Friday, March 9, 2012

Hana mikono, lakini anamudu kazi zake vema-Ni MwanaMama wa Sudan

Anaitwa Hokom Al, ni mwanamama wa huko Sudan ambaye alizaliwa miaka 45 iliyopita akiwa hana mikono kama unavyomuona. Mungu amempa uwezo wa kumudu kazi zake bila shaka yoyote. Hapa anamimina chai aliyowaandalia wageni majirani zake kwa kutumia mguu. Mungu ni muweza wa yote!

Hapa anaweka na anakoroga sukari katika chai hio kwenye kikombe

Hapa anaanika nguo na kuweka vibanio kwa kutumia mdomo, sijajua kama pia alizifua yeye hizo nguo au kuna mtu alimsaidia, ila we jua kwamba Mungu ni muweza!

No comments: