Tuesday, May 26, 2009

Unamkumbuka huyu?

Rais Arejea toka Marekani

JK akisalimiana na baadhi ya viongozi waliofika kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyere jijini Dar es salaam kumpokea wakati aliporejea nchini akitoka Marekani leo.Wa pili kushoto ni Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein na kushoto ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.


JK amerejea nyumbani mchana wa leo- Jumatatu, Mei 25, 2009- baada ya ziara yenye mafanikio ya kikazi ya siku nane katika Marekani.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar Es Salaam, Rais Kikwete amelakiwa na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na viongozi wengine wa Serikali.
JK na ujumbe wake alianzia ziara yake mjini San Francisco ambako alikutana na kuzungumza na Rais wa Chuo Kikuu maarufu cha Stanford, na kutembelea Silicon Valley, eneo maarufu zaidi duniani kwa shughuli za teknolojia ya kompyuta duniani.
Miongoni mwa makampuni makubwa ambayo Rais alitembelea katika eneo hilo ni CISCO, Google na IMB ambako alisisitiza shabaha ya Serikali yake ya kuifanya teknolojia ya kompyuta moja ya ngome kuu za maendeleo ya Tanzania.
Baadaye Rais alikwenda mjini Los Angeles ambako miongoni mwa mambo mengine alitunukiwa tuzo maalum la maendeleo ya afya na taasisi ya madaktari ya US Doctors for Africa.Rais Kikwete alikuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kupewa tuzo hilo kwa sababu ya mchango wake katika maendeleo ya huduma za afya katika Tanzania na Afrika.
Kilele cha ziara hiyo kilikuwa mjini Washington D.C. ambako alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Marekani, Barack Obama na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mama Hillary Clinton.
Mazungumzo kati ya JK na Rais Obama yalichukua muda wa saa moja katika Ofisi ya Rais wa Marekani ya Oval Office, na Rais Kikwete amekuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kualikwa ili kumtembelea na kufanya mazungumzo na Obama, tokea kiongozi huyo achukue uongozi wa Marekani Januari, mwaka huu.
Mjini Washington, JK pia alikutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Dominique Strauss Kahn, na viongozi wa taasisi nyingine muhimu kwa maendeleo ya Tanzania ikiwemo MCC na USAID.

JK pia alitembelea hospitali maarufu ya kijeshi ya utafiti ya Marekani ya Walter Reed pamoja na makumbusho ya Taifa ya kijeshi hapo hapo Washington. Katika hospitali hiyo aliweza kujiuonea shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kitengo cha huduma kwa majeruhi wa kivita, na kitengo cha utafiti wa magonjwa.

Tuesday, May 19, 2009

Kinachofanywa na majaji ‘Bongo Star Search’ ni udhalilishaji wa kutisha





BILA kumung’unya wala kutafuna maneno, nathubutu kusema nimesikitishwa na wale wanaoitwa wataalamu wa kusaka vipaji vya waimbaji. Kwangu, watu hawa si wataalamu bali wababaishaji ambao wanajiona wao ndio watu na wengine hawastahiki heshima inayojali utu wa mtu.

Nimeshangazwa na kampuni ya Vodacom ambayo inadhamini kampeni hii kwa kuruhusu watu hawa kutumia udhamini wao kuwatukana Watanzania na kuonyesha ulimwengu kuwa maskini hana haki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, nimehuzunishwa na wana habari wa kituo cha ITV kwa jinsi walivyoweka taaluma na heshima ya Watanzania kando na kutojali maadili na kuwaruhusu hawa wanaoitwa ma-DJ waliobobea kuwadhalilisha, kuwanyanyasa na hata kuwatukana vijana wanaosaka ajira kupitia usanii wa kuimba.

pichani kulia ni mtayarishaji wa muziki ndani ya studio za bongo records ambaye pia ni moja ya majaji ndani ya shindano la bongo star search
Ni matumaini yangu Baraza la Habari Tanzania na vikundi vya kutetea haki za binaadamu vitaangalia hivi vibwagizo vya matusi vya hawa ma DJ kwamba havirudiwi tena; na kuionya ITV kuachana na kile unachoweza kukiita uhuni uliobobea unaoonekana katika huo unaoitwa msako wa kuibua vipaji.
Kwa wale ambao hawakuona kipindi hiki cha safari iliyojaa mbwembwe za Ma-DJ watatu wanaume wawili na mwanamke mmoja, ya kusaka vipaji vya waimbaji Tabora na Kigoma, natoa maelezo ya muhtasari ya kile kilichoonyeshwa:

1. Kijana wa miaka kama 22 hivi akiwa amevalia nguo ambazo aliamini zingeliwavutia hao ‘majaji’ anaingia kwenye ukumbi. Wanaumuangalia kama kinyago na mmoja anamwambia vazi lako halituvutii.
“Tumetumia fedha nyingi kuja hapa na wewe unafanya utani; haya imba!”
Kijana anajitahidi kuimba na baada ya sekunde zisizozidi 10, wanamsimamisha na mmoja wao akisema huku ‘majaji’ wengine wakimcheka: “Katafute kazi nyingine, hujui kuimba. Unaona mlango ule..toka hapa.”

2. Dada mmoja alipongia tu aliambiwa haya imba. Alipoanza tu walimsimamisha na DJ mmoja kumwambia: “Nani kamwambia anajua kuimba?” mwingine anamwambia rudi nyumbani ufanye kazi ya kuzalisha watoto.

3. Mwingine alipoonekana sauti yake haivutii aliulizwa anafanya kazi gani. Alijibu kwa upole kuwa anapata riziki yake kwa kutia rangi viatu. Alipokaa kimya alisukumiwa makombora ya matusi na kuambiwa anaonekana kuwa ni kibaka na kilichofuata ni kuonyeshwa mlango wa kutokea.

Mengine mazito zaidi siwezi kuyaorodhesha, lakini kwa ujumla, kipindi hiki kilikuwa kielelezo cha kuvunja vijana moyo na heshima. Fikiria watoto, ndugu na jamaa za hawa vijana wataonaje wakishaona kipindi kile kilichokuwa hakina utu, nidhamu wala maadili.

Binafsi, nilipoona udhalilishaji wa aina ile dhidi ya vijana wenye nia ya kutaka kuwa wasanii (hata kama hawajui), nilijisikia kichefuchefu na kutamani hata kuzima runinga. Lakini nikaona hapana, ngoja nijiridhishe kwa kushuhudia vijana kadhaa watakachofanyia, kweli kabisa, ilichokishuhudia na kukiona kwa macho, kilitosha kupata jawabu kuwa, wanachofanya si kuibua vipaji vya wasanii, bali kuua vipaji.

Sidhani kijana aliyethubutu kujitokeza kuonyesha nia yake ya kutaka kuwa msanii na kuishia kuonyeshwa mlango na kuelezwa akazae watoto kama atakuwa na hamu ya kutaka kujiendeleza katika fani ya usanii.

Hii inatokana na ukweli kuwa, wapo wanaotaka kuimba, lakini hawana sifa hizo na baadhi yao wanazo, lakini hawajui njia za kupita. Aidha, kama hawa ma-DJ walikuwa wanaona kijana hana kipaji, kuna lugha ya kistaarabu ya kumweka kando na siyo kudhalilishana kama ambavyo wanafanya.

Hivyo, mmoja wa ‘majaji’ hawa angeliambiwa maneno ya kashfa kama yale waliyowatupia vijana wa Tabora na Kigoma angelihisi vipi? Hapana ubishi, kuwa vijana wengi wa Tanzania, kama walivyo wazee wao ni maskini.


Lakini, Watanzania ni maskini wa kipato na sio utu, heshima, ukarimu na hisani na ndio maana maelfu kwa maelfu ya watu huhama nchi zao na kuja kuishi hapa sio tu kwa vile ni nchi ya amani, bali watu wake ni watulivu na wenye kuthamini ubinaadamu.
Ni lazima vyombo vyetu vya habari na kampuni za biashara kama Vodacom, ziache kudhalilisha watu.

Unyanyasaji sio biashara nzuri na hautakiwi na Watanzania. Wahariri wa ITV na vituo vingine vya radio, televisheni na magazeti waelewe wajibu wao na maadili ya taaluma hii ya uandishi wa habari. Maadili ya taaluma ya habari yanalazimisha kuheshimu utu, ikiwa ni pamoja na watu maskini, kama wale vijana wa Tabora na Kigoma.


Kosa limefanyika, ni vizuri lisirudiwe. Lakini suala muhimu hapa kwa hawa ma-DJ, ITV na Vodacom kuwaomba radhi na hata kuwalipa fidia wale vijana waliodhalilishwa na kuwaambia Watanzania samahani.

Kuomba radhi ni ustaarabu na anayefanya kosa na kukataa kosa lake au kuomba radhi, basi huwa si mstaarabu. Kwa ma-DJ ni vizuri wakaelewa kwamba, wanachoweza kuchezea ni ala za muziki na sauti zao wakiwa juu na nje ya jukwaa, lakini sio maisha na heshima ya Watanzania wakiwemo vijana wa kimaskini kama wa Tabora na Kigoma.

ATM zinazotoa Kondom!!! Du Raha kweli!!!


Kampuni ya PSI inayosambaza mipira ya kiume ya Salama Kondom wiki iliyopita imezindua uuzaji wa kondomu hizo kwa njia ya ATM kama hii ionekanayo pichani.

Monday, May 18, 2009

Wanafunzi Mpo?!!! Brigtha amewawakilisha hapa!


Karibuni wanafunzi wangu wa MicroComputer application session ya Saa4-6 mchana. Leo licha ya mambo mengine tutakayosoma pia tutajifunza kutembelea websites mbalimbali kama hii blog uliyofungua hivi sasa. Hapa unaweza kuapata habari mbalimbali za burudani, elimu, siasa michezo n.k.

Karibuni sana hata kwa kutoa maoni yenu hapo chini ya blog!!!

Hebu oneni mavitu ya Nakaaya!!


Kwa vipimo vingi mwanamuziki Nakaaya Sumari hivi karibuni ndiye mwanamuziki kutoka Afrika Mashariki ambaye amekula ‘bingo” kubwa kwenye anga za muziki. Kama hujatambua au kusikia,nazungumzia mkataba wake na kampuni kubwa ya usambazaji muziki ulimwenguni ya SONY MUSIC yenye makao makuu nchini Marekani.

Hivi sasa wengi wanasubiri kuona ni jinsi gani Nakaaya atafanya ndani ya mkataba wake huo wakiamini kwamba kufanya kwake vizuri ndio kutakuwa kumefungua milango mingine kwa wasanii wengine wengi hususani wakizingatia vipaji mbalimbali vilivyopo nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Hapo ndipo sote tunapomtakia kila la kheri.

Lakini wakati macho na masikio yakingoja kwa hamu, Nakaaya anazidi kuonyesha kipaji chake katika muziki. Mfano mzuri ni huu wimbo uitwao I am An African ambao ni toleo jipya likiwa lililofanyiwa ukarabati na maujuzi na producer mahiri Hermy B. Ndani ya wimbo ameshirikishwa Chid Benz ambaye bila kusita amenata na beats vilivyo. Usikilize I am an African kwa kubonyeza player hapo chini. Kila la kheri Nakaaya. The world is watching! Keep rockin’

Manchester Bingwa


Ni Siku ya furaha kwa wadau wote wa Man Utd aka The Red Devils, Ambao juzi Jumamosi wametwaa ubingwa wa Premier League kwa kutoka sale (0-0) na Arsenal.

Wasafiri "wakichimba dawa" safarini!!


Mheshimia habari za kazi,
Mimi nilikuwa mmoja kati ya abiria waliokuwa wakisafiri hivi karibuni toka Dar es salaam kuelekea Tanga, nilishangazwa baada ya basi tulilopanda kusimama ghafla baada ya kusafiri kwa masaa kadhaa.

Nilipohoji abiria mwenzangu akasema kuwa hivi ni kituo cha kwenda kujisaidia, kwa mshangao sikuona jengo lolote kama choo, ila kundi la watu wanawake kwa wanaume waliteremka ndani ya basi na kuingia mwituni kujisaidia, ama kuchimba dawa kama wenyewe ilivyosikia wakisema.

sasa mdau wangu, sijui serikali yetu hii tunayopiga kelele kila leo lina msaada gani kwa wananchi angalau hata vyoo vya kulipia katika vituo vya mabasi, maana wakati mwengine unaweza safiri na watoto au waja wazito ambao wanahitaji kutumia choo mara kwa mara.

si dhani ni jambo la busara kama ningesafiri na mama mkwe nianze kumtafutia kichaka ili ajisaidie kama picha inavyoonyesha