Wednesday, September 29, 2010

CHUO KIKUU HURIA CHAANZISHA KOZI YA SHERIA YA MAWASILIANO


Katika Picha hapo Juu: Makamu mkuu wa Chuo kikuu huria cha Tanzania,Profesa Tolly Mbwete (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Uk Telecommunications Academy,Professa David Mellor wakisaini makaratasi ya makubaliano ya kufundisha stashahada ya uzamili katika sheria ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika hoteli ya impala,jijini arusha.

Habari Kaili Na;
Novatus Makunga,Arusha

Chuo kikuu huria cha Tanzania kwa kushirikiana na taasisi moja ya nchini Uingereza kimeanza kufundisha stashahada ya uzamili katika sheria ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa lengo la kudhibiti uharifu katika matumizin ya teknolojia ya mawasiliano

Programu hiyo inaendeshwa kwa pamoja kati ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Taasisi ya mawasiliano ya Uingeleza- Uk Telecommunications Academy kwa mkataba wa miaka mitano.

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano ya pande mbili hizo katika hoteli ya Impala ya mjini Arusha Profesa Tolly Mbwete alisema kuwa tayari wanafunzi ishirini wameshadahiliwa na chuo kikuu huria hapa nchini

“Wanafunzi kutoka nchi mbalimbali wapatao ishirini tumeshawachukuwa na wengine wanaofikia hamsini na watano wanafanya utafiti wao kukamilisha shahada zao.”alisema

Akifafanua zaidi alisema programu ianawahusu zaidi wataalamu walioko katika nyanja za teknolojia ,mawasiliamo,sheria,mauzo na masoko na siyo lazima wawe na shahada ya sheria

Alisema kuwa lengo la programu hiyo ni kuwawezesha wataalamu hao kuzisaidia taasisi zao kwa kutoa kutoa ushauri wa kisheria.

Alisema kuwa programu hiyo itapunguza hali ya sasa ya kukosekana ama kuwepo kwa wataalamu wachache wa sheria katika teknolojia ya habari na mawasiliano nchini katika makampuni ya mawasilino yakiwemo ya simu

Alisema kuwa programu hiyo itawezesha makampuni hayo kuhakikisha yanaheshimu haki ya kisheria ya wananchi wanapotumia mawasiliano ya makampuni hayo.

Aidha profesa Mbwette alifafanua kuwa wataalamu hao watakuwa msaada mkubwa msaada mkubwa nchini na katika nchi jirani katika kupambana na kushamiri kwa uharifu mkubwa katika mawasiliano i kukotokana na kupanuka kwa tekonolojia na utandawazi

Mkataba wa makubaliano ulisainiwa na Profesa Mbwette na Mwenyekiti ya Uk Telecommunications Academy, Profesa David Meller.

Monday, September 27, 2010

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Jamii


ICT ni mojawapo ya kazi ambayo kama utaiendekeza bila kuwa makini basi inaweza kukupelekea kupoteza au kuharibu mahusiano,marafiki na hata kutengwa na wanafamilia.Leo hii tutaangalia mustakabari wa wana ICT ndani ya jamii,mwisho kabisa tutapenda kupata maoni yako ni jinsi gani jamii na wana ICT wanavyoweza kushirikiana ili kuondokana kero zilizomo ndani yake.

Kazi za manane
Kwenye ulimwengu wa ICT kufanya kazi hadi usiku wa manane au kutolala usiku mzima ni jambo la kawaida kabisa,je ni mara ngapi mitambo imegoma kufanya kazi na ukakesha ofisini ukitatua matatizo? Ni mara ngapi upo katikati ya mapumziko nyumbani mara ukapokea simu ukiambiwa kila kitu site kipo down ukatakiwa kuacha mambo yako binafsi na kukimbilia site kurekebisha mambo?

Kuna siku niliwahi kuongea na mmoja wa wana ICT ambaye ni tegemezi kwenye kampuni moja ya mawasiliano mujini,yeye alilalamikia kuhusu kutoelewana na mchumba wake kwakuwa muda mwingi yupo ofisini na hata akirudi nyumbani kila wakati simu haziishi hivyo wanakosa muda wa kujadili mambo yao binafsi ukizingatia ndio kamaliza chuo hivyo bado kijanaa,kwetu sisi wana ICT hili linafahamika lakini je kwa walio nje ya ICT wanaweza kulifahamu na kulikubali??

Kwenda na wakati
Mtafaruku hauishii hapo,kumbuka kuwa ICT ni teknolojia inayoishi,hapa nina maana kila kukicha kuna mambo mengi yanagunduliwa au yakihitajika na wanajamii ambao kwao wao ni kila anachofikiria anajua ni lazima wana ICT atakuja na suluhisho,hivyo ni kazi yetu kuja na suluhisho la mahitaji ya wanajamii vilevile kuwa tayari kujifunza maarifa mapya pindi wenzetu wanapogundua,hivyo basi ukiwa mwana ICT wewe upo shuleni.

Kuna rafiki yangu aliwahi kutembelea nyumbani ninapoishi,maswali la kwanza aliloniuliza,Hivi lini utamaliza kusoma? Hivi vitabu vyote umesoma wewe au? Jibu linakuja ili kuwa mwana ICT bora ni lazima uwe na uwigo mkubwa mno wa idara kadha wa kadha huku ukijiupdate na teknolojia mpya,Hivyo muda kwetu ni kama almasi,ila jamii inaweza kutuelewa?

Wanawake na ICT
Hizi ndio sababu zinazopelekea wanawake kuikimbia hii fani ya ICT,kwani wao wakifikiria msongo uliopo kwenye ICT wanaogopa kuna uwezekano wakapoteza au kukosa wenza wao kwakuwa hawatakuwa na muda wa kuitunza familia kwani kama wengi ujuavyo mila zetu nyingi ni kuwa mama ndiye mtunzaji wa familia.Hili sio tu kwa Afrika,bali dunia nzima,iwe Marekani,iwe Uchina na hata Burundi,wanawake kwenye ulimwengu wa ICT ni wachache mno.

Ushauri
Hivyo basi leo hii,tungependa kujua wewe kama mwana ICT unapambana vipi na hii hali,Je unatumia njia gani kuweza kuielimisha familia yako na kukuelewa,Kwa wale ambao sio wana ICT je wewe kama mwana jamii una ushauri gani juu ya hili kwa wana ICT? Je wakinamama walio ndani ya ICT wanamaoni gani?

Kwa kuchangia maoni yako hapa unaweza kusaidia wana jamii na kuokoa ndoa na mahusiano kibao ambayo hadi sasa yapo kwenye mkimki mkimki na pia tukajenga jamii imara.

Tuesday, September 21, 2010

Mtangazaji na Producer wa Muziki KID BWAY ashambuliwa na Msanii


MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRIKA AMBAYE VILEVILE YU PRODUCER WA KUREKODI MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NDANI YA TETEMESHA PRODUCTION SANDU GEORGE MPANDA MAARUFU KWA JINA LA KID BWAY AMEVEMIWA NA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI.

TAARIFA ZINASEMA KUWA KID BWAY AKIWA NYUMBANI KWAKE LUMALA JIJINI MWANZA, JAMAA ALIYEMVANIA ALIFIKA NYUMBANI HAPO MAJIRA YA SAA 2:30 USIKU NA KUJITAMBULISHA KAMA MSANII AKIHITAJI KUFANYA RECORDING, BAADA YA MAZUNGUMZO NA KUJITAMBULISHA ALIKARIBISHWA NDANI HADI CHUMBA CHA KUREKODIA STUDIO.

NYUMBANI KWA MTANGAZAJI HUYO ANAISHI NA JAMAA ZAKE WAWILI AMBAO WAKATI KID AKIMKARIBISHA MTENDA UHALIFU HUO NYUMBANI HAPO JAMAA HAO WALIMWONA KIJANA HUYO KISHA KILA MMOJA AKAINGIA CHUMBANI KWAKE. DAKIKA KADHAA WAKASIKIA KWA KIPINDI KIREFU SPIKA ZA STUDIO ZIKIKOROMA ISIVYO KAWAIDA NA KUANZA KUDADISI HUKU WAKIMWITA KID BWAY KUWA INAKUWAJE! WAKAITA NA KUITA NDIPO WALIPO AMUA KUINGIA STUDIO NA KUMKUTA SAKAFUNI KAANGUKA DABU ZIKIMTOKA MASIKIONI, PUANI NA KWENYE MAJERAHA SEHEMU ZA KICHWA.

KWA HIVI SASA KID YUPO HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO AKIWA HOI HAJITAMBUI YAANI KAPOTEZA FAHAMU, ALITUNDIKIWA DRIPU YA MAJI IKIWA NI HUDUMA YA KWANZA AMBAYO AMEPATIWA JANA MARA BAADA YA KUFIKA HOSPITALINI HAPO AKISUBIRI KIPIMO CHA T SCAN KUONA KWA UNDANI ZAIDI SEHEMU ALIZODHURIKA. HAKUNA TAARIFA YOYOTE YA UPOTEVU WA MALI HALI INAYOPELEKEA WADADISI WA MAMBO KUDHANI KUWA YAWEZEKANA KULIKUWA NA VITA YA KICHINI CHINI AKA BIFU(AMBAYO HAIJAFAHAMIKA).

UCHUNGUZI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI UNAENDELEA KUJUA NINI SABABU ZA UVAMIZI HUO.

Friday, September 17, 2010

Irene Uwoya nae atembea na kichupi huko Dubai, haya jionee mwenyewe!


Issa Mnally Na Richard Bukos
Nyota wa Bongo Movies, ambaye pia ni Miss Tanzania Nambari 5, 2006/07, Irene Uwoya, anadaiwa kuliaibisha Taifa kufuatia kitendo chake cha kutembea nusu utupu kwenye Uwanja wa Ndege wa Mji wa Dubai uliopo Muungano wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), Amani lina data za kumwaga.


Kwa mujibu wa mtu mmoja (jina tunalo) aliyekuwa kwenye mji huo, tukio hilo lenye sura ya aibu lilijiri Jumatatu Septemba 6, 2010, saa nne asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Dubai ambapo msanii huyo alikuwa njiani kuelekea Tanzania.


Staa huyo anayeishi na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ nchini Cyprus (jirani na Uarabuni), alivaa kaptula ya ‘jinsi’ fupi kiasi cha kuwafanya watu uwanjani hapo ambao wengi wapo katika Mfungo wa Ramadhan, kumtumbulia macho ya ‘kulaani’ vazi hilo lenye majaribu makubwa.

MWANZO WA MKASA
Baada ya kuona wananchi wengi wakimtazama Irene katika nyuso za ‘kuhamasika’ kufuatia kivazi hicho ambacho juu alikivalia jezi Namba 3 yenye jina la Ndikumana mgongoni, ndipo mtu huyo alipoamua kuwasiliana na Mpiga Picha Wetu, Issa Mnally na kummegea ishu nzima.


Ilikuwa majira ya saa 4:04 asubuhi ya Jumatatu, ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu ya mkononi (sms) ukaingia kwenye simu ya mpiga picha huyo ukisomeka hivi:

“Haloo… (likiandikwa jina la mpiga picha huyo) mambo vipi? Kama unaweza majira ya saa tisa mchana (alasiri) leo nenda Uwanja wa Ndege wa Dar umpige picha Irene Uwoya, yaani kakaa uchi mpaka siye huku Dubai tumeona aibu sana kaka... ni noma, yule demu siyo kabisa.”


Baada ya kupata ujumbe huo, mpiga picha huyo alimwendea hewani mtuma ujumbe huo ambapo alijitambulisha kwa jina na kusema kwamba, yeye alikuwa Uwanja wa Ndege wa Dubai akimsindikiza jamaa yake na alimwona Irene, lakini kwa jinsi alivyovaa hakutaka kumsalimia (huenda wanafahamiana) kwani aliona aibu.

“Mimi nilikuwepo pale Uwanja wa Ndege wa Dubai, nilimwona Irene lakini sikutaka kabisa tusalimiane kwani ni aibu sana,” alisema mtu huyo.



KAULI YA CHANZO INAFANYIWA KAZI
Saa 8: 45 Wapiga Picha Wetu, Issa Mnally na Richard Bukos walitia timu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar na kutegesha kamera tayari kwa kusubiri ndege aliyopanda msanii huyo, Fly Emirates.

Ilikuwa saa 10:08 ndugu, jamaa na marafiki waliofika uwanjani hapo kupokea wageni wao walionekana wakipigwa butwaa huku wakiangalia upande wanaotokea wageni, kumbe Irene alishafika na sasa alikuwa akitoka ili kukutana na nduguze.


Ndipo Mapaparazi Wetu walipoanza kuwajibika kwa kumfotoa picha mbalimbali, lakini na yeye (Irene) alishtukia ishu na kuanza kukimbilia maeneo mbalimbali ya Uwanja huo kwa lengo la kukwepa kamera.

Hata hivyo, Wapiga Picha Wetu walimfukuza kwa nyuma huku nyota huyo akiwa anajiziba uso kwa mkoba mdogo wa mkononi.

WAPIGA PICHA WAKUMBANA NA KIMBEMBE
Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, mmoja wa ndugu waliokuja kumpokea msanii huyo alimkamata mmoja wa Mapaparazi Wetu na kufanya jaribio la kupora kamera hali iliyozua tafrani kubwa iliyosababisha Mpiga Picha Wetu kujeruhiwa mkono wa kuume, lensi ya kamera kuharibika na simu ya mkononi kupotea.


Baadhi ya watu waliokuwa wakushuhudia tukio hilo walisikika wakimpa vijembe ndugu huyo kwa kumwambia kuwa, alichotakiwa kufanya ni kumwonya Irene kuachana na mavazi yasiyo na maadili na si kupambana na Wapiga Picha.

Hata hivyo, kamera hiyo ilidhibitiwa vilivyo na Wapiga Picha Wetu na picha zilizokwishapigwa kuwa salama (angalia ukurasa wa mbele).

Tukio la ndugu huyo liliripotiwa muda huo huo kwenye Kituo cha Polisi Uwanja wa Ndege kwa kuandikishwa kwa jalada namba JNA/IR/174/010 ambapo Irene na familia yake wanasakwa na polisi wa kituo hicho ili kujibu shitaka la shambulizi na kuharibu mal

Mwigizaji mtoto "Lulu" alewa chakari na kuvua nguo!


Jelard Lucas wa GPL
WAKATI wa Siku Kuu ya Idd El Fitri hali ilikuwa tofauti kidogo kwa mkali wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye alinaswa na mwandishi wetu akiwa hoi bin taabani kwa ulabu.

Hali hiyo ilijiri Idd Mosi ndani ya Ukumbi wa Billicanas jijini Dar ambapo msanii huyo alikuwa akisherehekea Siku Kuu hiyo akiwa na shoga yake ambaye jina halikupatikana mara moja.


Awali wawili hao walikutwa na kamera yetu ndani ya Ukumbi wa Sun Sirro uliopo Shekilango Ubungo jijini Dar ambapo kulikuwa na uzinduzi wa kundi la Tip Top Connection na baadaye kuibukia katika Klabu Billicanas.

Akiwa ‘Bills’ na ‘shosti’ wake walizidi kugida bia na kadri muda ulivyozidi kusogea mbele ndani ya ukumbi huo, ndivyo Lulu alivyokuwa akionekana kulemewa kimtindo.


Kati ya watu waliokuwa karibu yao ni ‘Pedeshee’ mmoja mwenye asili ya Kihindi ambaye alijipendekeza kwa Lulu kwa kulipia vinywani na vilaji akiwa na lengo la kuondoka na msanii huyo kwenda naye anakokujua yeye.

Hata hivyo, ilifika mahali Lulu alzidiwa na pombe hizo na kuonekana kama vile alikuwa akitaka ‘kuangusha gari’.


Ilifikia hatua Lulu aliamua kutafuta sehemu ya kuegemea kutokanana kuzidiwa na pombe na kuinamisha kichwa kulala huku ‘Kanjibai’ huyo akiwa anemmezea mate pembeni yake.

Baadaye msanii huyo aliyekuwa mguu kwa mguu na shostito wake walishtukia mtego wa Pedeshee huyo wa Kihindi na kumtoka kiaina wakimwmabia wanatoka kidogo.


Mdosi baada ya kubaini kwamba ameachwa ‘njia panda’ alionekana akizagaazagaa huku na kule kumsaka msanii huyo na shoga yake lakini bila ya mafanikio kwani kwa wakati huo ilishatimu saa kumi na moja kasoro robo alfaajiri ambapo Lulu na shoga yake walichomoka na kuelekea pande za Sinza Makaburini.


‘Shosti’ wake Lulu.
Kamera yetu ilipowakimbiza pande hizo iliwakuta wamepiga kambi kwenye hoteli moja (jina tunalo) na baadaye kuelekea makwao huku wakiwa katika gari aina ya Hiace nyekundu iliyokuwa na wanaume wanne kama mabaunsa wao.

Mashindano ya Uimbaji "Tusker Project Fame" yazinduliwa Dar


Pichani kushoto ni Meneja matukio, Bahati Sigh akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu mchakato mzima wa ushiriki wa shindano la Tusker Project Fame mbele ya Waandishi wa Habari, ambalo limezindua kampeni yake ya 4 ndani ya hoteli ya Movernpick, mapema leo mchana jijini Dar, katikati ni Meneja Mkuu wa Uhusiano, mawasiliano na Jamii Dada Teddy Mapunda na mwisho kabisa ni Mshauri wa Masoko Dada Caroline wote kutoka kampuni ya bia ya Serengeti a.k.a SBL.

Meneja Mkuu wa Uhusiano, mawasiliano na Jamii wa SBL,Teddy Mapunda amewaeleza Waandishi wa habari kuwa nia na madhumuni ya kufanya shindano hili kwa Tanzania ni kutaka kuinua vipaji vya Watanzania hapa Tanzania.

Tusker Project Fame kwa mwaka huu itakuwa inashirikisha nchi tano ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Tanzania pamoja na Sudani ya Kusini.

Aidha Teddy amesema kuwa usahili kwa ajili ya shindano hilo utafanyika katika hoteli ya Peacock-Mnazi Mmoja siku ya jumamosi kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 11 jioni.

Amesema kuwa washiriki wa shindano hilo ni lazima wawe na umri wa miaka 23 na kuendelea na wawe na vitambulisho vyao kuhakiki umri wao,"fomu za kujiunga zinapatikana Mlimani City, Benjamin William Mkapa Towers, IPS Building pamoja na sehemu ya usahili wenyenyewe pale Peacock Hotel", amesema

Wednesday, September 15, 2010

Kumbe Kikwete analindwa na Majini!


Na Elvan Stambuli
MNAJIMU maarufu Afrika Mashariki, Sheikh Yahya Hussein, amesema katika taarifa yake ya Septemba 9, mwaka huu aliyozungumzia kumpa ulinzi usioonekana Rais Jakaya Mrisho Kikwete hakuzungumzia nguvu za giza au uchawi na badala yake alizungumzia ulinzi wa majini ambayo yapo duniani kote.

Akizungumza na mwandishi wetu nyumbani kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Sheikh Yahya alisema, “ Mimi sikuzungumzia nguvu za giza na wala sifanyi uchawi au ushirikina nilikuwa nazungumzia Majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waisalamu na Wakristo na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao.”

Akifafanua zaidi mnajimu huyo alisema kila binadamu ana jini na akatoa mfano wa Mfalme Solomon ambaye anatajwa katika vitabu vitakatifu vya kidini alikuwa na Jeshi la Majini na aliwatumia katika ujenzi na vita na hata Rais wa nne wa Indonesia marehemu Abdulrahman Wahid aliyetawala kati ya mwaka 1999 mpaka mwaka 2001 aliwatumia sana Majini kwa ulinzi wake binafsi na mikutano ya chama chake kiitwacho National Awakening Party ( PKB).

“Kwa hiyo nawataka viongozi wa kidini na kisiasa wasihusishe mambo haya na uchawi, haya ni mambo ya kawaida na yanafanyika ulimwenguni kote hata hao viongozi wa kidini nao wanawatumia Majini katika kazi zao, na viumbe hivi vipo anayebisha asome vizuri vitabu vya dini na kamwe siyo uchawi,” alisisitiza mnajimu huyo.

Hivi karibuni Sheikh Yahya alisema atamuongezea ulinzi usioonekana Kikwete, kauli ambayo ilitafsiriwa na baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini kuwa ni mambo ya kichawi na nguvu za giza, hivyo kumshutumu.

Mfanyabiashara abomolewa nyumba yake


Kwa Hisani ya GPL
Nyumba iliyopo kwenye plot namba 157 ya Shaban Makumlo (pichani) Mbezi Beach Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, hivi karibuni ilibomolewa na kundi la vijana huku familia iliyokuwa ikiishi ikiwa ndani, anaripoti Makongoro Oging’.

Chanzo chetu cha habari kimedai nyumba hiyo ambayo ujenzi wake uligharimu zaidi ya shilingi milioni 100 imebomelewa huku Shabani akiwa amefungua kesi Mahakama Kuu, yenye jalada namba 18/2010 kuhusiana na mgogoro unaohusu eneo alilojenga nyumba hiyo, lakini kabla ya kutolewa uamuzi amevamiwa na nyumba kubomolewa.

“ Shabani alipopata taarifa ya kuvamiwa kwa mji wake alifika eneo la tukio na kukuta zoezi la ubomoaji linaendelea, aliwasihi watoke lakini waliendelea ndipo alipiga risasi hewani kwa lengo la kuwatawanya,” kilisema chanzo hicho.

Imeelezwa kuwa, licha ya kuwatisha kwa kupiga risasi juu, vijana hao waliendelea na ubomoaji ndipo alimjeruhuwi mmoja pajani jambo lililowafanya wenzake wasogee mbali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Elias Kalinga alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa analifanyia uchunguzi.

Tuesday, September 14, 2010

Askari Usalama wa Taifa ajimiminia risasi mdomoni, afa

OFISA wa Usalama wa Taifa , Bw. Mzee Mnyete (32), amejiua kwa kujipiga risasi mdomoni iliyotokea kichwani na maiti yake imekutwa ikiwa imelala kitandani chumbani kwake ghorofa ya nne Block 'A' Makumbusho Kijitonyama kwenye nyumba za Usalama wa Taifa.


Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari maiti hiyo iligundulika jana saa 2:45 asubuhi wakati ofisa huyo akitafutwa kwa ajili ya kazi maalum na viongozi wake.

Ilidaiwa kuwa, baada ya ofisa huyo ambaye alikuwa hajaoa kutoonekana kazini jana, ndipo wenzake waliamua kwenda kwake na kukutwa mlango ukiwa umefungwa.

Baada ya kuchungulia kwa ndani waliona mwili wa ofisa huyo ukiwa umelala kitandani kwake, walipovunja mlango walibaini akiwa amekufa huku akiwa na jeraha la risasi mdomoni na kichwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Bw.Elias Kalinga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ingawa alieleza kuwa alikuwa nje ya ofisi kutokana na kutojisikia vizuri.

" Nipo hospitali afya yangu si njema naumwa lakini hata mimi nimezipata taarifa hizi hivyo nitazifanyia uchunguzi wa kina,"alisema Kamanda Kalinga.

Wednesday, September 8, 2010

Warembo Miss Tanzania wanusurika kufa baharini!


Hemed Kisanda na Jelard Lucas wa GPL wanaripoti
WAKATI Watanzania wakiwa na hamu kubwa kutaka kumjua ni nani atatwaa Taji la Miss Tanzania mwaka huu, ni Mungu tu ndiye aliyeweza kuokoa maisha ya warembo hao kufuatia kupinduka kwa mtumbwi waliokuwa wamepanda kuelekea katika kisiwa kimoja ndani ya Bahari ya Hindi kwa ajili ya kupiga picha.


Hali hiyo ilitokea Jumapili iliyopita umbali wa mita 15 kutoka ufukwe wa Bahari ya Hindi karibu na Hoteli ya Giraffe, Mashariki mwa Jiji la Dar e Salaam ambako warembo hao wameweka kambi tayari kwa shindano hilo.

Imeelezwa kwamba tukio hilo ambalo lingeweza kupoteza uhai wa warembo hao lilitokea baada ya mtumbwi huo kukumbwa na dhoruba kufuatia kuchafuka kwa hali ya hewa baharini.


Lundenga akipiga mbizi
Kwa mujibu wa habari tulizozipata, ndani ya mtumbwi huo kulikuwa na warembo tisa ambao walikuwa wakitangulia kwenda katika kisiwa hicho kabla ya mtumbwi huo kurudi kuwachukua wengine.

Risasi Jumatano limeweza kupata majina ya warembo waliokuwa katika mtumbwi huo kuwa ni Angelina Ndege (Lindi), Salma Mwakaluka (Dar City Centre), Flora Martin (IFM-Vyuo Vikuu), Fatma Ibrahim (Kanda ya Ziwa- Mara), Magreath Godson ( Kanda ya Ziwa- Shinyanga) , Shadya, Christina Justine (Chuo Kikuu Huria) na Ummy Malik (Sinza- Kinondoni) na mmoja ambaye jina lake halijapatikana.


Dalili za kutokea kwa ajali hiyo zilianza kuonekana mita 10 baada ya mtumbwi huo kuanza safari ambapo ulipofika mita 15 kutoka nchi kavu hali ya hewa ilibadilika na mawimbi mazito yakaanza kuupiga hivyo kushindwa kuhimili kasi na kupinduka.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko muda mfupi baada ya taarifa hizo kutolewa, Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga ‘Anko Hashimu’ alikiri kutokea kwa ajali hiyo na kusema ilikuwa ya kawaida kama ambavyo ajali nyingine zinavyotokea.



“Ni kweli ajali imetokea lakini ni ya kawaida kama zinavyotokea ajali nyingine,” alisema Lundenga na kuongeza kuwa, walifahamu kwamba warembo wengi hawajui kuogelea hivyo walijiandaa kwa kuwapa majaketi maalum ya kuogelea ‘Life-jackets’.

“Kama vile haitoshi, tulishaandaa boti yenye kasi ‘speedboat’ kwa ajili kutoa msaada kwa lolote ambalo lingeweza kutokea,” alisema Lundenga.

Katika hatua nyingine, Lundenga amewashukuru wazazi wa walimbwende hao kwa kuwa na moyo wa uvumilivu hata baada ya taarifa za tukio hilo kutolewa.

“Kwa kweli tunashukuru kwa uvumilivu wao maana kama wangekuwa na moto ingekuwa balaa,” alisema Lundenga.

Aidha, aliongeza kwamba, warembo wote walipatiwa matibabu maalum ya kuwarudisha katika hali zao za kawaida na wako tayari kwa ajili ya shindano.

Katika hatua nyingine mmoja wa warembo walio katika kinyang’anyiro hicho (jina tunalo) ameliambia gazeti hili kuwa kulizuka hofu kubwa na vilio kutawala baada ya hali ya hewa kuchafuka na hatimaye kupinduka kwa mtumbwi na kuwaacha wakizama baharini kabla ya kuokolewa na waogeleaji waliokuwa kwenye ‘Speedboat’.

"BREAKING NEWS"-Mchumba wa Maimatha Jesse wa TBC1 afariki duni!


By Michuzi Blog:
HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE NA ZA KUTHIBITIKA KABISA, ZINARIPORI KWAMBA MKURUGENZI MSAIDIZI WA BENDI YA MUZIKI WA DANSI YA DIAMOND MUSICA, PERFECT KAGISA 'P. DIDDY' (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA.

P. DIDDY AMBAYE ALIKUWA NI MCHUMBA WA MTANGAZAJI MAARUFU WA TBC1,MAIMATHA JESSE AMEPATWA NA MAUTI HAYO LEO HII WAKATIKA AKIWA KATIKA MATEMBEZI YAKE YA KILA SIKU BAADA YA KUANGUKA GHAFLA KATIKA BARABARA YA LUMUMBA, MNAZI MMOJA, JIJINI DAR ES SALAAM

MWILI WA MAREHEMU UMEPELEKWA KATIKA HOSPITAL YA TAIFA YA MUHIMBILI KWA UCHUNGUZI ZAIDI.

TUNAENDELEA KUFUATILIA KWA UKARIBU NA TUTAWALETEA KILA KITAKACHOKUWA KINAJIRI KATIKA MSIBA HUU.

Tuesday, September 7, 2010

Dr. Slaa afunguliwa Mashataka

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa (pichani), amefunguliwa kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaami, akidaiwa fidia y ash. bilioni moja kwa madai ya kunyang’anya mke wa mtu.

Kesi hiyo namba 122 ya mwaka 2010, ilifunguliwa leo mahakamani hapo na Aminiel Mahimbo kwa kupitia ofisi ya mawakili ya Amicus.

Mahimbo anadai kuwa, Dk. Slaa kamnyang’anya mkewe wa ndoa Josephine Mushumbusi.

Kwa kupitia nakala ya hati ya madai, Mahimbo anadai fidia ya sh. milioni 200 kutokana na hasara alizozipata baada ya mdaiwa huyo, kumtangaza mkewe wa ndoa Josephine kuwa mchumba wake na sh. milioni 800 ikiwa ni hasara ya jumla aliyopata.

Mlalamikaji huyo, anadai Septemba 7, 2002 alifunga ndoa na mwanamke huyo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushirika wa Kijitonyama na kuishi maeneo mbalimbali ikiwemo Kimara, Baruti, Dar es Salaam.

Pia anadai katika maisha yao ya ndoa wamebahatika kuwa na watoto wawili ambao ni Upendo aliyezaliwa Mei Mosi, 2003 na Precious aliyezaliwa Machi 14, 2007.

Mahimbo alidai, ndoa kati yake na Josephine haijavunjwa na chombo chochote na kwamba, bado ni mke wake halali.

Kwa mujibu wa hati hiyo, Mahimbo alidai hivi karibuni, mkewe alikuwa na safari za mara kwa mara na aliamini ni za kikazi. Josephine ni mfanyabiashara ambaye anaendesha kampuni iitwayo Green World Clinic.

Alidai katika tarehe na mahali tofauti, Dk. Slaa alimtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe, suala ambalo si kweli.

Mlalamikaji huyo alidai, uhusiano uliopo kati ya watu hao wawili umemfanya adhalilike na kunyanyasika katika jamii na anaiomba mahakama kumzuia Dk. Slaa kuendelea kujihusisha kimahusiano na mkewe.

Anaiomba mahakama kumwamuru Dk. Slaa kumlipa bilioni moja na kulipa gharama za kuendeshea kesi.

Mahimbo amedai ameambatanisha na cheti cha ndoa na Josephine, picha za harusi, vyeti vya kuzaliwa vya watoto na nakala za vipande vya magazeti zilizopigwa wakati Dk. Slaa akimtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe.

Mume aeleza alivyoporwa mke na Dk. Slaa


Aminiel Mahimbo Mume wa ndoa wa Josephine Mushumbusi

NAKUACHIA kibanda chako, nakwenda kwenye nyumba yangu.”

Hayo yalikuwa maneno ya mwisho ambayo Aminiel Mahimbo aliambiwa na mkewe, Josephine Mushumbusi siku alipoachwa na mkewe huyo aliyeamua kwenda kwa mgombea wa urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa.

Mahimbo ambaye ni mume halali wa Josephine, (kwa ndoa ya kanisani) alisema anakumbuka kuwa ilikuwa Machi mwaka huu na hakujua mke wake alipokuwa akienda na wala hakuhisi dalili yoyote ya kuwepo kwa mwanamume mwingine katika ndoa yao mpaka siku mwanawe wa kwanza Upendo (7) alipomwambia “baba tunaishi na daddy”.

Akisimulia kisa hicho kilichoanza takribani miezi saba iliyopita, katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana, Mahimbo ambaye ndoa yake ilifungwa Agosti 16, 2002 na Mchungaji Lewis Hiza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, alisema hakujua kama huyo ‘daddy’, ni Dk. Slaa mpaka siku moja alipoambiwa na mama mkwe wake.

“Baada ya (Josephine) kuondoka nyumbani, tulikwenda mpaka nyumbani kwao kusuluhishana, lakini alikataa katakata kurudi nyumbani na wazazi walikasirika na kumfukuza.

“Siku moja mama mkwe alikuja Dar es Salaam (kutoka nyumbani kwao Mwanza) na alikwenda kumtembelea mama yangu Kijitonyama,” alisimulia.

Alisema alipopata taarifa ya kuwepo kwa mama mkwe wake Dar es Salaam, aliwasiliana naye kwa simu na katika mazungumzo hayo mama huyo alikuwa akilia huku akimwambia kuwa mume mpya ni Dk. Slaa.

“Nilimpigia baba yake mdogo, Ruhendela (hafahamu jina la pili anahisi ni Mushumbusi ambalo ni la ukoo) kutaka kufahamu ukweli wenyewe, akathibitisha hilo na kusisitiza kuwa familia haimtambui mheshimiwa, inanitambua mimi,” alisema.

Kabla ya kufahamu hilo, Mahimbo alisema siku moja ilikuwa sikukuu, akaomba kupewa watoto awapeleke kwa bibi yao, na walipokuwa njiani, mwanawe Upendo alimwonesha hoteli ambayo Josephine, Dk. Slaa na watoto hao walikuwa wakiishi.

“Sikumbuki jina, ila ipo barabarani ukishapita Makongo maeneo ya Tegeta na siku hiyo baada ya kuwarudisha watoto, mama yao aligundua Upendo katoa siri ya mahali wanapoishi.

“Alimpiga na baada ya hapo akanipigia simu na kumpa Upendo aongee na mimi, alikuwa akilia akisema baba njoo unichukue siwezi kuishi huku,” alisimulia Mahimbo.

Alisema wakati akijitayarisha kwenda kumchukua mwanawe, ndugu zake walimshauri asiende kwa kuwa ilikuwa saa tatu usiku na walikuwa wakihofia usalama wake.

Kwa mujibu wa Mahimbo, mama mkwe wake alimwambia kuwa Dk. Slaa na Josephine, walihamia katika hoteli ya Abla Hotels Apartment iliyopo Victoria Dar es Salaam.

“Nafikiri bado wapo hapo, juzi juzi nilikwenda hapo kutaka kuonana na mheshimiwa (Dk. Slaa), waliniambia kuwa yupo ndani amepumzika siwezi kumuona muda huo,” alisema Mahimbo.

Gazeti hili liliwasiliana na hoteli hiyo kwa simu ambapo mhudumu mmoja alisema hawezi kuelezea taarifa za watu, lakini akathibitisha kuwa Dk. Slaa alikuwa akiishi hapo.

Mahimbo alisema aliwasiliana na Mchungaji Hiza ambaye aliahidi kuzungumza nao tofauti kabla ya kuwaita pamoja kwa ajili ya usuluhishi.

“Nimeongea na Mchungaji Hiza, amesema ameshazungumza na Josephine na ataniita kwenda kuzungumzia hilo, juzi alikuwa Dodoma kulikuwa na mkutano wa viongozi wa dini,” alisema.

Pia Askofu Mkuu wa KKKT, Alex Malasusa alipohojiwa alisisitiza kuwa hawezi kuzungumzia hilo kwenye simu.

Hata hivyo Mahimbo alisema zamani alikuwa akizungumza na watoto wake, Upendo na Precious, lakini kwa sasa ana miezi miwili au zaidi ya mmoja tangu awaone watoto hao na hata simu siku hizi hawapewi.

Mahimbo alisema hakuwahi kuhisi kwamba mkewe alikuwa akiisaliti ndoa yao na mara kwa mara alikuwa akisafiri kwenda mikoani hasa Dodoma wakati wa Bunge akijua ni kikazi mpaka alipofahamu kuwa mkewe anaishi na Dk. Slaa, ndio aliposhituka kuwa safari za mkewe Dodoma hazikuwa za kikazi tu.

Alisema mpaka sasa Josephine ni mke wake halali, lakini hana hakika kama wanaweza kurudiana tena kwa kuwa amemdhalilisha.

Na wakati Mahimbo akiwa njia panda akishindwa kujua hatima ya ndoa yake, Dk. Slaa, Padri msomi `amelitangazia’ taifa mbele ya mikutano ya kampeni ya chama chake cha Chadema kuwa Josephine ndiye mke wake mtarajiwa.

Katika kudhihirisha kuwa `hatanii’, amekuwa akizunguka naye katika mikoa mbalimbali nchini anakopita kufanya kampeni ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania baadaye mwaka huu.

Dk. Slaa alidiriki pia kumkana mke wake wa miaka nenda miaka rudi, Rose Kamili aliyezaa naye watoto wawili, akidai kwa sasa hana mahusiano naye, bali ana `chombo kipya’, Josephine.

Ni baada ya kumtangaza Josephine ndipo habari zilipovuja kuwa, mwanamke huyo anayetamba naye Dk. Slaa ni mke wa mtu aliyefunga ndoa kanisani mwaka 2002, lakini akaamua kuondoka katika mazingira ya kutatanisha na kutua kwa mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya Chadema.

Kwa upande wa Rose, mwanaharakati na mwanasiasa aliyeiongoza CCM katika Kata ya Basotu Hanang akiwa Diwani kwa miaka 16 kabla ya kuhamia Chadema hivi karibuni na kutangaza kugombea ubunge Hanang, amekuwa kimya kuzungumzia suala la mumewe.

Na hata juzi walipokutana katika kampeni za Dk. Slaa mkoani Manyara.

Rose ingawa alikuwa jukwaa moja na Josephine alionesha ukomavu kwa kujali kampeni zake hadi mgombea huyo wa urais alipoondoka Hanang kwenda Mbulu kuendelea na kampeni zake.

Mwanamke abakwa hadi kufa Arusha!

MWANAMKE mmoja mkazi wa Kitongoji cha Kisambare, Usa River wilayani Arumeru, amebakwa hadi kufa na kundi la wanaume akiwemo mumewe wa ndoa.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Basilio Matei (Pichani chini)amemtaja marehemu huyo kuwa ni Juliana Zacharia (38) na mumewe Stewart Yesaya Msemo anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kula njama na wabakaji kufanya kitendo hicho.

Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo la kusikitisha lilitokea majira ya usiku katika nyumba ambayo bado inajengwa baada ya kuburuzwa kutoka eneo alilokuwepo na kuingiliwa kwa zamu na wanaume hao.

Alisema kuwa kabla ya tukio hilo, marehemu alikuwa na ugomvi na mumewe uliosababisha watengane kwa muda na kwamba siku ya tukio Juliana alionekana katika baa moja akiwa na mumewe huyo wakinywa pombe huku wamekaa meza tofauti.

Aliongeza kuwa inadaiwa kuwa muda mfupi mumewe alionekana akiongea na kundi la wanaume, muda mfupi marehemu alienda kujisaidia ambapo hakurejea tena hadi mwili wake ulipokutwa umetelekezwa eneo
hilo.

Hata hivyo, imedaiwa kuwa kabla ya tukio hilo mumewe baada ya kuongea na kundi la wanaume alitoweka ghafla.

Kamanda Matei alisema baada ya taarifa hiyo polisi walifika na kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu uliokuwa mtupu na kubaini kuwa
sehemu zake za siri zilikuwa zimeingiliwa na kukuta mabaki ya mbegu za kiume.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya, Tengeru na Polisi wanamshikilia mume wa marehemu huyo kwa mahojiano zaidi huku watuhumiwa wengine wakiendelea kutafutwa.

Uingereza yalemewa na wanafunzi wa kigeni wasiorudi makwao!

By BBC
Waziri wa uhamiaji atasema, idadi ya wanafunzi wa kigeni wanaoruhusiwa kuingia Uingereza "haikubaliki."

Katika hotuba itakayotolewa baadae, atahoji iwapo Uingereza inawavutia wanafunzi bora- ikiwa nusu tu ya visa zinazotolewa kwa wanafunzi zimetolewa kwa wale wanaosomea elimu ya juu.

Kauli za Bw Green zinatolewa huku utafiti wa wizara ya mambo ya ndani zikisema moja ya tano ya wanafunzi bado wako Uingereza, miaka mitano baada ya kupewa viza.

Wizara hiyo imewafanyia utafiti wahamiaji ambao hawatoki Ulaya waliokuja Uingereza mwaka 2004.

Kundi kubwa zaidi- takriban watu 185,000- walikuwa wanafunzi, na asilimia 21 bado walibaki nchini hata miaka mitano baadae.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya mambo ya ndani Danny Shaw alisema, pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wa kigeni, Bw Green ameamua suala la mabadiliko ya uhamiaji wa wanafunzi kulipa kipaumbele
'Shagalabagala'

Mawaziri pia wana nia ya kutathmini viza za kufanyia kazi kwani mbili ya tano ya kundi hilo wamebaki Uingereza baada ya miaka mitano.

Kabla ya hotuba yake, Bw Green alisema: " Hatuwezi kuhisi tu kuwa kila anayekuja hapa ana uwezo ambao Uingereza hauna."

Aliiambia kipindi cha redio cha BBC Radio 4: " Sitaki kuingilia mafanikio yaliyopatikana kwenye vyuo vyetu."

Bw Green alisema: "Kwanini wanabaki? Wanabaki kufanya nini? Hili ni jambo tunalotakiwa kuliangalia kwa upana zaidi hasa katika mfumo wa uhamiaji."

Ofisi ya takwimu za taifa zilizotolewa mwezi uliopita zilionyesha uhamiaji umeongezeka kutoka 33,000 hadi 196,000 kwa mwaka 2009.

Idadi ya viza zilizotolewa kwa wanafunzi zimeongezeka kwa asilimia 35 hadi kufikia 362,015.

Bw Green alisema takwimu hizo ni ushahidi tosha kuwa serikali ya muungano ilirithi mfumo wa uhamiaji ambao uko "shagalabagala"

Alisema, " Takwimu hizo zinaniambia kwamba tunatakiwa kuangalia njia nyingine zote zinazotumiwa na watu kuingia nchini, labda kwasababu ya elimu, sababu za kuungana na familia, na pia, hasa, njia zinazowapa ukaazi wa kudumu."

Rooney nae ktk Kashfa ya Ngono!!!


Mshambuliaji Wayne Rooney amesafiri na kikosi cha England kwa ajili ya pambano la kufuzu kucheza fainali za Euro dhidi ya Switzerland licha ya tuhuma zinazohusiana na maisha yake binafsi.

Chama cha Soka cha England kimethibitisha kusafiri kwa Rooner. Mchezaji huyo amesafiri na kikosi cha England kitakachocheza siku ya Jumanne katika kundi lao la C.

Hata hivyo, kocha wa England Fabio Capello atalazimika kuamua iwapo Rooney yupo makini kimawazo kucheza mechi hiyo. Habari zilizotolewa na gazeti la News of the World pamoja na Sunday Mirror, zimefichua taarifa hizo na magazeti yote ya udaku ya Uingereza yalisheheni habari za kashfa ya Rooney kwenda nje ya ndoa.

Rooney alifanya kazi nzuri wakati England ilipowalaza Bulgaria mabao 4-0 katika uwanja wa Wembley siku ya Ijumaa, baada ya kutocheza vizuri wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.

Monday, September 6, 2010

Kumbe "Linah" na "Amini" ni wapenzi!!!



STAA chipukizi katika gemu ya Muziki wa kizazi kipya Bongo, Estalinah Sanga ‘Linah’hapo juu anayeliwakilisha ‘gemu’ kutoka nyumba ya vipaji THT amemuanika mtu anaye vunja naye amri ya sita na kuzima minongo’no iliyoenea mtaani kuwa anatoka na nguli wa hip hop nchini, Ibrahimu Musa ‘Roma’

Linah anayetamba kwenye chati za Bongo Fleva hivi sasa na ngoma ya ‘Wrong number’ aliyomshirikisha Barnaba ameliambia Ijumaa kuwa, ameamua kuweka kila kitu wazi ili kuepuka maneno ya watu ambao anahisi wanataka kuharibu uhusiano wake.

“Nimesikitishwa na taarifa za kuwa mimi natoka na Roma, huo ni uzushi kwani Roma ni shemeji yangu na kila anaye fahamu ukweli anajua kuwa mtu wangu ni Amini Mwinyimkuu yule aliyeimba wimbo maarufu wa Bado Robo saa,” alisema Linah.

Nyota huyo alitanabaisha kuwa, anampenda Amini kuliko kitu kingine chochote hivyo hafikirii kufanya jambo lolote ambalo litatishia uhai wa uhusiano wao mpaka mpango na ahadi yao ya kufunga ndoa itakapotimia.

Saturday, September 4, 2010

Ushawahi kuona Day Care kwa ajili ya Mbwa?, soma hapa


Dogs heading to Totally Dog day center
Dogs heading to Totally Dog day center in Miami, Tuesday, Aug. 17, 2010, sit in their seats. Daily up to 25 dogs board the yellow school bus for their ride to the five acre fully fenced doggy playground complete with a bone shaped swimming pool. Some of the dogs are dropped off by their owners in business parking lots and others are picked up at their homes.

Thursday, September 2, 2010

Wasanii wetu


Irene Uwoya a.k.a. Mrs Ndikumana ktk pozi la kushuti muvi

Hapa yupo na Vincent Kigosi a.k.a Ray the Greatest

Eliza wa TZ avishwa pete ya uchumba na Kelvin


Ilikuwa ni kama utani katika nyumba ya Big Brother katika shindano lilopita kwa kijana Kelvin kumsalandia dada yetu Elizabeth Gupta lakini siku zote waswahili wanasema hatafutae huwa achoki na akichoka ujue kapata.Ndani kabisa ya ukumbi wa comedy club port Harcout Kelvin chuwang na Elizabeth walipopanda kwa pamoja kuimba wimbo wa kelvin "una pata mambo" baada ya kumaliza kuimba ndipo kelvin akapiga magoti na akatoa pete na kumwambia Lizzy "Elizabeth will you marry me"basi tena dada yetu hakuwa na neno tena.


Kelvin akiwa na Elizabeth.Nadhani wadu mtakumbuka zaidi Danger zone

Kelvin na Elizabeth wakiwa ndani ya Abuja

Mkoloni na mwenzake wanywa mtori hatari!!


Kwa Hisani ya Jiachie Blog

Habari za kuvunjika vunjika zilizoifikia JIACHIE mapema leo asubuhi zinaeleza kuwa mmoja wa Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Fred Marik a.k.a Mkoloni (kulia) ambaye pia ni Mwanachama wa chama cha CHADEMA inadaiwa leo mapema asubuhi akiwa ameambatana na msanii na mwanachama mwenzake G.Solo walikwenda kupata kifungua kinywa maeneo ya MEEDA BAR-Sinza jijini Dar.Inadaiwa kuwa wote wawili waliamua kupata mtori eneo hilo,lakini katika hali isiyo ya kawaida mmojawao (Mkoloni) akaanza kujisikia vibaya kwa kusumbuliwa na tumbo na kuanza kuishiwa nguvu,Habari zinazidi kudatisha kuwa baada ya kutokewa na hali hiyo ikabidi watu wamkimbize haraka zahati ya karibu maeneo ya Palestina-Sinza kwa huduma ya kwanza.


Habari zinaeleza kuwa mara baada ya kufika kwenye zahanati hiyo na kuchukuliwa vipimo,ikabainika kuwa bado tatizo halijaonekana kuwa ni nini ama ni kitu gani, hivyo wakashauriwa waende hospitali ya Mwananyamala kwa vipimo zaidi,kukawa hakuna namna ikabidi wampeleke hospitali ya Mwananyamala ambapo mgonjwa huyo alipatiwa vipimo na kubainika kuwa alichokunywa kilikuwa kimewekwa madawa ya kulevya, Kwani mgonjwa huyo alikuwa akikoroma sana na kuonekana kama mtu aliyepoteza fahamu..

Kwa mujibu wa taarifa zilizokuwa zikiingia ndani ya JIACHIE , ni kwamba msanii huyo bado amelazwa katika hospitali hiyo kwa matibabu zaidi.Wadau habari ndiyo hiyo tuendelee kuvuta subra zaidi kwani kuna mdau mkubwa wa JIACHIE amenitonya anakwenda hospitalini hapo kumjulia hali msanii huyo

JWTZ latimiza miaka 46


Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Davis Mwamunyange pichani akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari,alisema kutimiza miaka 46 kwa Jeshi hilo kumeendana na maboresho mbalimbali yenye lengo la kuleta tija katika katika suala zima la ulinzi wa amani mipaka ya nchi.

Pamoja na hayo Jenerali Mwamunyange aliongeza kuwa kwa muda wa karibuni Jeshi la Tanzania limekuwa likifanya maonesho mbalimbali yanayosaidia kuonesha wananchi masuala yanayohusu Jeshi lao.

Akielezea historia ya Jeshi hilo Jenerali Mwamunyange alisema kuwa awali maadhimisho hayo yalifanyika baada ya miaka 10 ambapo kwa sasa yanafanyika kila baada ya miaka 5 yenye kushirikisha Jeshi lote nchini.

Kila mwaka JWTZ huadhimisha wiki ya majeshi ambapo kwa kawaida huanza tarehe 26/8/2010 hadi tarehe 1/9/2010 ambapo mwaka huu sherehe hizo ziliadhimishwa katika kambi ya wanajeshi wa majini kituo cha kigamboni ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dokta Hussein Mwinyi.

Kutoka Dereva teksi hadi msanii wa filamu


Emmed Hamis ‘Ramsey wa bongo’, Ester Flavian,Daud Tairo Michael, na Raulant Anthon ‘makala

Kutoka Udereva teksi hadi msanii na mwandaaji wa filamu
*Anatingisha na filamu za ‘Fake Pregnant’ Where Is Love, na sasa ‘Aunt Suzzy’.

WASANII nchini wataneemeka na kufaidi matunda ya kazi zao za filamu nchini ni pale tu watakapoamua kutoa kazi zilizo na ubora, utashi kwa jamii ikiwemo kufikisha ujumbe wa haraka na mpangilio sahihi wa filamu yenyewe.

Hayo ni maneno yake msanii na mwandaaji wa filamu anayekuja kwa kasi kubwa hapa nchini, Daud Michael, anayetamba na filamu za ‘ Upside Down’, ‘Where Is Love’, ‘Fake Pregnant’ na filamu ambayo ipo mbioni kutoka iliyojaa mastaa kibao ya ‘Aunt Suzzy’.

Katika mahojiano maalum na Tanzania Daima Wikienda, Daud Michael anayemiliki studio yake ya kisasa ijushughulishayo na uandaaji wa filamu mbalimbali hapa nchini inayofahamika kama ‘D Production, iliyopo maskani ya Mabibo Makutano jijini Dar es Salaam.

Daud anasema kuwa mpaka alipofikia ni safari ndefu katika tasnia hiyo ya sanaa kwani aliweza kupita milima na mabonde kama wasemavyo waswahili mpaka kufika hapo alipo na kuwa na kampuni yake hiyo sambamba na kutoa filamu zake ambazo jamii wamezikubali.