Wednesday, December 5, 2012

Na Hamida Hassan
MWANAMUZIKI, Mwingereza Athuman ‘Tanzanite’ ameibuka na madai mazito kuwa, eti msanii mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemroga.

 
Mwingereza Athuman ‘Tanzanite’.
Akizungumza katika kituo kimoja cha redio jijini Mwanza hivi karibuni, Tanzanite alidai kuwa aliugua sana kifua ambapo alifikia hatua ya kutoa makohozi yenye damu yaliyochanganyika na nywele.
“Nilikwenda hospitali lakini hali ilizidi kuwa mbaya, tukageukia kwa waganga wa kienyeji, lakini kila sehemu tuliyokuwa tukienda tulikuwa tukitajiwa jina la Nasibu kuwa ndiye aliyenifanyia ‘mandingo’.
“Nilikuwa sitaki kuamini moja kwa moja lakini nikawa najiuliza kwa nini sehemu tisa nilizoenda nitajiwa mtu huyo tu?
“Nikiangalia sababu, wazee hao walikuwa wananiambia kuna vitu tulikuwa tunagombania na huyo mtu, hao wazee wenyewe hawajui ni vitu gani,” alidai Tanzanite.

Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Diamond ili azungumzie madai hayo lakini hakuweza kupatikana mara moja, jitihada za kumpata zinaendelea.
Diamond na Tanzanite waliwahi kuingia kwenye bifu kisa kikiwa ni Tanzanite kugandamizia biti ya wimbo wa Mbagala katika wimbo wake Kafara.


No comments: