Wednesday, January 11, 2012

MWANAMUZIKI CHARLES BABA KUIBUKA NA MPYA MASHUJAA BAND

Meneja wa Mwanamuziki Charles Baba,Benard Msekwa akionyesha bahasha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) yenye mkataba uliosainiwa na Mwanamuziki huyo ambao ameutuma kwa njia ya DHL.

Meneja wa Mwanamuziki Charles Baba,Benard Msekwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na mwanamuziki wake huyo kujiunga rasmi na Bendi ya Mashujaa.Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala wa Bendi ya Mashujaa,Yohana Mlawa.
Stori Kamili
MWANAMUZIKI wa zamani wa bendi ya African Stars wana Twanga Pepeta, Mbwana Gabriel Cyprian maarufu kwa jina la Charles Baba ametunga wimbo maalum wa kuanzia kazi katika bendi yake mpya ya Mashujaa kama sehemu ya utambulisho wake rasmi.

Meneja wa bendi hiyo, Benard Msekwa alisema kuwa wimbo huo utatambulishwa rasmi kesho Ijumaa katika onyesho maalum litakalofanyika kwenye ukumbu wa Business Park kwa kushurikiana na wanamuziki wa bendi hiyo pamoja na bendi nyingine mbili, Mapacha Watatu na Extra Bongo.

Msekwa alisema kuwa wimbo huo ni ‘suprize’ kwa mashabiki wa muziki wa dansi hapa nchini baada ya kusaini mkataba mnono wa miaka miwili.

Alisema kuwa hatua ya kutunga wimbo huo ni kuthamini kile alichokipata kutoka kwa uongozi wa Mshujaa na hasa wanatarajia kuona mambo makubwa siku ya onyesho lake. Kuhusiana na maamuzi ya kujiunga na Mashujaa, Msekwa alisema kuwa jumla ya bendi tano zilikuwepo katika mchakato wa kumwania mwanamuziki huyo katika bendi hiyo.

“Kulikuwa na bendi nyingi sana ambazo zilimtaka mwanamuziki wangu, lakini tulishindana kuhusiana na dau ambazo walizotoa,” alisema Msekwa.

Alifafanua kuwa Charles kwa sasa yupo nchini Dubai kwa mapumiziko na mkataba aliusaini akiwa huko na kuutuma kwa njia ya DHL. Aliongeza kuwa Charles anatarajiwa kuwasili nchini kesho saa 9.00 alasiri kwa ndege ya shirika la Emirates akitokea Dubai.

Mmoja wa Wakurugenzi wa bendi ya Mashujaa, Yohana Mlawa alisema kuwa wamefarijika kushinda mbio za kumchukua mwanamuziki huyo na sasa milango ya usajili wao imefungwa.

“Kama mnavyofahamu, tayari tumemchukua Charles na mwimbaji wa zamani wa bendi ya FM Academia maarufu kwa jina la Thalathin Tatu na tayari amekwenda sambamba na wanamuziki wanzake wa bendi hiyo,” alisema Mlawa.
Alisema kuwa hakuna mwanamuziki yoyote wa bendi ya Mashujaa ambaye ataondolewa katika bendi yao baada ya kuingia wanamuziki hao wawili.  

No comments: