Thursday, January 26, 2012

Polisi wa Colombia wateketeza mitambo ya Mihadarati

Askari wa kikosi maalum cha kupambana na dawa za kulevya wakiwa WAMELIPUA mitambo haramu ya kutengenezea dawa hizo huko Puerto Concordia, Colombia jana Jumatano January 25, 2012. Zoezi hilo lilikua ni kupambana pia na waasi wa FARC na kuharibu miundombinu yao, ambapo viwanda haramu 17 viliharibiwa, ndege 2, boti 22, kilo 692 za unga wa Coca na tani 13 za michanganyiko mbalimbali ziliharibiwa pia. Watu 10 walikamatwa kuhusishwa na tukio hilo

Helikopta mbili (Hii ya karibu na ile ya mbali) zikiruka juu ya anga la Puerto Concordia wakati wa zoezi hilo

Askari wa kikosi maalum cha kupambana na dawa za kulevya wakikagua mitambo haramu ya kutengenezea dawa hizo huko Puerto Concordia, Colombia

No comments: