Tuesday, January 31, 2012

Msikilize Pastor Posh na wimbo wake uitwao "Tawala"

Picha mbalimbali za Harrison Mwakyembe, Samuel Sita na James Lembeli

Kumbuka ameugua sana ugonjwa wa ngozi, ona amevaa kofia na glovu kuhifadhi mwili. Samwel Sita anasema kalishwa sumu. Du mi simo aisee wanajua wenyewe. Ila inasikitisha sana.

Samwel Sita madhabahuni kanisa la Ufufuo na Uzima kwa Mchungaji Gwajima Kawe Dar es Salaam

Walio katika mapambano na ufisadi, kushoto kwenda kulia ni Anne Kilango, Samwel Sita, James Lembeli na Harrison Mwakyembe.

Hapa Mwakyembe anaonekana kwa karibu, kulia kwake ni James Lembeli

Samwel Sita akishuka ngazi

Dreads/Rasta nyingi ninazoona mtaani huwa chafu kwa vile hazioshwi mara kwa mara, hizi je?

Muumini wa madhehebu ya Hindu aitwaye Sadhu akitikisa kwa nguvu dreads zake ili kuzikausha mara baada ya kuziosha katika mto, ambapo kwao wahindu hio ni sehemu ya ibada zao. Wachache sana huosha dreads zao. Nyingi hazigusi maji kwa miezi mingi tu. Usafi ni muhimu kuepuka harufu.

Baridi kali yauwa watu 36 Ulaya mashariki

Baridi kali sana yenye mawingu, ukungu na barafu kali imeshauwa watu takribani 36 hadi sasa huko Ulaya mashariki, hapa ni Arosa Switerland ambapo imefikia nyuzi -15 Centigredi, ni baridi kali sna kwa kweli.

Msichana akichungulia nje ya dirisha baada ya kuweka mkono kufuta barafu huko Ukraine Ulaya mashariki

Monday, January 30, 2012

Unakumbuka Tyson alivyong'ata sikio la Evander??

Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaska akikagua sikio la Bondia bingwa wa zamani wa uzito wa juu Evander Holyfield katika mji mkuu Colombo leo Jumatatu Januari 30, 2012. Evander aling'atwa kipande cha sikio na bondia Tyson mwaka 1997. Rais Rajapaska alimkaribisha Evander ikulu kunywa nae chai.

Jione taswira tofauti za Jengo la AU-Addis Ababa Ethiopia

Ni jengo la urefu wa mita 100, sawa na uwanja wa kabumbu toka goli moja hadi lingine.

Ni mambo ya Mchina (Hun Haa!)

Sio kila kitu cha Mchina ni kibaya

Hapa ni kwa ndani

Ukumbi wa mikutano

Kitu kimesimama wima, raha sana kutazama

Si mchezo aisee!!

Nimeipenda picha Hii!!

Lakini je Mtanzania akijipaka rangi za NCHI NYINGINE na akaishabikia ambayo si Tanzania, itakua ni USALITI au bado ni MZALENDO na ni kawaida?

Waliopigana vita Iraq wakaribishwa Marekani

Washiriki wa gwaride/maandamano ya heshima ya kuwapokea/kuwakumbuka waliopigana vita vya Iraq. Sherehe hio ilifanyika huko ST. Louis Marekani, wapo waliouawa na wapo waliorudi salama.

Mwanamama Stephanie King akiwa amebeba picha ya mjomba wake Kanali Stephen Scott alieuawa Iraq mwaka 2008. Stephanie alikua miongoni mwa walioandamana kuwapokea na kuwakumbuka maveterani wa vita vya Iraq.

Larry Connor, askari wa Marekani aliepigana vita vya VIETNAM akipiga salute kutoa heshima kwa askari wanaorejea toka Iraq. Kwa TANZANIA askari hatakiwi kupiga saluti kama hiyo hadi avae sare/uniform kamili ya jeshi. Huyu kavaa kiraia na amepiga. Jeshi letu TANZANIA lina NIDHAMU kubwa katika swala hili.

Ujumbe wa Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kuhusu Malaria-Gonga utamsikia Kikwete na wengine ingawa unamwona huyo mama!!

Watu 26 wauawa katika tukio la moto nchini Peru.

Miili ya watu waliuawa kwa moto ikiwa imelazwa mbele ya waokoaji na zima moto. Wapo walioungua na wengine walikosa hewa na tukio hilo lilitokea katika kituo cha ukarabati wa afya za watumiaji wa dawa za kulevya kitwacho "Christ is Love" huko Lima mji mkuu wa nchi ya Peru juzi Jumamosi Januari 28, 2012.

Baadhi ya ndugu wa watu waliokumbwa na tukio hilo wakifuatilia kwa majonzi zoezi la uokoaji. Ni huzuni kwa kweli

Friday, January 27, 2012

Usitawale nchi ukajisahau, huyu yamemkuta

Dikteta wa zamani wa nchi ya Guatemala Efrain Rios Montt afikishwa mahakamani kwa mauaji ya kimbali aliyofanya wakati akitawala nchi hiyo
Diktetea huyo akiwa mesimama katikati ya askari wa usalama wakati wa usikilizaji wa kesi yake jana Alhamisi Januari 26, 2012

Baadhi ya ndugu wa watu walioawa wakati wa utawala wa dikteta huyo, wakisikiliza kesi hiyo

Bango kubwa lenye baadhi ya picha za watu waliopotea na yaaminika waliuawa na dikteta  huyo Efrain Rios Montt 


Novak Djokovic amchapa Andy Murray katika nusu fainali-Tennis

Alimpa kichapo cha 6-3, 3-6, 6-7, 6-1, 7-5 katika mashindano ya Australian Open. Ona alivyolala kwa furaha.
Hapa akimpongeza kwa kushindana naye (Andy Murray ni huyo kulia) 
Novak akirudisha mpira

Andy akishangilia kushinda seti ya 3, lakini mambo yalimgeuka baadae

Hapa ndio shughuli nzima ilipofanyika

Tabiri kitakachotokea!!


Wajishona midomo na kujikata mwilini, akina nani na kwanini?

Mfungwa wa gereza la Bishkek nchini Kyrgyzstan akiwa amejishona mdomo wake jana Akhamisi Januari 26, 2012 kupinga hali mbaya katika gereza hilo. Hali mbaya zipo karibu magereza yote duniani sio Afrika peke yake. Ukumbuke gereza unaadhibiwa ingawa pia unafundishwa mambo kadhaa.

Angalia huyu alivyojikata mikononi, ni ujasiri haswa ila hauna maana kwavile anajiumiza mwenye, je akifa hiyo hali nzuri gerezani itamsaidia nini?

Ilibidi askari wa gereza watembelee vyumbani kuna hali halisi. Duniani kuna mambo. Kuishi kwingi kuona mengi.

Thursday, January 26, 2012

Mabadiliko makubwa Facebook, kuwa makini


Facebook ikiwa ni nyumba ya online kwa mamilioni ya watu duniani, hivyo mabadiriko yanayotokea kwenye facebook ni dhahiri yanaathiri kwengi wetu. Katika siku za karibuni Facebook wamekuja na kitu kipya mbacho wenyewe wanakiita Timeline , hii Timeline ni mpangilio mpya wa kurasa ya facebook ambao unamuwezesha mtumiaji kupanga picha,matukio nk kulingana na muda husika. 
Picha inayoonesha muonekano wa timeline ndani ya Facebook.
 Katika Timeline, utaweza kupanga taarifa zako kwa mtindo wa kipekee zaidi huku ikimpa nafasi mtembeleaji kuzipitia kwa haraka zaidi. Kama utaangalia picha ya hapo juu, utaona kwenye timeline yangu mtu akija mara ya kwanza ataona marafiki,picha na mengine meengi. Siyo hayo tu, kwa kutumia timeline mtu anaweza kuangalia matukio yako toka siku ya kwanza uliyojiunga na facebook.
 Katika siku zilizopita Timeline ilikuwa ni kwa wanaohitaji, ila kuanzia tarehe moja mwezi wa pili timeline itakuwa ni lazima, utake usitake ni lazima utumie au kwa lugha ya kiufundi tunaweza iita de
fault. Hivyo usishangae kuona mabadiriko kwenye kurasa yako.

 Kitu ambacho kimenivuta kuandika hii makala ni kuwa, ingawa timeline ni nzuri na ya kuvutia, ila Facebook inaonekana wanazidi kufanya mambo kuwa magumu,nidhahiri kuwa kufanikiwa kwa facebook kumekuja kutokana na urahisi wa utumiaji. Hivyo kufanya mambo kuwa magumu kutawafanya watu wengi kuikimbia au kushindwa kuifungua hususan wale walio kwenye mgao wa bandwith (internet zilizo taratibu mno). Kuna siku niliwahi kuona mpachiko wa rafiki yangu ambaye ni mtumiaji mzuri mno wa faceboo, yeye alikuwa akilalamika kwa kusema nani amesema tunataka hii timeline?


 Kitu kingine kikubwa ambacho kinaniumiza kichwa ni privacy, facebook wenyewe mara kibao wamekiri kuwa privacy ni moja ya vitu vinavyowaumiza kichwa, kwenye facebook ya sasa mtu anaweza kuona matukio yako ndani ya wiki hadi mwezi,ila sasa kwenye hii timeline mtu anaona tukio tangu siku ya kwanza uliojiunga facebook, sasa  huku si kuwaumbua watu?  Chukulia mfano kwa wale wenzangu na mimi wazee wa kuongopa, huu si ndio mwanzo wa kukamatwa?  Hivyo basi kwa kuweka timeline kuwa default kutawatatiza wengi. Habari njema ni kuwa kuanzia sasa unaweza kuanza kufuta matukio kadhaa usiyopenda kuwaonesha watu hadi hapo januari 31.
 Je wewe unalionaje hili?

Bomu walilolengwa askari wa NATO lawauwa waAfghanstan 4

Moshi ukipanda angani baada ya bomu la kujitoa mhanga lililotegwa katika gari kulipuka huko Lashkar Gah katika jimbo la Helmand nchni Afghanstan leo Alhamisi January 26, 2012. WaAfghanstan 4 waliuawa na wengine 31 kujeruhiwa, amesema hayo Bwana Dawood Ahmadi msemaji wa Gavana wa jimbo hilo. Bomu hilo lililengwa kwa kikosi cha NATO kinachotoa misaada eneo hilo lakini likauwa watu wasiokusudiwa kabisa. Ugaidi haufai.

Gari lenyewe lililolipukiwa na bomu ndio hili hapa eneo la tukio

Je mjadala wa VAZI LA TAIFA ni muhimu kwa waTanzania muda huu?




WAKATI nchi ikikabiliwa na matatizo mengi makubwa na mazito, serikali kwa kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imezua kwa mara nyingine tena mjadala usiokuwa na tija yoyote kwa wananchi hususani walalahoi – mjadala wa kutafuta vazi la taifa!
Mjadala huu hauna tija yoyote kwa Watanzania, ukiondoa watu wachache ambao hawana mipango yoyote ya maana kwa jamii.  Hawa ni watu ambao wana fursa za kila siku kwenda Ulaya na sehemu nyingine duniani ambapo wanachokitaka ni kujulikana wanatoka Tanzania!
Ni aibu kwamba wakati kama huu ambapo serikali ingekuwa inaendesha mijadala muhimu kama  kuandikwa kwa katiba mpya, inakubali watu kupoteza muda na raslimali kwa ajili ya kujadili magauni na mashati ambayo Watanzania wanatakiwa wayavae wakiwa ndani au nje ya nchi hii.
Kwa kifupi, hivi tunatafuta vazi la taifa ili iweje?  Na tukishalipata vazi la taifa na kuanza kulivaa litatuongezea chumvi kwenye mboga au sukari kwenye chai?




Je, nchi gani miongoni mwa hizi zina vazi rasmi la taifa?  Au, je, ni lini ziliwahi kukaa na kupoteza muda kujadili vazi la taifa?

Kwa nini Watanzania tusiutumie muda wetu wa masaa 24 ya siku moja kujadili ukosefu wa maji ya kunywa katika sehemu kubwa ya nchi hii?  Kwa nini tusianzishe mijadala angalau ya kurudisha uhai wa Reli ya Kati ambayo inabidi iwahudumie mamilioni ya watu nchini?

Nani aliwahi kusema vazi la taifa huja kwa kujadiliwa kwenye vikao?  Nani aliwahi kusema, kwa mfano, mtindo wa muziki hujadiliwa kwenye vipindi vya radio na televisheni?

Hivi mtindo kama “Ndombolo” wa Congo na “Kwaito” wa Afrika Kusini ilijadiliwa kwenye vijiwe vya Kinshasa na Cape Town?

Mitindo hiyo ya muziki ilikuja yenyewe.  Haikujadiliwa vijiweni au redioni!

Vivyo hivyo, mitindo ya uvaaji wa watu wa Afrika Magharibi, kama vile Nigeria, Ivory Coast, Guinea, Mali, na kadhalika, ilikuja yenyewe. Hakuna vikao vilivyofanyika na kupendekeza aina hiyo ya uvaaji.


Kwa nini tunashindwa kuelewa ukweli huo mdogo ambao hata watoto wa shule za msingi wanaufahamu?

Kuna wakati wapenda muziki walikaa na kuamua eti mtindo wa dansi nchini uitwe “Achimenengule”!  Kilichofuata ni kwamba uamuzi huo uliishia kwenye meza walizokuwa wamezikalia wakati wa majadiliano hayo.

Hapakuwa na “Achimenengule” wala nini hadi leo!
Mtindo wa mavazi au kitu chochote huwa havipangwi, hujitokeza vyenyewe kwa kukubalika kimyakimya kwa watu – si kwa kutangazwa!

Hivi hatuna kitu cha maana cha kujadili kwa manufaa ya watu wengi? Kwa nini Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni inakubali kujishusha kiasi hicho wakati majuzi tu ilishindwa kuisafirisha timu ya wanawake ya taifa ya soka kwenda Namibia wakati kila mwaka inapewa bajeti nono na bunge?

Iwapo tatizo ni Watanzania kutaka kujulikana nje ya nchi, basi dawa yake ni ndogo sana.  Mtanzania anayetaka kujulikana akiwa nje ya nchi hii ni kuvaa nguo yoyote na akaiandika kwa maandishi makubwa sehemu yoyote, kwa mfano: “I am a Tanzanian” (kwa Kiingereza), “Je suis un Tanzanien” (Kifaransa)  au “Yo soy on tanzano” (Kihispania).
Yote hayo yanamaanisha kwamba: “Mimi ni Mtanzania”.
Hiyo inatosha kabisa kuwafanya watu wakufahamu kwamba unatoka katika nchi mojawapo za bara maskini la Afrika.  Inatosha!

Huna haja ya kuchora picha ya twiga au mlima Kilimanjaro kwani twiga ni wengi sana duniani achilia mbali milima mirefu zaidi ya Kilimanjaro.

Hata hivyo, kwa kifupi kabisa: Watu waliopania kwamba Tanzania lazima iwe na vazi la taifa ambalo litawatambulisha wakiwa ndani na nje ya nchi hii, wasipoteze muda kulitafuta – watumie mavazi ya Kimasai!

Ni mavazi yenye kuvutia na ni ya kipekee ambayo Mtanzania akivaa nje ya nchi hii ni hakika watu watamshangaa na kumfurahia.

Kama vazi hili watu hawalitaki basi ni heri tujadili jinsi ya kuzipatia shule za sekondari za kata kompyuta, tujadili jinsi ya kusomesha na kuwalinda maalbino nchini, tujadili jinsi ya kupunguza bei za betri za radio ili mamilioni ya maskini nchini waweze kuzitumia kirahisi kwa radio na tochi zao.

Kujadili mashati na magauni ya kuvaa wakati tuko kwenye ndege tukielekea Ulaya au wakati tuko kwenye semina za kujadili posho ni kupoteza wakati na raslimali za taifa bure.
Hivi Watanzania hatuna cha maana cha kufanya kwa ajili yetu na wajukuu zetu?

Sikiliza maelezo ya Ubinafsishaji na maendeleo Lake Tanganyika Hotel Kigoma 1

Usipoamini shauri yako! Huyo mama sio mtu ni SANAMU

Huyu mwanaume akishangaa kwa karibu sanamu iitwayo "Mama na Mtoto" huko New Delhi katika uzinduzi wa tamasha la wasanii wa India. Wenzetu wapo kiwango cha juu maana utadhani ni mtu kweli kumbe ni sanamu. Sanamu zetu Tanzania nyingi hazionyeshi mfanano na mtu waliyemkusudia, wajifunze kwa hawa wa India wanafanyaje.

Huyu nae ameamua kusogelea kwa karibu sana lakini haibadiliki kuwa mtu BADO INABAKI KUWA SANAMU TU.

Polisi wa Colombia wateketeza mitambo ya Mihadarati

Askari wa kikosi maalum cha kupambana na dawa za kulevya wakiwa WAMELIPUA mitambo haramu ya kutengenezea dawa hizo huko Puerto Concordia, Colombia jana Jumatano January 25, 2012. Zoezi hilo lilikua ni kupambana pia na waasi wa FARC na kuharibu miundombinu yao, ambapo viwanda haramu 17 viliharibiwa, ndege 2, boti 22, kilo 692 za unga wa Coca na tani 13 za michanganyiko mbalimbali ziliharibiwa pia. Watu 10 walikamatwa kuhusishwa na tukio hilo

Helikopta mbili (Hii ya karibu na ile ya mbali) zikiruka juu ya anga la Puerto Concordia wakati wa zoezi hilo

Askari wa kikosi maalum cha kupambana na dawa za kulevya wakikagua mitambo haramu ya kutengenezea dawa hizo huko Puerto Concordia, Colombia

Kasheshe nzito apata Waziri Mkuu wa Australia

Waziri Mkuu wa Australia mwana mama Julia Gilad akisindikizwa mzobemzobe na wa askari na walinzi wake kutoka katika sherehe ya utoaji zawadi huko Canberra leo Alhamisi January 26, 2012. Alitolewa mbiombio mara baada ya kundi la kabila la  Aboriginal (watu wa asili wa nchi hiyo) kuvamia ukumbi. Muangalie hadi kiatu kimoja kimevuka. 

Mlinzi wake akijitahidi kumwepusha na hatari ya wavamizi hao wa Aboriginal. Kwanza alijificha ndani ya jengo kwa takriban dakika 20, kisha ndio ukafanyika mpango wa kumtorosha.

Tuesday, January 24, 2012

Soma habari hii, utashangaa sana!!

Mamba huyu alimkata mkono wa kushoto msimamizi/daktari wa wanyama huko Shoushan Zoo mjini Kaohsiung, Taiwan. Mamba huyo alipigwa risasi 2 akauachia mkono na madaktari walifanikiwa kuunganisha na mwili wa daktari huyo, mamba hakufa na daktari hakufa wote wanaendelea vema. Ni kweli imetokea, duniani kuna mambo.

Hata ulaya mazingaombwe yapo!

Wapita njia wakimshangaa msanii mwana Mazingaombwe wa kiJerumani Johan Lorbeer akining'inia hewani kwa kushika mkono wake ukutani huko Chemnitz mashariki mwa Ujerumani. Lorbeer alifanya mambo hayo wakati wa uzinduzi wa Tamasha la sanaa "Weltecho"