Tuesday, January 17, 2012

Papa ajeruhi na kuua mtu Afrika Kusini

Waokoaji wakiwa wanamtoa mtu aliyejeruhiwa na papa baharini katika pwani ya mashariki ya bandari ya St. Johns huko Afika Kusini juzi Jumapili January 15, 2012. Kaubao ka kutelezea kwenye maji (Surfboard) ndiko kalikotumika na muokoaji kujikinga na papa huyo wakati akiwa kwenye zoezi la uokoaji. Msemaji wa kituo cha afya alikopelekwa mtu huyo, Sizwe Kupelo alisema mtu huyo alipata majeraha makubwa mikononi na kifuani baada ya kupambana na papa huyo kwa zaidi ya dakika 5. Mtu huyo alitibiwa eneo la tukio lakini alifariki baadae wakati anapelekwa hospitali. Huzuni sana,

No comments: