Thursday, February 24, 2011

Huyu ndio mmiliki wa Dowans

Brigetia Jenerali Mohamed Al Adawi ndie mmiliki wa Dowans-Ila alikuwa wapi siku zote asijitokeze?

Ukitwanga ni lazima Upepete

Wacheza show wakiwa kazini
Si mchezo ati!

Mambo 8 unayohitaji kuyajua kuhusu Didier Drogba!

Drogba na Mkewe aitwaye LALLA DIAKITE
Nadhani wengi mnamfahamu, jamaa anaitwa DIDIER YVES DROGBA TEBILY, ni mshambuliaji nyota wa Timu ya wazee wa 'Darajani' CHELSEA ya England. hAya ni mambo kadhaa usiyoyajua kuhusu uyu 'Mshkaji'. Amezaliwa tar 11 march 1978 kule YOUMOSSOKRO mji uliko kusini mashariki mwa IVORY COAST.
2. Akiwa na umri wa miaka mitano wazazi wake waliacha kazi ivyo walimuomba mjomba ake aitwae MICHAEL GOBA aliekuwa anacheza soka Ufaransa amchukue akaishi nae Ufaransa baada ya hali yao kimaisha kuwa ngumu!
3. Alipenda sana kumsaidia Mjomba ake kusafisha viatu vyake vya Soka huku akimwambia kwamba nae anataka akacheze mpira na watoto wenzake ndipo mjomba ake akatambua kwamba kume nae anapenda kucheza mpira.
4. Ana wadogo zake wawili waitwao JOEL DROGBA na FREDY DROGBA mwenye miaka 18 anayeichezea timu ya LEMANS ambao pia ni wanasoka mahiri wanaocheza soka nchini Ufaransa.
5. Mama yake hupenda kumwita Drogba jina la 'TITO' kutokana na kumpenda aliyekuwa Dikteta wa zamani wa Yugoslavia aitwae JOSIP BROZ 'TITO'.
6. Anapenda sana kula kuku na wali na pia Mahindi yaliochanganywa na Maharage aka 'MAKANDE!
7. Ameoa na mkewe ni raia wa MALI aitwae LALLA DIAKITE ambaye walikutana Paris Ufaransa na wamejaaliwa watoto watatu huku mtoto wake mkubwa aitwae ISAAC akielekea kuwa Mwanasoka ajae kama babake!
8. Mkewe ni muislam wakati yeye Drogba ni Mkatoliki.

Msanii Tino ajitetea kwamba "HAKUNA KIBAYA NILICHOFANYA KATIKA FILAMU YA SHOGA"

Hii ndio Cover Picture katika filamu hiyo iitwayo "SHOGA"
Kwa Hisani ya ray blog
Hakuna kibaya ambacho nimecheza ndani ya Filamu ya SHOGA ambacho kitafanya serikali kuendelea kuifungia filamu yangu ya SHOGA isiingie mitaani,Hayo ni maneno ya Tinno ambayo aliniambia nilipokutana naye leo katika maeneo fulani hivi hapa Dar es salaam.Serikali aijafanya vibaya kwani inatimiza majukumu yake katika kujiridhisha kama filamu hii aijaenda kinyume na maadili yetu.Nina matumaini makubwa baada ya serikali kujiridhisha kwa kuiangalia filamu hiyo wataniruhusu kuisambaza.Mashabiki wangu wakae mkao wa kula kuisubiri kazi hiyo,Hayo ni maneno ya Tinno muhusika mkuu katika filamu ya SHOGA na pia ndio mmiliki wa Filamu hiyo

MAANDALIZI YA MTANANGE WA SOKA KATI YA BONGO MOVIE STAR NA BONGO FLEVA WAPAMBA MOTO

Timu ya Bongo Muvi
Ule mpambano wa kuchangia ndugu zetu waathirika wa Mabomu ya Gongolamboto pale uwanja wa Taifa umezidi kupamba moto baada ya kila timu kujinasua kutoka na ushindi.
Hawa ni timu ya Bongo Fleva wakiweka mikakati

Kila timu imejipanga vyema kuonyesha kandanda la kufa mtu na tunawaomba watu mjitokeze kwa wingi kuja kushuhudia mtanange huo ili kufanikisha malengo yetu ya kuchangia ndugu zetu

MUIGIZAJI STEPHEN KANUMBA ANENA KATIKA JUKWAA LA SANAA BASATA

Muigizaji maarufu wa filamu nchini Steven Charles Kanumba ameibuka na kusema kwamba, wasanii si chanzo cha kuporomoka kwa maadili katika jamii bali tatizo hilo linasababishwa kwa kiasi kikubwa na utandawazi unaombatana na mabadiliko ya teknolojia duniani.

Akiwasilisha mada kuhusu Harakati za kuivusha tasnia ya filamu katika ngazi za kimataifa kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kanumba alipuuza malalamiko kwamba, wasanii wa filamu wamekuwa chanzo cha kuipotosha jamii kupitia yale wanayoyaigiza na kusema kwamba,malezi na utandawazi ni tatizo kubwa kwa sasa katika taifa na wazazi hawana budi kudhibiti watoto wao ili kuwaepusha na wimbi hili.

“Maadili hayako katika filamu tu,tunapozungumzia maadili ni katika nyanja nyingi.Leo mtoto mwenye miaka tisa anamiliki simu tena yenye internet,humo anaangalia facebook na picha za ajabu halafu mtoto huyu akiharibika watu wanasema ni filamu,hii si kweli” alisisitiza Kanumba ambaye amecheza zaidi ya filamu 40 hadi sasa.
Aliongeza kwamba,kwa kawaida wanapoandaa filamu wamekuwa wakiandika umri wa watazamaji wake lakini wazazi wengi wamekuwa wakipuuza na kuwaacha watoto kuangalia filamu ambazo hawapaswi kuangalia.Alitaja filamu kama ya This Is It ambayo anasema kuna watoto hawaruhusiwi kuiangalia lakini wazazi na walezi wengi wanapuuza hilo .
“Filamu zetu tunazotengeneza zinakuwa na ujumbe kwa jamii,zinabeba masuala yaliyomo ndani ya jamii.Suala la nani aangalie kilichomo tumekuwa tukiziwekea umri wa watazamaji.Naomba mniambie jamani hayo tunayoyaonyesha katika filamu yetu hayapo katika jamii?Na kwa nini sasa tulaumiwe kwa mambo ambayo yako ndani ya jamii zetu” alihoji Kanumba.

Akizungumzia suala la wao kuwa waongozaji,waandishi wa simulizi (script writers) na watafutaji mandhari (location) katika filamu moja,Kanumba alisema kwamba,ni suala la kawaida na limekuwa likifanyika katika nchi mbalimbali duniani na mara nyingi hufanywa ili kukwepa mlolongo mrefu na pia kubana matumizi.
Juu ya wizi katika kazi zao,Kanumba alisema kwamba,Chama cha hakimiliki (Cosota) kimekuwa kikijtahidi lakini tatizo limekuwa kwenye nguvukazi ya mamlaka hiyo lakini pia sheria ambazo zinaonekana hazikidhi matakwa.

Hata hivyo,akizungumzia hilo kwa niaba ya Cosota,Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba,sheria mpya za hakimiliki ziko katika kiwango cha kupelekwa bungeni kwa ajili ya kupitishwa na uwezekano mkubwa ni kwenye bunge lijalo la mwezi wa nne.

Tuesday, February 22, 2011

Stara Thomas ameokoka!

Aliyekua muimbaji wa nyimbo za bongo fleva Stara Thomas sasa amempa Bwana Yesu maisha yake!
Hapo awali alisikika kwa nyimbo maarufu kama Sikia, Sitorudi nyuma, my body na Chldren rights ambapo hivi karibuni amevuma na wimbo wa nipigie alioshirikishwa na AT.
“Nilipata wito kutoka kwa Yesu kwa kuwa aliwaita watu wote wasumbukao na kulemewa na mizigo waende kwake atawapumzisha” alisikika akisema Stara
Awali alikua akiabudu dhehebu la Jamatrine kwa sasa anaabudu kanisa la Shalom lililoko Mbezi Salasala! Karibu kwa Bwana Yesu Stara!

Shetani ni mwizi wa mipango na malengo yetu!

Yeremia 28:11-12 “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho, nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza”

MIPANGO na MALENGO!

Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu, Tukisoma Neno hapo juu tutaona jinsi Mungu anavyotujali na kutuwazia mambo mema juu ya maisha yetu na ametupa uhuru kumwendea, kumuita ili yeye atusikilize. Hii ni juu Maisha yetu…kwamba anatuwazia mawazo ya amani wala si mabaya!

Kama kawaida shetani hakosi kujihudhurisha kwenye baraka zetu, anataka aibe yale Mungu amewaza kwetu. Yale unayowaza kufanya, biashara, huduma, kazi, familia yako, vipawa nk…kile Mungu ameweka kwako…shetani naye anataka akiharibu ili usifikie kwenye mpango sahihi Mungu aliokuandalia.

Lakini kama utaangalia na kulinda kile Mungu amekupatia, ile mipango na malengo yako, adui hawezi kukushinda. Maana utajua hila zake utamshinda, hatakupata. Shika sana ulichonacho!!

Yusufu Makamba adaiwa ‘kuua majirani zake kwa kiu’

Elizabeth Suleyman wa Gazeti la Mwananchi

KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, anadaiwa na wakazi wa Wazo Hill, jijini Dar es Salaam kujiunganishia maji nyumbani kwake yaliyopaswa kusambazwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Hata hivyo, Makamba amepuuza madai hayo akisema ana haki ya kuunganishiwa maji kama Mtanzania, ili mradi afuate taratibu na awe analipa ankara.Mwajuma Omari, mkazi wa eneo hilo, alisema wamekuwa wakitaabika kwa kukosa maji, kwa sababu bomba walilokuwa wakitegemea maeneo yao limeunganishwa kwa Makamba.

“Hivi sasa tunataabika na hatuji hatima yetu, ukiwaeleza Dawasco wanadai wataunganisha mabomba mengine na kuendelea kuchimba visima,” alisema Omari.Mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye hakutaka kutajwa, alisema toka enzi za Mzee Rashid Kawawa, wakazi wa eneo hilo walikuwa wanategema maji yanayotoka kwenye mabomba hayo.“

Tumekuwa tukijiuliza, iweje Dawasco waunganishe mabomba hayo kijanja kwa Makamba na kutufanya tukose maji kwa kulazimika kutumia ya kisima?” alihoji.

Akizungumzia suala hilo ofisini kwake jana, Ofisa Uhusiano wa Dawasco, Merry Lyimo, alipuuza malalamiko ya wakazi hao kuwa hayana msingi wowote na kwamba, mabomba waliyofunga kwa Makamba hayahusiani na wakazi hao.

Lyimo alisema walifunga bomba hilo kwa Makamba muda mrefu, hivyo malalamiko ya wananchi hao yakosa nguzo ya kusimamia. “Mbona wanamlalamikia yeye tu! Kwa sababu kama ni mabomba hayo tumeyafunga kwa watu wengi na kama hawana maji, Dawasco imejizatiti kuwawekea kisima ili wasikose kabisa,” alisema Lyimo na kuongeza:

“Hatujaona sababu za msingi za wao kulalamika... Makamba ni mteja wetu wa muda mrefu na tayari ameuganishiwa maji, hivyo wanapaswa kusubiri, mradi endelevu wa kuwaongezea visima vingine ili wasikose maji.”

Akizungumza kwa simu kuhusu malalamiko hayo, Makamba alisema yeye ni binadamu kama walivyo wengine, ana haki zote za kuunganishiwa maji.“Hao waliokueleza malalamiko hayo… siwezi kuyajibu ni vema ukaenda kwa walioniunganishia bomba la maji,” alisema Makamba na kuongeza:“Kigezo cha kuwa Katibu Mkuu wa CCM hakimaanishi sina haki ya kupewa maji, hivyo siwezi kuzungumzia hilo kawaulize Dawasco.”

Alisema aliomba kuunganishiwa maji tangu mwaka 1994, akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na alifuata taratibu zote.

Mmiliki Dowans utata mtupu

*Mbunge ataka akamatwe apigwe picha kwa nguvu
*Achanganya wananchi, wahoji maswali lukuki
*CTI wataka mitambo yake itaifishwe haraka

Na John Daniel-Gazeti la Majira

MBUNGE wa Ubungo Bw. John Mnyika ameitaka serikali kutumia vyombo vyake
vya dola kumtia mbaroni Bw. Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, aliyejitaja kuwa ndiye mmiliki wa Kampuni ya Dowans Holdings SA na kampuni tanzu ya Dowans Tanzania Limited.

Mbunge huyo amesema serikali inapaswa kuchukua hatua hiyo kwa madai kuwa mtu huyo alishakana kuhusika na kampuni hiyo wakati alipohojiwa kuhusu uhusiano wake na Dowans.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bw. Mnyika kwa vyombo vya habari jana, Bw. Al Adawi anapaswa kutiwa mbaroni kwa kuwa ametii kile alichosema katika tamko lake la Februari 16, mwaka huu la kutaka mmiliki wa mtambo huo ajitokeze.

Alisema katika tamko hilo aliitaka serikali itaifishe mitambo ya Dowans na kuiwasha kama sehemu ya kupunguza makali ya mgawo wa umeme na kuwataka wamiliki wake popote walipo duniani kujitokeza hadharani iwapo wana sababu za kuepusha mitambo yao isitaifishwe.

"Nilitarajia mmiliki wa Dowans ambaye angejitokeza angekiri hadharani kama wamedanganywa na kampuni ya Richmond na vyombo vingine katika kuhamishiwa mkataba ili kuweka msingi muhimu wa majadiliano, lakini imekuwa tofauti.

"Kutokana na hilo naomba kutoa rai kwa vyombo vya dola vimkamate vimpige picha na kumuhoji Al Adawi kwa mujibu wa sheria ya uhujumu uchumi na sheria nyinginezo kutokana na maelezo tata yaliyotolewa mpaka sasa kuhusiana na kampuni ya Dowans," alisema Bw. Mnyika katika taarifa yake.

Alidai kuwa kilichomshangaza ni kuwa siku chache baada ya tamko lake Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja, alinukuliwa na gazeti moja Februari 18 mwaka huu kuwa serikali haitataifisha mitambo hiyo kwa kuwa hiyo siyo sera ya CCM.

"Ikumbukwe kwamba katika gazeti la Mwanahalisi toleo namba 128 la Machi 2009 Al Adawi alikanusha kuwa yeye sio mmiliki wa Dowans kama alivyonukuliwa katika Mahojiano na KLHN.

Kama amekuwa akikanusha kuwa si mmiliki lakini sasa amejitokeza kuwa ndiye mmiliki kuna kila sababu ya vyombo vya dola kumuhoji zaidi," alisisitiza Bw. Mnyika

Alitaka vyombo vya dola vimuhoji Bw. Al Adawi kuhusu utata wa kampuni ya Dowans Holdings SA ambayo kumbukumbu zake kamili hazipo Costa Rica inapoelezwa kusajiliwa na kuwa na ofisi zake.

"Kwa kuwa sasa wanaotajwa kuwa wamiliki wa Dowans wameanza kujitokeza ni muhimu pia wamiliki wa kampuni ya Portek Systems and Equipment PTE Ltd ambayo inatajwa kumiliki hisa takribani 40% kwenye Dowans wakatajwa na wakajitokeza," alisisitiza.

Alirejea ushauri wake wa kuitaka serikali kuitaifisha mitambo ya Dowans na kuchukua hatua stahiki dhidi ya ukiukwaji wa sheria uliyojitokeza ili kuepusha kasoro zingine kujitokeza katika hatua za dharura zinazokusudiwa kuchukuliwa hivi sasa.

"Kutaifisha mitambo ya Dowans sio kutekeleza sera ya chama chochote, ni kuzingatia maslahi ya taifa na kusimamia utawala wa sheria ikiwemo sheria ya uhujumu uchumi,"alisisitiza Bw.Mnyika katika taarifa yake.

Mbali na Bw. Mnyika, baadhi ya wasomaji wa gazeti walikerwa na kitendo cha mfanyabiashara huyo kukataa kupigwa picha ili Watanzania waweze kumuona, isijekuwa aliyejitokeza ni mtu mwingine asiyehusika.

"Biashara ni matangazo kama ilivyo siasa. Wafanyabiashara na wanasiasa ni watu wanaopenda kupigwa picha na kujitangaza Watanzania, Huyu Al Adawi ni mfanyabiashara wa namna gani asiyependa kupigwa picha na kuonekana? Sisi tuna walakini na biashara yake," alisema Bw. Jerome John, mkazi wa Kigilagila.

Mkazi mwingine wa Ilala ambaye hakutaka kutaja jina lake, alionesha hasira kwa wanahabari kwa kushindwa kumlazimisha Bw. Al Adawi kumpiga picha au kutunmia mbinu za kipaparazi kunasa picha yake ili iweze kuonekana.

Katika hatua nyingine, suala la Kampuni ya Dowans limezidi kuwachanganya wabunge baada ya watumiaji wakubwa wa umeme kuhoji Kamati ya Nishati na Madini, sababu za kushindwa kuishauri serikali kutaifisha mitambo ya kampuni hiyo haraka kunusuru taifa.

Pia kamati hiyo ya bunge imetakiwa kujibu iwapo nchi haikufanya makosa kuingia katika mkataba na Dowans wakati bunge liliazimia kusitishwa kwa mkataba wa Richmond baada ya kubaini mapungufu kadhaa.

Katika kikao kilichofanyika Ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam jana kati ya Kamati hiyo ya Bunge na viongozi wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Baraza la Biashara la Taifa (TNB) na Mfuko wa Sekta Binafsi (TPSF) wadau hao walitaka kamati hiyo kuchukua hatua za haraka kunusuru uchumi wa nchi.

Vyanzo vyetu ndani ya kikao hicho vilieleza kuwa viongozi waandamizi wa taasisi hizo walionyesha wazi kukerwa na mjadala wa Dowans wakati nchi ikiwa katika hali ngumu ya umeme na kuitaka kamati hiyo kutoa majibu ya uhakika na kuweka siasa pembeni.

"Viongozi wa CTI, Bi. Esta Mkwizu, Bw. Arnold Kilewo na wale wa TPSF walituhoji ni kwa nini tunakazania tu kuzungumzia mitambo ya Dowans badala ya kuitaka serikali kununua mitambo yake.

Lakini kubwa zaidi walitaka mitambo ya Dowans itaifishwe haraka ili itumike kuzalisha umeme wa dharura kama mali ya nchi, walishangaa kwa nini nchi inapoteza mabilioni ya fedha bila sababu," kilisema chanzo chetu ndani ya kikao hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho viongozi hao wa wafanbiashara wakubwa ambao ndio watumiaji wakubwa wa umeme kwa asilimia 8,0 waliitaka kamati hiyo kueleza iwapo si kosa kwa nchi kuingia mkataba na Dowans wakati bunge iliazimia kuwa mkataba wa Richmond haukuwa halali.

Awali akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo yaliyojiri katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Januari Makamba alisema wadau hao walilalamikia ukosefu wa umeme na kwamba hali hiyo imelisababishia taifa hasara ya mabilioni ya fedha.

"Tatizo la umeme ni kubwa kiuchumi, kwa mfano Twiga Cement pekee licha ya kutumia jenereta bado wanapoteza karibu milioni 20 kwa siku.

Kama taifa tunapoteza karibu dola za Marekani 200,000 kwa siku kutokana na ukosefu wa umeme, hii ni hali mbaya sana, ndio maana tumelazimika kuzungumza kwanza na wadau kujua ukubwa wa tatizo kiuchumi," alisema Bw. Makamba.

Alisema katika kikao hicho ambacho kilikuwa bado haijafikia mwisho CTI waliweka wazi kuwa kati ya viwanda 280 vinavyomilikiwa na wanachama wake 50 wameshindwa kuendelea na uzalishaji na kusitisha kazi kwa muda kwa ukosefu wa umeme.

"Kama mnavyojua tunatakiwa kuanza vikao vyetu wiki mbili kabla ya bunge lakini tuliomba kibali maalumu kwa Spika kufanya vikao kutokana na ukubwa wa tatizo hili, leo (jana) tumekutana na wadau, kesho (leo) tutakutana na Wizara ya Nishati na Madini na kesho kutwa TANESCO.

"Pia Jumamosi tutaitisha public hearing (mdahalo wa wazi) pale Karimjee, tutaandaa vizuri ili tupate mawazo ya wadau kwa utaratibu mzuri," alisema Bw. Makamba.

Alisema Kamati hiyo itakutana na wadau wote wanaohusika na umeme wa gesi ili kutoa mapendekezo yatakayokidhi haja ya taifa kuondokana na adha ya sasa.

Alisema Kamati yake haijatoa mapendekezo yoyote kuhusu mitambo ya Dowans na kwamba kilichonukuliwa na vyombo vya habari yalikuwa maoni yake binafsi kabla ya kikao cha kamati hiyo.

"Kamati itatoa mapendezo yake kwa serikali Jumanne ijayo baada ya kumaliza kazi yake, kwa sasa tunaendelea na vikao ili kujua nini kinachotakiwa hasa kuokoa taifa letu na ukosefu wa umeme," alisema.

Alipoulizwa iwapo Kamati yake itamwita mtu aliyejitangaza kuwa mmiliki wa Dowans anayedaiwa kutua nchini juzi na kuzungumza na wahariri wa vyombo vya habari kwa sharti la kutopigwa picha alisema hawana sababu ya kufanya hivyo.

Hata hivyo alisema uamuzi wa serikali kutumia au kutotumia mtambo wa Dowans kuzalisha umeme wa dharura kwa sasa ni uamuzi tu na kwamba si jambo gumu na kufafanua kuwa kamati yake haiwezi kuishinikiza kufanya hivyo au kutofanya.

Alisema kabla ya kutoa mapendekezo yake kamati yake itafanya ziara kujionea hali halisi ya nishati hiyo katika vituo vyote vinavyozalisha umeme isipokuwa Mtera ambapo tayari wametembela.

Du Kikwete na Gbagbo uso kwa uso!

Picha moja ni sawa na maneno elfu moja.Ni kweli.Katika kuitazama picha hii,nimepata maneno mia tisa na tisini na nane na bado yanakuja.Ni picha ya Rais Jakaya Kikwete na wa Ivory Coast,Laurent Gbagbo(nashindwa kuandika neno linaloanza na R kwa huyu bwana) walipokutana jijini Abdijan nchini Ivory Coast.Amani,raha ya kukutana,tumaini jipya,ukombozi,uongozi wa ki-afrika,siasa kama mchezo bila uadui,nothing personal but policies and poltricks…maneno mengi…

Rais Kikwete ni miongoni mwa viongozi waliomo katika jopo maalumu la Umoja wa Afrika lililopewa jukumu la kujaribu kusuluhisha mgogoro unaorindima nchini humo kufuatia uchaguzi mkuu mwaka jana ambapo inaaminika na kukubalika na wengi kwamba mpinzani wa Gbagbo,Allasane Ouattara ndiye aliibuka mshindi halali.

Kumbuka kuisoma picha,kuangalia wote waliopo pichani kisha uandike insha yako kichwani au katika karatasi.Sijui unapata maneno mangapi?

Monday, February 21, 2011

Hatimaye huyu ndio MMILIKI WA DOWANS!

Mmiliki wa Dowans, Brigedia Jenerali (Mstaafu) Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, anayeishi Oman, ametua nchini na kuzungumza na vyombo vya habari katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, Dar es Salaam. Akiwa na wakurugenzi wawili Stanley Munai na John Miles, alisema amelazimika kuja kwa sababu amesikia watu wanadai hawamjui mmiliki wa Dowans, na kwamba wanawadhania baadhi ya Watanzania kuwa ndio wamiliki wa Dowans. Akasema: "Mimi ndiye mmiliki wa Dowans."

Akasema si kawaida yake kuzungumza na vyombo vya habari, na kwamba hataki kupigwa picha yoyote, kwa sababu yeye ni mfanyabiashara asiyependa makuu na asiye na makeke. Akasema amewekeza katika nchi 12 duniani, na kwamba katika zote hizo anawakilishwa na rafiki zake; na kwamba hapa nchini aliletwa na Rostam Aziz mwaka 2005 kwa ajili ya mradi wa Fibre Optic.

Katika hili la sasa, alisema amekuja kujadiliana na Tanesco juu ya hatima bora ya kibiashara kwake na fursa ya umeme kwa Watanzania, katika mazingira ya sasa ya mkataba unaodaiwa kuwa na utata, na deni la bilioni 94 analoidai Tanesco baada ya Dowans kuwashinda Tanesco mahakamani. Alizungumza kwa Kiingereza, na nimeweza kunukuu baadhi ya kauli zake moja kwa moja alipokuwa akijibu baadhi ya maswali na hoja za waandishi. Hizi hapa:

1. “I am here to find a happy resolution, a business decision. I am ready to offer something nice to Tanesco if it works out.”

2. “I don’t want to be known. I am a low-profile businessman. I walk free here in Dar es Salaam, and no one knows I own Dowans.”

3. “Rostam Azizi is a friend of mine. He invited me to come and invest here, but he didn’t put in any cent in the project.”

4. “I have businesses in 12 countries allover the world. I can’t go and represent myself in every country. That’s why I gave Rostam power of attorney.”

5. “We have not been tarnished, but we have been mixed up with something else (Richmond)”

6. “I do not need to be cleared by anyone; my electricity here will clear me.”

Tuzo za Muziki wa Injili (Gospel)

Balozi wa ZindukaProfesa J akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu Tamasha la Tuzo za wasanii wa mziki wa Injili linalotarajiwa kufanyika februali 27 Kulia ni Mratibu wa Tamasha hilo, Haris Kapiga.
********************************

TANZANIA Gospel Promoters (TGMP) kwa mara nyingine tena baada ya miaka mitano kupita wameandaa tamasha la Tunzo za Muziki wa Injili (Gospel Music Awards) lililopangwa kufanyika Februari 27 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo asubuhi katika mkutano na waandishi wa habari Mratibu wa Tamsha hilo Haris Kapinga kutoka Kampuni ya Clouds Media Haris Kapinga alisema tamasha hilo litatumika kuwapongeza na kufanya tathmini ya jumla kwa wasanii binafsi na tasnia nzima huku Tunzo mbalimbali zitatolewa.

Tunzo hizo ni wimbo bora wa mwaka, mwandishi bora wa mwaka, mwimbaji bora wa kike wa mwaka, mwimbaji bora wa mwaka wa kiume, kundi bora, msanii bora wa muiziki wa Injili wa mwaka na mwimbaji anayechipukia katika uimbaji wa nyimbo za Injili. Wimbo wa mwaka, video bora, Mtayarishishaji bora wa mziki wa video wa mwaka , Mtayarishaji bora wa muziki, Tunzo ya Jumuiya, Kwaya bora ya Akapela,Kwaya bora inayotumia ala, bendi bora ya muziki wa Injili, Kwaya bora inayotumia ala ya Piano.

“Jinsi watu watakavyoweza kupiga kura, kura zitaanza kupigwa Januari 29 mwaka huu na kufikia kilele cha February 12 huku fomu zote zilizopigiwa kura zitatakusanywa Februari 13” alisema Kapinga. Anaendelea kwa kusema kuwa mdhamini mkuu wa tamasha hilo ni Mradi wa kutokomeza Malaria , Zinduka ambao zaidi ya lengo kuu la kupambana na Malaria inatumia tamasha hili kuwaunganisha viongozi wa dini mbalimbali kwa kuanza na madhehebu ya dini ya Kikristo ili kupeleka ujumbe kuhusiana na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.

Tangu Mradi huo ulipoasisiwa nchini mwaka 2010 umekuwamradi wa kwanza unaofanya kazi kwa kushirikiana na sekta mbalimbali katika jamii ili kusimamia pamoja na kumaliza ugonjwa wa Malaria nchini kote.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa dini ambao ni Sister Mariana Francis kutoka Roman Catholic, Mchungaji David Mwasota ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste, Mchungaji Solomon na John Gao wa Makanisa ya Anglican, ambao wote kwa pamoja wamewakumbusha wana jamii na kuwahimiza Watanzania katika kujilinda, kuepukana na vifo vinavyoweza kuzuilika.

“Tunaimani kwamba kwa kutumia nguvu ya muziki wa Injili , mwamko na ufahamu kwenye jamii vitaongezeka sana huku jamii na waumini wakiunganisha nguvu ya kupambana na Malaria” alisema Mwasota.

Soucre: Bongo Weekend – 28/1/2011

Monday, February 14, 2011

nyboma et madilu - voisin (avec dally kimoko)

Unaifahamu "Wahapahapa Band?"

Bendi hii ni ya ‘watoto wa hapahapa nyumbani’, huu ndio msingi wa bandi hii kubandikwa jina la “Wahapahapa”.

Bendi hii ndio nguzo kuu katika shughuli nzima ya utayarishaji na kurekodi nyimbo zote unazozisikia katika mchezo wa radio wa “Wahapahapa”.

Tanzania, imethibitishwa kisayansi, kuwa ndio mama wa binadamu wote alizaliwa hapa, basi ukweli huu una kila sababu ya kututhibitishia kwamba hata mirindimo ya miziki yote duniani imezaliwa hapa, na hapa ndipo ilipo bendi ya “Wahapahapa”.

Bendi ya Wahapahapa inapiga muziki wake kuenzi utamaduni, si tu ule wa mtanzania, bali wa wanadamu wote. Wahapahapa pia inatumia muziki wake kusaidia wasikilizaji katika harakati zao za kujiletea maendeleo, na bila kusahau suala zima la kuienzi lugha tamu ya Kiswahili.

Aina ya muziki unaopigwa na bendi hii umebatizwa jina la “TanzRock”, na hili ndilo jina pia la albamu ya kwanza.

Aurlus Mabele et le Groupe Loketo- Tala Mamina

Aurlus Mabele et le Groupe Loketo- Canon Scie

Saturday, February 12, 2011

Thursday, February 10, 2011

Monday, February 7, 2011

Soukous Dance Promo - Diblo Dibala

Kujamba ni marufuku huko Malawi (Ashakum si Matusi)

Mzozo umezuka nchini Malawi kufuatia mapendekezo kutaka kufikishwa bingeni kuhusu kujamba, kuwa ni kosa. Waziri wa sheria wa Malawi, George Chaponda amesema muswada huo utakaojadiliwa kuwa sheria ndani ya bunge wiki ijayo, utapiga marufuku kabisa kwa mtu kufanya haja hiyo hadharani. Waziri huyo amekiambia kituo kimoja cha radio nchini humo- kwa maneno yake - "nenda chooni kama unajisikia kujamba". Hata hivyo mkuu wa wanasheria nchini Malawi Anthony Karanga amesema kufanya haja hiyo hakufikii kuharibu hali ya hewa kiasi cha kuwa kosa la jinai. Mwandishi wa BBC nchini humo anasema wananchi wa Malawi wanajiuliza mapendekeo ya sheria hiyo, iwapo itapitishwa, itatekelezwaje.

Congo - Diblo Dibala - Ann'Amour