Wednesday, February 8, 2012

MMOMONYOKO WA ARDHI WATISHIA UFUKWE WA KINGO ZA ZIWA VICTORIA HUKO MWANZA

 Wahenga walisema usipoziba ufa utajenga ukuta. Hii inajidhihirisha katika ukingo wa Ziwa Victoria sehemu za bustani mwanana ya jiji la Mwanza ambapo pametengenezwa na kupandwa nyasi nzuri ili wakaazi wa Rock City wapumzike na kupunga upepo. Tatizo ni kwamba ukuta uliojengwa kwenye kingo za mto huo zimeanza kumomonyoka, na hatua za haraka zisipochuliwa kurekebisha hali hiyo madhara makubwa yatatokea. Isitoshe Globu ya Jamii imeshuhudia watu wakitupa taka kwenye sehemu zilizibomoka!

Huyu mama bila shaka anasikitikia hali ilivyoanza kuwa mbaya sehemu hii mwanana

Pamoja na mandhari ya kuvutia lakini Hali si shwari kama inavyojionesha...

sehemu ya uzio nayo imeanza kumeguka. Hii huenda inasababishwa na watu kutumia njia ya mkato baada ya kukosekana pa kuingilia kwa upande huu 

Vibati vya uzinduzi wa bustani hii inasemekana vimeshafanywa chuma chakavu na wajuaji

Huduma ya maji ya ziwa inapatikana kwa urahisi, hivyo wazee wa jiji la Mwanza shime itunzeni sehemu hii

No comments: