Monday, May 14, 2012

SIMBA YATOLEWA MASHINDANONI NA AL AHLY SHANDY KWA MATUTA SUDAN

Baadhi ya wachezaji wa Simba wakiwa na huzuni baada ya timu yao kutolewa kwa mikwaju ya penati na Al Ahly Shandy katika mchezo wa marudiano huko Sudan. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam Simba ilishinda magoli 3-0 na kujiweka katika nafasi nzuri ili kusonga mbele katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho inayoandaliwa na Shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrka (CAF) kabla ya kulinda ushindi wake mnono ilioupata jijini Dar es salaam kwa  kukubali kipigo hicho kilichowasukumiza nje ya mashindano hayo.  Al Ahly ilipata penati tisa (9) baada ya kushinda bao 3-0, na Simba walikosa penati mbili. Hivyo Simba imetolewa kwa magoli 12 kwa yao 11(Dakika 90 jumlisha na ya penati)

No comments: