Wednesday, May 30, 2012

Usikubali kila "OFA"

Jamaa kaingia Bar na kukuta watu wametulia wanapiga mambo yao,nae akaanza kutoa oda kwa mkwara kama ifuatavyo:-

Jamaa: "Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji,maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji."

Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,

Jamaa: "Muhudumu nipe supu na kila mutu humu ndani mupe supu maananinapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu."

Watu wakapewa supu,tena safari hii wakapiga makofi kumpongeza.

Jamaa: "Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mupe bili maana wakatinalipa bili yangu kila mutu lazima alipe yake."

Zogo lilianzia hapo.... Tabiri kilichotokea

No comments: