WAREMBO wanaotaka kushindana katika shindano dogo la kumsaka
mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Dunia (Miss World 2012)
wameombwa kuendelea kuchukua fomu za kushindana katika kinyang’anyiro
hicho na kuzirudisha kabla ya Juni 4.
Mkurugenzi
wa Lino International Agency, Hashim Lundenga amesema kuwa wanatarajia
kufanya mchujo wa washiriki Juni 5 kwa ajili ya kubakiza warembo 10 kwa
ajili ya kuwania nafasi ya kushiriki katika mashindano ya Dunia
yaliyopangwa kufanyika Agosti 18 kwenye ukumbi wa Dongsheng Fitness
Center Stadium, mjini Ordos, Inner Mongolia, China.
Lundenga
alisema kuwa zoezi hilo lilisimamishwa kutokana na zuio la Serikali na
wakati huo, jumla ya warembo 12 walikuwa wamekwisha chukua fomu za
kushiriki. Alisema kuwa muda wa kufanya mashindano hayo umekaribia na
wanatarajia kuitangaza tarehe mpya hivi karibuni.
Alisema
kuwa amefurahishwa na kasi ya kuchukua na kurejesha fomu, hata hivyo
wanahitaji warembo wengi zaidi ili kuweza kupata wigo mpana kwa ajili ya
kumsaka mrembo atakayewania taji la Dunia ambalo kwa sasa lina mikononi
mwa mrembo kutoka Venezuela, Ivian Sarcos.
“Tunakaribia
kufanya mashindano madogo hivi karibuni, hivyo ni wajibu wetu
kuwakumbusha warembo wanaotaka kuwania taji hilo kufanya hivyo kabla ya
Juni 4 ili kuweza kuingia katika zoezi la mchujo,” alisema Lundenga.
Alisema
kuwa mpaka sasa jumla ya nchi 84 zimekwisha pata wawakilishi wao kwa
ajili ya mashindano hayo. Nchi 32 pamoja na Tanzania bado hazija chagua
wawakilishi wao katika mashindano hayo.
Fomu
za kuomba kushiriki zinapatikana katika ofisi za Miss Tanzania za
jijini na mawakala wote wa mashindano hayo katika mikoa ya Tanzania
Bara. |
No comments:
Post a Comment