Friday, January 13, 2012

KANISA LATUMIA BENDERA, RAMANI NA PICHA YA RAIS KULIOMBEA TAIFA

 Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Bw. Stephen Ngonyani 'Almaarufu Profesa Majimarefu' akihutubia wananchi waliohudhuria mkutano wa dini ulioandaliwa na kanisa la FPCT kwa ajili ya kuliombea Taifa ambapo mbunge huyo aliwataka wananchi wajiandae kutoa maoni yao kwa tume itakayoundwa na rais jakaya kikwete ya marekebisho ya katiba

 Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assembly Of God (TAG) Mch. Yohana Tindika wa kanisa hilo la Mazinde (Kushoto), akimuombea Rais Jakaya Kikwete kupitia picha waliyoishika kwenye mkutano wa kuliombea Taifa uliofanyika mjini Mombo. wengine ni Askofu wa kanisa la FPCT Askofu Davie Mulenga na anayemfuata ni Mchungaji John Mitindo

Mchungaji wa Kanisa la Pentecostal Assembly of God (PAG) la mjini Mombo Mch. Peter Mgonja (Kushoto) akiombea viongozi wote wa Tanzania kwa kutumia ramani ya nchi yetu kwenye mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya benki katika mji mdogo wa Mombo. wengine kulia ni Askofu wa kanisa la Free Pentecostal Of Tanzania, askofu Davie Mulenga ambaye ndiye mratibu wa mkutano huo wa kuliombea taifa la Tanzania na viongozi wake baada ya kumalizika miaka 50 ya Uhuru

Askofu wa kanisa la FPCT askofu Davie Mulenga (kulia) akiwa ameshika bendera ya Tanzania kuliombea Taifa baada ya kumalizika miaka 50 ya Uhuru na nchi kuwa na amani hivyo walitumia mkutano huo kuliombea taifa ili miaka mingine 50 ya uhuru taifa lisiingie matatizoni, wengine walioshika bendera hiyo ni viongozi wa kata ya Mombo wa Chama Cha mapinduzi akiwemo Mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini Bw. Stephen Ngonyani 'Almaarufu Profesa Majimarefu'.

No comments: