Mashabiki hawakuonekana kulifurahia Vazi laleo la Wema
imeonekana kama kawabania hivi kwani ni tofauti na walivyo
tegemea.Sababu si ushaijua lakini?Hahaha endelea kuenjoy picha nyingine
uone jinsi show ilivyo bamba.
Wasanii
wa Filamu hapa nchini Aunt Ezekiel,Wema ambae amaependeza sana nadhani
pamoja na Shilole wakiwasikiliza mashabiki wao wanataka nini.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Diamond akiwaimbisha
mashabiki na wapenzi wa muziki huo waliojitokeza kwa wingi usiku huu
kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,kwenye uwanja wa Sokoine,mkoani
Mbeya.
Wasanii wa Filamu hapa nchini Aunt Ezekiel,Wema pamoja na Shilole wakiwasikiliza mashabiki wao wanataka nini.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Diamond akiwaimbisha
mashabiki na wapenzi wa muziki huo waliojitokeza kwa wingi usiku huu
kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,kwenye uwanja wa Sokoine,mkoani
Mbeya.
Msanii wa bongofleva kutoka THT,Barnaba akiwaimbisha mashabiki wake
usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2012 ndani ya uwanja wa
Sokoine mkoani Mbeya.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah akiimba kwa hisia jukwaani
usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwenye uwanja wa
Sokoine,Mkoani Mbeya.
Mashabiki kibao.
Mashabiki kibao.
Wadau wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea usiku huu.
Watu kibao ndani ya sokoine usiku huu.
Mmoja wa wasanii mahiri wanaotikiza kwenye anga ya muziki wa
bongofleva hasa katika miondoko ya R&B,Ben Paul akikamua vilivyo
jukwaani huku mashabikiwa wake wakishangilia kwa shangwe.
Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mh. Dkt. Norman Sigallah
akimtaja mshindi wa gari aina ya Vits itolewayo na kampuni ya Push
Mobile,ikiwa ni sehemo mojawapo ya mchakato wa tamasha la Serengeti
Fiesta 2012,anayeshuhudia ni Meneja masoko wa Push Mobile Rugambo Rodney
na kulia ni Chiku Saleh kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ,ambapo
katika bahati nasibu hiyo iliyochezeshwa,aliyeibuka mshindi ni Eva B
Mgovani.
ni full kujiachi tuu ndani ya uwanja wa sokoine usiku huu.
Pichani kati ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mh. Dkt. Norman Sigallah
akiwa katika picha ya pamoja na Meneje vipindi wa Clouds FM,na mdau
mwingine.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya anaefananishwa na mashabiki wake
kama Ray C,aitwaye Recho kutoka THT akitumbuiza jukwaani usiku huu ndani
ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012
Mashabiki wakishangilia vilivyo usiku huu,huku makamuzi ya wasanii yakiendelea jukwaani.
Msanii wa bongofleva anaetikisa kwa nyimbo kadhaa ikiwemo,Mama
halima,Aifora na nyinginezo akiwaimbisha mashabiki wake kama
waonekanavyo pichani usiku huu.
Mkali mwingine anaekuha juu katika mambo ya kuchana a.k.a kughani
Stamina akiamsha kitim kitim kwa wakazi wa mji wa Mbeya usiku huu ndani
ya tamasha la Serengeti Fiesta.
Linah akicheza na Shabiki wake ndani ya viwanja vya Sokoine mkoani Mbeya jukwaa la Serengeti Fiesta 2012.
No comments:
Post a Comment