Wednesday, February 29, 2012

MTOTO WA GADDAFI ATAKA NYARAKA ZA KIFO CHA BABA YAKE!!

Mwanasheria wa mtoto wa kanali Muammar Gaddafi amefungua shauri kisheria katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu (ICC) kutaka nakala ya vyeti vya kifo cha kiongozi huyo wa zamani wa Libya.


Mwanasheria huyo wa Aisha Gaddafi, Nick Kaufman amesema hatua hiyo inachukuliwa kama sehemu ya kuonyesha kuwa baraza la serikali ya mpito ya Libya haikuendesha kwa usawa kesi ya kaka yake  Saif al-Islam ambaye alikamatwa jangwani kusini mwa nchi hiyo mwezi Novemba mwaka jana.


Mahakama hiyo ya makosa ya uhalifu huko The Hague,Uholanzi imemwambia mtoto huyo wa Gadafi,Aisha ambaye yupo nchini Algeria kutafuta taarifa kutoka kwa mamlaka mpya za Libya.


Hata hivyo mwanasheria  Kaufman amesema hakuna upande wowote wa serikali mpya uliokubali maombi yake ya kutaka taarifa juu ya kifo cha baba yake.

No comments: