Wednesday, May 30, 2012

WAZIRI wa Mambo ya Ndani Mhe. Dk Emmanuel Nchimbi akutana na Viongozi wa Dini na Waandishi Zanzibar kuhusu VURUGU zilizojitokeza!



Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk.Emmanuel Nchimbi, akizungumza na Viongozi wa Jumuiya za Kiislam na Wadau wac Sekta ya Utalii Zanzibar, kuhusiana na fujo zilizotokea juzi Zanzibar, kulia Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema na kushoto Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali.




Waziri Dk. Nchimbi akisisitiza jambo katika Mkutano wake na Viongozi wa Dini kuzungumzia Vurugu zilizotokea juzi katika mitaa ya mji wa Zanzibar




Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema, akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Kilimani.




Viongozi wa Jumuiya za Kiislam Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza nao kuhusiana na matukio yaliotokea katika Visiwa vya Zanzibar.




Viongozi wa Jumuiya za Sekta ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, akizungumzia hali iliojitokeza juzi ya fujo katika mitaa ya Mji wa Zanzibar. na kulani hali hiyo.isitokee tena ikaharibu Amani ya Visiwa vya Zanzibar ambavyo vinasifika kwa Amani katika Afrika Mashariki.




Mwandishi wa habari wa Nipashe Mwinyi Sadala akiuliza swalim katika Mkutano huo.uliowashirikisha Viongozi wa Jumuiya za Dini na Wadau wa Sekta ya Utalii kuziungumzia vyurugu hizo.




Mwandishi wa Redio HIT FM, Jacob, alipota fursa ya kuuliza, katika Mkutano huo na Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Nchimbi.




Ofisa wa Ubalozi wa Marekani aliopo Zanzibar Jefferson Smith, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kurudisha hali ya Amani katika Mji wa Zanzibar bila ya kutokea madhara kwa Wananchi na kulipongeza kuwakutanisha Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Dini na Wadau wa Sekta ya Utalii kuzungumza nao, jinsi ya kuzuiya tatazo hili lisitokee tena




Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZATO Zanzibar Abulswamad, amesema yeye amefarijika kwa ujio wa Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP,na amelitaka jeshi la Polisi kuzuiya fujo kama hizi zisitokea tena katika Visiwa vya Zanzibar ambavyo huzoretesha shughuli za Kitalii ikizingatiwa wakati huu ni msimu wa Utalii ikizingatiwa Zanzibar ni moja ya nchi zilizokuwa na Vivutio vya Utalii.




SHEKH. Saleh Zam, akitowa shukrani kwa niaba ya Wanajumuiya za Kiislam Zanzibar baada ya kumalizika kwa Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar. Picha na Othman Mapara



Mmoja wa washiriki akieleza jambo







Mmoja wa washiriki katika mkutano huo


No comments: