Thursday, May 31, 2012

WABUNGE WA CHADEMA WAANGWA RASMI KWA KUANGALIA MECHI YA KIMATAIFA



Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe, Peter Msigwa na Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, wakiwa na uongozi wa tawi la Chadema Washington DC, Libe Mwangombe, (wa nne kulia), Mjomba a.k.a Cosmas, Mzee wa swahilivilla Aboh Shatry (wa pili kulia), pamoja na mashabiki wa US, wakiiunga mkono bendera ya taifa.

Idadi ya wapenzi waliohudhuria katika mpambano huo ni 67,656 wakiwemo Mhe. Nassari Joshua pamoja na Mhe. Peter Msigwa.


Wabunge wa chama cha Chadema wakipata flash ya pamoja na warembo wa Kibrazil ndani ya uwanja wa FedexField, uliopo Landover Maryland nchini Marekani.


Picha ya pamoja na viongozi wa juu wa Chadema kwenye mpambano wa US na Brazil usiku wa kuamkia leo Alhamis Mei 31,2012 ndani ya ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland nchini Marekani.

Nabendera ya taifa wakishangilia Bao la kwanza la Brazil lilifungwa kwa Penalti na mchezaji Neymar.

Wachezaji wa Brazil wakilinda ngome yao kwa kuwadhibiti wachezaji wa timu ya US kwenye mechi hiyo ya kirafiki ambapo timu ya Brazil waliweza kuwabamiza US bao 4-1 nyumbani kwao.

US hoi kwa Brazil baada ya kubamizwa bao nne bao la kwanza lilifungwa na Neymar, la pili na Thiago mnamo dakika ya 11, kipindi cha kwanza. Bao la US lilifungwa na Hercules Gomes dakika ya 44 kipindi cha kwanza hadi mapumziko Brazil 2 US 1 kwenye mchezo wa kirafiki.

Forward wa United States, Landon Donovan, akipandisha majeshi juu huku akidhibitiwa na mlinzi wa Brazil Marcelo katika mpambano wa kirafiki.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa katika uwanja wa FedexFeild, uliopo Landover Maryland nchini Marekani.
---
Baada ya kazi kubwa ya kuzindua na kuimarisha tawi la Chadema Washington DC, Maryland na Virginia, Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Peter Msigwa na Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, usiku wa jana Jumatano Mei 30, 2012 waliagwa rasmi kwa kuangalia mpambano wa kimataifa kati ya US na Brazil ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland nchini Marekani.
(Picha / maelezo na swahilivilla.blog spot.com)

No comments: