ya Mji Mpya anaacha kitanda chake kizuri anakwenda kulala kwenye nyumba ya wageni inayopaswa kulala mimi mgeni kutoka Mbeya.  Hii yote ni watu kukosa uelewa katika somo hili la harusi.  Wanalichukulia kama maigizo  ya Kanumba (mcheza sinema Steven)," alisema mchugaji huyo ambaye  baada ya kumtaja Kanumba waumini wote waliofurika kwenye ibada hiyo waliangua vicheko

Akifafanua zaidi, mtumishi huyo wa Mungu alisema hali hiyo inatokana na watu kushindwa kuzidhibiti nafsi zao
zilijojaa tamaa nyingi na kukosa hofu ya
Mungu.
Maoni ya Mhariri/Mwenye Blogu:
Hii ni kweli tena ni muhimu sana. Ndoa yangu niliyofunga Juni 14, 2003 nilifanyia FUNGATE/HONEY-MOON kwenye kitanda changu nyumbani. Sikuona HESHIMA kumpeleka mke wangu mpendwa na kufanya nae TENDO LA NDOA katika KITANDA CHA WOTE huko Gesti, Hoteli, Lodge au vyovyote utakavyoita. 

No comments: