Thursday, January 26, 2012

Mabadiliko makubwa Facebook, kuwa makini


Facebook ikiwa ni nyumba ya online kwa mamilioni ya watu duniani, hivyo mabadiriko yanayotokea kwenye facebook ni dhahiri yanaathiri kwengi wetu. Katika siku za karibuni Facebook wamekuja na kitu kipya mbacho wenyewe wanakiita Timeline , hii Timeline ni mpangilio mpya wa kurasa ya facebook ambao unamuwezesha mtumiaji kupanga picha,matukio nk kulingana na muda husika. 
Picha inayoonesha muonekano wa timeline ndani ya Facebook.
 Katika Timeline, utaweza kupanga taarifa zako kwa mtindo wa kipekee zaidi huku ikimpa nafasi mtembeleaji kuzipitia kwa haraka zaidi. Kama utaangalia picha ya hapo juu, utaona kwenye timeline yangu mtu akija mara ya kwanza ataona marafiki,picha na mengine meengi. Siyo hayo tu, kwa kutumia timeline mtu anaweza kuangalia matukio yako toka siku ya kwanza uliyojiunga na facebook.
 Katika siku zilizopita Timeline ilikuwa ni kwa wanaohitaji, ila kuanzia tarehe moja mwezi wa pili timeline itakuwa ni lazima, utake usitake ni lazima utumie au kwa lugha ya kiufundi tunaweza iita de
fault. Hivyo usishangae kuona mabadiriko kwenye kurasa yako.

 Kitu ambacho kimenivuta kuandika hii makala ni kuwa, ingawa timeline ni nzuri na ya kuvutia, ila Facebook inaonekana wanazidi kufanya mambo kuwa magumu,nidhahiri kuwa kufanikiwa kwa facebook kumekuja kutokana na urahisi wa utumiaji. Hivyo kufanya mambo kuwa magumu kutawafanya watu wengi kuikimbia au kushindwa kuifungua hususan wale walio kwenye mgao wa bandwith (internet zilizo taratibu mno). Kuna siku niliwahi kuona mpachiko wa rafiki yangu ambaye ni mtumiaji mzuri mno wa faceboo, yeye alikuwa akilalamika kwa kusema nani amesema tunataka hii timeline?


 Kitu kingine kikubwa ambacho kinaniumiza kichwa ni privacy, facebook wenyewe mara kibao wamekiri kuwa privacy ni moja ya vitu vinavyowaumiza kichwa, kwenye facebook ya sasa mtu anaweza kuona matukio yako ndani ya wiki hadi mwezi,ila sasa kwenye hii timeline mtu anaona tukio tangu siku ya kwanza uliojiunga facebook, sasa  huku si kuwaumbua watu?  Chukulia mfano kwa wale wenzangu na mimi wazee wa kuongopa, huu si ndio mwanzo wa kukamatwa?  Hivyo basi kwa kuweka timeline kuwa default kutawatatiza wengi. Habari njema ni kuwa kuanzia sasa unaweza kuanza kufuta matukio kadhaa usiyopenda kuwaonesha watu hadi hapo januari 31.
 Je wewe unalionaje hili?

No comments: