Thursday, January 26, 2012

Kasheshe nzito apata Waziri Mkuu wa Australia

Waziri Mkuu wa Australia mwana mama Julia Gilad akisindikizwa mzobemzobe na wa askari na walinzi wake kutoka katika sherehe ya utoaji zawadi huko Canberra leo Alhamisi January 26, 2012. Alitolewa mbiombio mara baada ya kundi la kabila la  Aboriginal (watu wa asili wa nchi hiyo) kuvamia ukumbi. Muangalie hadi kiatu kimoja kimevuka. 

Mlinzi wake akijitahidi kumwepusha na hatari ya wavamizi hao wa Aboriginal. Kwanza alijificha ndani ya jengo kwa takriban dakika 20, kisha ndio ukafanyika mpango wa kumtorosha.

No comments: