Friday, May 17, 2013



Askofu Mkuu Mstaafu Mtega azungumza na waandishi wa habari

 
 Baba Askofu Mstaafu Norbert Mtega, akijibu maswali ya waandishi wa habari mkoani Ruvuma.
Picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi hao.(Picha na Juma Nyumayo)
--------------------------------------------------------- 

Na Nathan Mtega,Songea




 SIKU moja baada ya Askofu Mkuu wa jimbo kuu la Songea Mhashamu Norbet kutangaza kustaafu nafasi hiyo kauli ambayo ilizua maswali na mijadala mingi miongoni mwa waumini wa kanisaa katoliki nchini na wananchi kwa ujumla ameamua kuzungumza na waandishi wa habari mjini Songea kufafanua zaidi kuhusiana na uamuzi wake huo.




Alisema kuwa ni wazi kuwa uamuzi huo aliouchukua umewashitua wengi lakini amelazimika kufikia uamuzi huo kufuatia kukumbwa na matatizo ya kiafya yaliyojitokeza kwake katika siku za hivi karibuni ambayo hakuwahi kuyapata kwa miaka mingi ya maisha yake pamoja na utume.




 Askofu Mtega aliwaambia waandishi wa habari kuwa yeye ataendelea kuitwa Askofu mkuu mstaafu na amepanga kuendelea kuishi ndani ya jimbo kuu la Songea  na yuko tayari kueendelea kutoa ushurikiano kwa kiongozi mwingine atakaeteuliwa kushika nafasi hiyo huku akiiasa jamii kuishi kwa amani na utulivu na kuepuka kubaguana kwa misingi ya dini,ukabila na itikadi za kisiasa bali waweke moyo wa uzalendo wa taifa mbele.




Alisema kuwa ameona ni vyema akakaa pembeni ili aweze kupata muda mzuri wa kupumzika na kupata matibabu ili afya yake ikitengamaa aweze kuwa mashauri mzuri kuliko kuendelea kunga’ang’ania mpaka afikike hatua ya kupoteza kumbu kumbu na kuwa kikwazo na hoja ya jimbo kuzorota katika siku za mbele.




 Akijibu maswali ya baadhi ya waandishi wa habari kuhusiana na mambo ambayo angependa ayaone yakifanyika alisema kuwa suala la elimu nchini siyo la kulipuuza na linapaswa kuwekewa misingi mizuri na imara kuanzia ngazi ya elimu ya msingi kwa sababu utaratibu uliopo wa kufanyia marekebisho alama za wahitimu waliofeli katika mitihani haulisaidii taifa kielimu pamoja na uhifadhi wa mazingira ambayo yanaendelea kuharibiwa kwa kasi kubwa na jukumu la kuvinusuru hivyo vyote ni la kila mmoja kwa maslahi ya taifa.




 Aidha aliwataka viongozi wa kanisa katoliki jimboni humo kujikita zaidi katika kuimarisha imani kwa waumini katika kanisa hilo ambalo yeye amelitumikia kwa kipindi cha miaka 22 na Jimbo la Iringa ambalo alilitumikia kwa kipindi cha miaka sita ambalo kwa sasa linaongozwa na Askofu Tarciusi Ngalalemkutwa ambaye sasa ataliongoza pia jimbo kuu hilo la Songea linaloachwa na Askofu Mtega.

No comments: