KUTOA TAARIFA ZA SIRI KATIKA
MAWASILIANO YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAI
Hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imegundua kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunzaji wa siri za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi. Mawasiliano hayo yamefikia hatua ya kuchapishwa katika vyombo vya habari.
Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha wenye makampuni ya Simu na wananchi kwa ujumla kuwa, kutoa taarifa za mawasiliano binafsi ya simu bainA ya watumiaji wa huduma hiyo, ni uvunjaji wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Na. 3 ya mwaka 2010 na Kanuni za Mawasiliano (Kulinda Wateja) za mwaka 2005.
Kifungu cha 98 ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kinasema;
(1) “Mtu yeyote ambaye ni mfanyakazi wa kampuni yenye leseni ya kutoa huduma za mawasiliano, au mwakilishi wake, ana wajibu wa kutunza siri za mawasiliano binafsi na taarifa zozote za siri za wateja kwa mujibu wa sheria hii”
(2) “Mtu yeyote haruhusiwi kutoa taarifa binafsi za mteja yeyote alizopokea au kusikia kwa mujibu wa sheria hii isipokuwa tu mtu huyo ameruhusiwa kwa mujibu wa sheria”
Kifungu cha 123 (1) kinasema:-
Mtu yeyote ambae bila sababu za msingi atasababisha kuingilia au kuzuia kupokewa kwa mawasiliano yeyote ya kielektroniki anafanya kosa and akipatikana na makosa atatakiwa kulipa faini ya shilingi za kitanzania zisizopungua milioni tano au kwenda jela kwa muda wa usiopungua miaka miwili au adhabu zote kwa pamoja”
Kanuni ya 12 ya Kanuni za Mawasiliano
za mwaka 2005 za Tanzania (Kulinda Wateja) inasema:-
“Mtoa huduma za Mawasiliano haruhusiwa kuingilia kati, kusikiliza au kutoa taarifa zozote za mazungumzo ya mteja yeyote yaliyopitia kwenye mtandao wa mtoa huduma, isipokuwa kwa ruhusa kulingana na mahitaji maalumu kwa mujibu wa sheria zilizopo”
Kutolewa kwa taarifa za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa simu za mkononi ni lazima kunafanywa na mtu mwenye ujuzi na uelewa wa jinsi ya kupata taarifa hizo na wenye ruhusa ya kufanya hivyo katika mtandao wa Kampuni husika ya kutoa huduma ya mawasiliano; ama peke yake au kwa kushirikiana na wenzake kwa kuingia kwenye mtandao kwa makusudi kwa lengo la kuingilia mawasiliano binafsi ya watu, ambayo ni uvunjaji na kinyume na matakwa ya kifungu cha 123 cha Sheria Na. 3 ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta.
Mamlaka ya Mawasiliano inayakumbusha Makampuni ya simu kuweka uzuizi na kuhakikisha siri za mazungumzo binafsi ya wateja zinahifadhiwa na hazitolewi kwa yeyote isipokuwa kwa mujibu wa sheria na; kuhakikisha yanafanya uchunguzi kugundua walioiningilia mazungumzo binafsi ya wateja.
Wananchi wanapewa tahadhari kuhusu kutafuta au kutaka kupata taarifa za mawasiliano ya siri kutoka kwa watoa huduma na kuzitumia taarifa hizo binafsi za mawasiliano pasipo kufuata utaratibu ulioruhusiwa kisheria.
Kwa taarifa ambazo zimechapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni, Mamlaka ya Mawasiliano inafanya uchunguzi wa uvunjwaji huo wa sheria kwa kutoa taarifa binafsi za wateja kinyume na sheria. Baada ya kuwabaini wahusika, Mamlaka itachukua hatua za sheria kwa yeyote atakayebainika kuvunja sheria hiyo.
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
22 Desemba 2010
This blog is for critical thinkers, people with open mind, ready to accept criticisms and work on them. Sharing the know-how, skills and experiences of Life and Technology at large. You are warmly welcome!! ---------------------------------------------------- Blogu hii ni kwa ajili ya wenye fikra makini wapendao kupokea na kufanyia kazi ukosoaji. Walio na mtazamo chanya tena mpana katika kushirikishana maarifa, ujuzi na uzoefu wa maisha na teknolojia kwa ujumla wake. Karibuni sana !!!
Thursday, December 23, 2010
Wednesday, December 22, 2010
Tido Mhando atemwa TBC
Sadick Mtulya na Patricia Kimelemeta
BAADA ya kufanya kazi nzuri ya kuboresha matangazo na uendeshaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), serikali imeamua kuachana na mkurugenzi wa chombo hicho, Tido Mhando baada ya mkataba wake kuisha, lakini mtangazaji huyo maarufu ameielezea uamuzi huo kuwa kuwa ni wa utata.
Kuenguliwa kwake kumefanyika takriban miezi miwili baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambao TBC iliripoti kwa kina na bila kupendelea chama chochote na hivyo kujivunia sifa kemkem kutoka kwa watazamaji wa TBC1 na wasikilizaji wa redio hiyo ya umma.
“Hatua hii imenishtua kidogo na hata hivi ninapoongea na wewe wafanyakazi wengi wamepata mshtuko na wengine wanalia," alisema Tido alipoongea na Mwananchi jana. "Ni juzi (Jumatatu) ndio niliandikiwa barua na serikali ya kutakiwa kuondoka.... ilikuwa kinyume kabisa na uratatibu wa serikali.
“Barua ya kutakiwa kuondoka niliipata mara baada ya kukutana na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Vijana , Seti Kamwanda.’’
Tido, ambaye kabla ya kujiunga na TBC alikuwa mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC), alisema kwa mujibu wa taratibu mfanyakazi anayemaliza mkataba wake anatakiwa kujulishwa suala hilo miezi sita kabla.
"Kimsingi (barua) hukumbusha kwamba mkataba unamalizika na kama serikali inakusudia kuuendeleza au la. Sasa hilo halikufanyika kwangu," alisema.
Kwa mujibu wa Tido, hatua hiyo inaweza kutafsiriwa tofauti na wananchi hasa ikizingatiwa kwamba imefikiwa miezi miwili tu tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu.
Wafanyakazi walipata taarifa ya kuondolewa kwa Mhando jana baada ya mkurugenzi huyo kubandika tangazo la kuwataarifu kuwa anaondoka na kwamba ametakiwa akabidhi ofisi kwa Joe Rugabaramu.
"Tangazo linasema kuwa amefanya kazi na sisi kwa miaka minne na sasa mktaba wake umeisha na kwamba ametakiwa akabidhi ofisi kwa Rugarabamu," alisema mmoja wa wafanyakazi wa TBC.
"Baadaye alitushukuru kwa ushirikiano wetu kazini na akatuambia tusubiri hadi hapo mkurugenzi mpya atakapotangazwa."
Mfanyakazi mwingine alisema kuwa walitarajia kuwa Mhando angetimuliwa mapema kabla ya uchaguzi kwa kuwa wanadai kuja kwake nchini kulitokana na uhusiano wake na kigogo mmoja wa CCM ambaye kwa sasa hayuko madarakani.
"Angetimuliwa hata kabla ya Desemba 15, lakini ikaonekana kuwa isingekuwa sahihi," alisema mfanyakazi huyo ambaye alieleza kuwa Mhando aliwasiliana pia kwa simu na mfanyakazi mmoja mmoja kumuelezea uamuzi huo wa serikali.
Habari za Tido kuondoka TBC zilianza kuvuma wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wakati iliposemekana kuwa alikuwa akipigana vijembe vya chinichini na vigogo wa CCM kutokana na vyombo hivyo vya umma kutangaza habari bila ya upendeleo.
Baadhi ya mambo yaliyoibua hisia kuwa mtendaji huyo wa shirika la umma angeondolewa ni msimamo wake wa kuendelea kurusha hewani kipindi cha "Jimbo kwa Jimbo" ambacho kilikutanisha wagombea ubunge wa vyama mbalimbali vya siasa kwenye mdahalo kuhusu maendeleo ya eneo lao.
Kipindi hicho kilichorushwa kwa wakati mmoja na vituo vya televisheni na redio kilianza kwa kushirikisha wagombea wote wa ubunge kwenye jimbo, lakini katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akaandika waraka wa kuzuia wagombea wa CCM kushiriki kwenye mdahalo huo akidai kuwa chama hicho tawala kina njia zake za kufanya kampeni.
Pamoja na CCM kujitoa, TBC iliendelea kurusha vipindi hivyo hadi kumalizika kwa uchaguzi ambao uliisha kwa CCM kupoteza viti vingi Tanzania Bara, ikiwa ni mara ya kwanza tangu serikali iruhusu mfumo wa vyama vingi.
"Ilikuwa aondoke kabla kampeni hazijaanza ingawa mkataba wake ulikuwa umalizike Desemba 15. Lakini serikali ilikuwa inarekebisha mambo yake na kumtafuta mtu anayeweza kurithi nafasi yake," chanzo cha habari cha ndani serikalini kilidokeza.
Chanzo kingine alisema: "Kuna watu wanaajiriwa pale TBC ambao malipo yao yanayotokana na Saccos ya shirika hilo, kitu ambacho ni kinyume na taratibu za serikali zinazotaka mwajiriwa alipwe na Hazina."
Jitihada za gazeti hili kumpata katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Seti Kamhanda hazikuzaa matunda.
Alipoulizwa endapo atakubali kurejee kwenye wadhifa huo ikitokea serikali ikamwita tena, Mhando alijibu: "Nitalazimika kuchukua muda zaidi kutafakari hilo kwa kina.
“Nitafanya maamuzi ya kazi ya kufanya kulingana na wakati utakavyokuwa, lakini itanichukua muda kidogo kutafakari hilo kwa kuwa nimefanya kazi mfululizo.’
Kuhusu utendaji wa shirika hilo, Tido alisema amefarijika kwa kiasi kikubwa na mafanikio ya kiutendaji yaliyofikiwa.
“Nilikuwa na mipango mikakati mingi ya kuendeleza shirika hili hususani kulifanya lijiendeshe kwa kujitegemea bila ya kuhitaji ruzuku serikalini," alisema na kuendelea:
“Lakini nimefarijika vya kutosha na utendaji wangu na mafanikio yaliyofikiwa na TBC hadi wananchi kukiamini chombo hiki na ‘reaction’ imekuwa nzuri kutoka kwao na kwa vyama vya siasa.’’
Mbali na kurusha taarifa za kampeni katika njia iliyoonekana kuwa si ya upendeleo hata kwa chama tawala, TBC ilifanikiwa sana katika urushaji wa moja kwa moja wa matangazo ya mechi za mpira wa miguu na matukio makubwa ya kisiasa na kijamii.
Mechi za michuano mbalimbali ya kimataifa na ya ndani, urushaji wa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge, urushaji wa moja kwa moja wa matukio makubwa na staili ya utangazaji ulilifanya shirika hilo kuwa na mvuto mpya na hivyo kuweza kupambana na vituo vingine vya redio na televisheni vya kampuni binafsi.

Friday, December 17, 2010
DADA ZETU CHAMBO CHA KUWAPATIA URAIA WAGENI
Kutoka Michuzi Blog
Jana nilipata sijui niite bahati au balaa? Call it eye opener. Nilikwenda kweye msiba huko Mbezi ya Kimara. Katika huo msiba, dada yetu (soma mtanzania) alifariki na “mumewe” ni mtu wa Afrika Magharibi, almaarufu kwa kucheza sinema zenye kuvuta hisia za watu wengi.
Idadi kubwa sana ya raia wa nchi hiyo katika huo msiba ilinifanya nijiulize maswali kadha wa kadha. Wanafanya nini wote hao nchini? Wana vibali vya kuishi nchini kihalali? Si vema ku judge mtu kwa sura yake au alivyo ila kwa tathmini ya haraka kuhusu raia hao wa kigeni, wengi wao niwanalekea ni misheni town.
Raia wengi wa kigeni wanaotaka kuishi nchini wanakimbilia kuwaghilibu dada zetu wawaoe na kuwazalisha ili wapate uhalali wa kukaa bila ya kubugudhiwa. Na dada zetu katika harakati za “to make the ends meet” wanaingia katika mitego hii bila ya kujijua.
Akina kaka nao kwa mbalii wanakuja katika huu mtego. Akishampata mke wa kigeni (wakenya wanaongoza), utitiri wa ndugu wanakuja kwa shem!.Halafu? Malizia sehemu ya mwisho waraka huu
Mlango mwingine usiotamkwa sana unaotumiwa kuwaingiza wageni ni kwa kupitia taasisi za kidini. Kuna makanisa mpaka wafagizi wametoka nje. Watumishi wa Mungu wanaokwenda kupata neno la Mungu katika makanisa hayo wafumbue macho na kuhoji uhalali wa kuleta wafanyakazi toka nje! Tena wahubiri ndo wamechachamaa na kufagilia inter marriages eti kuwa zinaleta maendeleo! (Commercialization of religions)
Sina maana ya ubaguzi ila kama ni kuja nchini waje kwa kufuata taratibu zinazotakiwa na muda wao ukiisha waondoke pasi na hodi. Wamejazana huko kariakoo, Kinondoni na kwenye viwanda, magereji na magodown. Jamani mpaka masokoni nako tunahitaji “maexpatriate”?
Mamlaka husika kwa maana ya vyombo vya uhamiaji na vinavyohusika na usalama wa raia, umefika wakati muafaka wa kuamka usingizini na kutuepusha na balaa linalokuja siku za usoni.
Napata maono ya kuwa inabidi hawa raia waliooa dada/kaka zetu wafuatiliwe kwa kina. Ndoa hizi huwa zinaishia vipi? Kwa divorce? Kwa vifo? Na akina nani wanakufa? Sisi au wao? Hatima ya watoto inaishiaje? Wanatelekezwa au wanachukuliwa/toroshwa kwenda “kwao”?

Wednesday, December 8, 2010
Matembezi ya Hisani, kuchangia Elimu Arusha, Desemba 17
Na Arusha Mambo
Ofisi ya Mbunge ya Jimbo la Arusha Mjini imeanza kazi zake rasmi na kuipa ahadi ya Elimu kipaumbele ili kuhakikisha watoto kati ya mia tano hadi elfu moja wanawezeshwa kujiunga na Elimu ya Sekondari ifikapo Januari 2011.
Huu ni utekelezaji wa ahadi ya Mbunge wa Jimbo hilo Mheshimiwa Godbless Lema aliyoitoa wakati wa Kampeni, kuwa atashirikiana na wananchi wa Jimbo lake kupata fedha ili kulipa ada kwa watoto hao wasiokuwa na uwezo watakaokuwa wamefauli kujiunga na elimu ya Sekondari na wale wanaoendelea na masomo katika shule za Serekali.
Mheshimiwa Lema amesema, tayari Kamati ya Maendeleo ya Jimbo (THINK TANKERS) imeundwa ili kuanza mikakati ya kuandaa matembezi ya hisani yatakayofanyika tarehe 17/12/2010 kufanikisha kupata fedha kabla ya mwezi Januari ili ada hizo ziweze kulipwa.
Amesema uteuzi wa wajumbe wa kamati hiyo aliyoiteua umezingatia jinsia, elimu, vigezo vya uwajibikaji, kuheshimika mbele ya jamii, uwezo wa uelewa na uhamasishaji, michango ya wateuzi katika kazi za kijamii, uwezo wa kufikiri na sifa zao kwa Jamii bila kujali itikadi.
Kazi ya kwanza ya kamati hiyo ni kuunda na kusimamia kamati ndogo itakayosimamia Mfuko wa Elimu wa Jimbo na kuandaa mchakato wa uwazi wa upatikanaji wa watoto na kusimamia tukio la upatikanaji wa fedha.
Hata hivyo Mheshimiwa Lema ameomba wananchi wa Jimbo lake bila kujali itikadi wajitokeze kwa wingi siku hiyo na kutoa michango yao ya hali na mali bila kujali udogo au ukubwa wa vipato walivyonavyo ili kwa pamoja waweze kuijenga Arusha Mpya.
Amesema kabla ya tarehe 13 mwezi huu atakuwa ameshaiapisha kamati hiyo na siku hiyo ndipo wananchi, waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa maendeleo watakapoelezwa mfumo wa uchangiaji, uchangiaji huo utakavyoendeshwa, jinsi ya kupata watoto wenye uhitaji pamoja na matembezi yenyewe yatakavyofanyika.
Aidha ameomba mshikamano toka kwa wananchi wa Jimbo la Arusha na wale wa jumuiya za kimataifa wanaoishi Arusha kujitokeza kuchangia maendeleo na kuleta mawazo yao yatakayoleta changamato za maendeleo katika jimbo hilo na amewasihi wananchi wa jimbo lake kuwa kuanzia sasa watu wajifunze kujali na kuwasaidia wahitaji wanaoishi nao.
Amesema vipaumbele vingingine vitakavyofanyiwa kazi haraka baada ya elimu ni miundombinu, afya ikiwemo usafi wa Jiji, watoto wanaoishi katika mazingira magumu ma upatikanaji rahisi wa huduma za kijamii.
Mheshimiwa Lema (Mb.) ameomba Makampuni, Taasisi mbalimbali zilizopo Arusha na Watanzania wote waliopo nje ya Tanzania wanaopenda kuchangia maendeleo katika Jimbo lake wajitokeze kusaidia maendeleo katika jimbo hilo ili kuweka historia ya maendeleo ya kweli kupitia Nguvu ya Umma.

Tuesday, December 7, 2010
Njama hizi ni hatari
Na Luqman Maloto
Ujumbe mfupi wa maneno (SMS) unaohusishwa na mpango wa kijasusi wa kumuua Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Zuberi Kabwe (pichani), umenaswa na Uwazi.
Katika SMS hiyo, aliyeiandika alisisitiza kwamba Zitto atakufa kwa siri lakini kabla ya kutekeleza kifo chake, atanyang’anywa nyaraka zote alizonazo ambazo hazikufafanuliwa kwenye ujumbe.
SMS hiyo, iliyonaswa kwenye simu ya mmoja wa makada wa CHADEMA (jina tunalo), ametajwa kama mmoja wa watakaotekeleza mpango wa kumuua Zitto, inasomeka:
“Nawaarifu kwamba nipo Mara nimemaliza kukutana na viongozi wa Mwanza. Inaelekea hawakubaliani na hoja yetu ya kumfukuza Zitto, sasa nilikwisha kusema kwamba tuweke mkakati kwenye Media JF. Ni …, … na … (yanatajwa majina ya watu).”
SMS hiyo inaendelea: “Ni …, … na … (majina mengine ya makada wa CHADEMA) watatekeleza kazi tuliyowapa na … (anatajwa kiongozi wa CHADEMA) atawapa mtu wa kuwaongezea nguvu.”
Ujumbe huo hauishii hapo, unaendelea: “Kuweni makini, hakikisheni amewapa nyaraka zote alizonazo kabla ya kumuua, usiri unahitajika… atawasaidia kujua nyendo zake na hii tu ndiyo njia ya kukinusuru chama.”
Uchunguzi unaonesha kuwa SMS hiyo ilizunguka kwa watu kadhaa ambao wanadaiwa wapo kwenye mtandao ulioandaliwa kutekeleza mpango wa kukatisha maisha ya Zitto.
Gazeti hili limebaini kuwa mmoja wa wabunge wazoefu wa Viti Maalum (CHADEMA) alitumiwa kisha naye akaituma (kui-forward) kwa mwenzake ambaye ni memba mpya ndani ya bunge.
Gazeti hili lilifuatilia mnyororo wa SMS hiyo na kugundua kwamba wakati ujumbe ukizungushwa kwa wanaodaiwa wana mtandao, uliingia ‘kirusi’ kwa kumfikia mtu ambaye hakukubaliani na wazo la kumuua Zitto.
“Hapa hatari iliyopo ni kwamba kuna mtu ambaye hakubaliani na wazo la kumuua Zitto, ndiyo atakuwa amevujisha,” kilisema moja ya vyanzo vyetu.
Chanzo chetu kilisema kuwa mtu huyo baada ya kupata SMS hiyo, aliituma kwa mama yake Zitto, Shida Salum ambaye naye ‘aliifowadi’ kwa mwanaye.
Gazeti hili lilimpata Zitto na alikiri kupata SMS, ingawa alidai kuwa uchunguzi ndiyo utafanikisha kumnasa mhusika mkuu wa ujumbe huo.
Zitto, akijibu bila uchangamfu, alisema wakati mwingine anahisi kuna watu wanatumiwa ili kukivuruga CHADEMA.
“Nafsi yangu haisemi kama ni kweli. Inawezekana kuna watu wametuingilia, Mungu ndiye anajua,” alisema Zitto.
Alipoulizwa kuhusu kuripoti polisi, Zitto alijibu:
“Nikiripoti ni kwa ajili ya uchunguzi wa kipolisi tu. Sitaki kutoa kwenye vyombo vya habari, sihitaji mgogoro kwenye chama.”
Kwa upande wa Mama Zitto, alikiri kupata SMS hiyo na kueleza kwamba tayari amesharipoti kwenye vyombo vinavyohusika.
“Sitaki kuizungumzia hiyo SMS, inachunguzwa kipolisi,” alisema Mama Zitto.
Gazeti hili lilizungumza na Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Regia Mtema ambaye ni mmoja watu wanaodaiwa kutumiwa SMS hiyo ambaye alikiri.
Hata hivyo, Regia aliye pia Ofisa wa Oganaizesheni wa chama hicho alisema: “Hiyo SMS sijatumiwa mimi peke yangu, kila mtu makao makuu anayo.
“Nafikiri kuna watu wametengeneza lakini hakuna mpango wa kumuua na kwanini auawe?”
Baada ya kuzungumza hayo, simu ilikatika na alipopigiwa tena hakupokea mpaka tuliapoamua gazeti kwenda mitamboni.
Wakati Zitto akipuuza ufuatiliaji wa SMS hiyo, chanzo chetu kimoja ndani ya makao makuu ya CHADEMA, kilisema kuwa si vema kudharau vitu kwa sababu ujumbe huo una alama za hatari.
“Mimi sipendi sana kuzungumzia mambo ya marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA), lakini naye kifo chake kilitokea akiwa na mvutano na viongozi wengine wa chama kama ilivyo kwa Zitto sasa,” kilisema chanzo chetu.
Mpango wa kumuua Zitto, inakuja baada ya matukio kadhaa ambayo yalikaribia kuondoa uhai wake, ikiwemo kuwekewa sumu kwenye maziwa.
Miaka minne iliyopita, Zitto alikunywa maziwa yenye sumu kwenye hoteli moja jijini Mwanza na kuokolewa na aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum (CCM), marehemu Amina Chifupa ambaye alimpigia simu na kumueleza asiendelee kunywa.
Hata hivyo, kutokana na wingi wa maziwa aliyokuwa amekunywa dakika chache baada ya kupokea simu ya Amina, aliishiwa nguvu na kukimbizwa kwenye hospitali moja jijini humo ambapo alipatiwa matibabu.

Subscribe to:
Posts (Atom)