Wednesday, September 15, 2010

Mfanyabiashara abomolewa nyumba yake


Kwa Hisani ya GPL
Nyumba iliyopo kwenye plot namba 157 ya Shaban Makumlo (pichani) Mbezi Beach Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, hivi karibuni ilibomolewa na kundi la vijana huku familia iliyokuwa ikiishi ikiwa ndani, anaripoti Makongoro Oging’.

Chanzo chetu cha habari kimedai nyumba hiyo ambayo ujenzi wake uligharimu zaidi ya shilingi milioni 100 imebomelewa huku Shabani akiwa amefungua kesi Mahakama Kuu, yenye jalada namba 18/2010 kuhusiana na mgogoro unaohusu eneo alilojenga nyumba hiyo, lakini kabla ya kutolewa uamuzi amevamiwa na nyumba kubomolewa.

“ Shabani alipopata taarifa ya kuvamiwa kwa mji wake alifika eneo la tukio na kukuta zoezi la ubomoaji linaendelea, aliwasihi watoke lakini waliendelea ndipo alipiga risasi hewani kwa lengo la kuwatawanya,” kilisema chanzo hicho.

Imeelezwa kuwa, licha ya kuwatisha kwa kupiga risasi juu, vijana hao waliendelea na ubomoaji ndipo alimjeruhuwi mmoja pajani jambo lililowafanya wenzake wasogee mbali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Elias Kalinga alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa analifanyia uchunguzi.

No comments: