
Kwa Hisani ya Jiachie Blog
Habari za kuvunjika vunjika zilizoifikia JIACHIE mapema leo asubuhi zinaeleza kuwa mmoja wa Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Fred Marik a.k.a Mkoloni (kulia) ambaye pia ni Mwanachama wa chama cha CHADEMA inadaiwa leo mapema asubuhi akiwa ameambatana na msanii na mwanachama mwenzake G.Solo walikwenda kupata kifungua kinywa maeneo ya MEEDA BAR-Sinza jijini Dar.Inadaiwa kuwa wote wawili waliamua kupata mtori eneo hilo,lakini katika hali isiyo ya kawaida mmojawao (Mkoloni) akaanza kujisikia vibaya kwa kusumbuliwa na tumbo na kuanza kuishiwa nguvu,Habari zinazidi kudatisha kuwa baada ya kutokewa na hali hiyo ikabidi watu wamkimbize haraka zahati ya karibu maeneo ya Palestina-Sinza kwa huduma ya kwanza.
Habari zinaeleza kuwa mara baada ya kufika kwenye zahanati hiyo na kuchukuliwa vipimo,ikabainika kuwa bado tatizo halijaonekana kuwa ni nini ama ni kitu gani, hivyo wakashauriwa waende hospitali ya Mwananyamala kwa vipimo zaidi,kukawa hakuna namna ikabidi wampeleke hospitali ya Mwananyamala ambapo mgonjwa huyo alipatiwa vipimo na kubainika kuwa alichokunywa kilikuwa kimewekwa madawa ya kulevya, Kwani mgonjwa huyo alikuwa akikoroma sana na kuonekana kama mtu aliyepoteza fahamu..
Kwa mujibu wa taarifa zilizokuwa zikiingia ndani ya JIACHIE , ni kwamba msanii huyo bado amelazwa katika hospitali hiyo kwa matibabu zaidi.Wadau habari ndiyo hiyo tuendelee kuvuta subra zaidi kwani kuna mdau mkubwa wa JIACHIE amenitonya anakwenda hospitalini hapo kumjulia hali msanii huyo
No comments:
Post a Comment